Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Na kuna mwingine anaitwa messenger of Allah ambaye aliongoza uporaji na mauwaji na kuoa vibinti under age hapo huwezi kupewa majibu na both side za wafia dini.

Huyo ndo naona hata kum discuss pointless, hata hajajaribu kujionesha kwamba ana consistency uone pa kumkamatia wapi.

In fact ana contradictions nyingi na kubwa kiasi kwamba mpaka kitabu chake mwenyewe kinakuambia ukikuta contradiction jinsi ya kuitatua ni vipi.

Kitabu cha mungu chenyewe kinakubali kuwa na contradictions.

Mungu gani huyo kama si wa maboksi.

Si bora mtu aseme tu Hail His Imperial Majesty Selassie I and him kingly character which stepped on the bomb and the bomb couldn't explode, tuiweke katika mythology ya Waafrika kama muujiza wa Selassie. Tujue mtu anayesema hivi kaamua kumchomekea mu Ethiopia tuliyemjua na kumuona amepigana dhidi ya ubeberu wa Mussolini kutetea historia na utamaduni wa muafrika

Angalau uongo wake utakuwa na justification ya ku neutralize white supremacy.

Leo waaafrika kibao wanamuangalia Muarabu na Myahudi.
 

Unajua huenda nikawa na maswali magumu sana kuliko wewe kuhusu huyu Mungu nnayemwamini lakini kwa uelewa wangu, mambo niliyoyaona, vitu nnavyoviona na kujifunza, bado hadi sasa hivi naamini uwepo wa Mungu licha ya hayo maswali.

Kwa wale wanaofikiri lengo langu ni kubishana au kushindana na Kiranga, Matola, Activister, CYBERTEQ na wengine wanakosea sana. Kwa ufupi ni kwamba hata kama leo hii Kiranga akasema kwamba Mungu yupo, haitasimamisha shauku yangu ya kutafuta majibu ya maswali yangu kuhusu Mungu nnayemwamini.

Ukifuatilia mijadala mingi ya wasomi, wanafalsafa, wachungaji, waumini, wasioamini uwepo wa Mungu, wanasayansi n.k utaona inajikita zaidi katika kuleta malumbano ya hoja za mantiki na kisayansi, sasa nnachojiuliza kama huyo Mungu anathibitishwa kwa watu kubishana kwa hoja tu, kwa kweli hata mimi simtaki na ndio maana narudia tena hata kama kila mtu atasema Mungu yupo haimaanishi itanifanya nisitishe kiu yangu ya kumtafuta Mungu.

Ikiwa Mungu anapatikana kwa kukubaliana kwa hoja tu, basi atakuwa ni watu wachache sana tena wenye taaluma, wanafilosofia, wanasayansi na wengine wenye upeo mkubwa wa kufikiri.

Mungu inabidi ajidhihirishe mwenyewe, Mungu wa kutetewa na wanadamu simtaki!
 
Last edited by a moderator:

Sasa mungu kajidhihirisha mwenyewe?
 
Last edited by a moderator:

Hh:thumbdown:
 

na mimi nangoja hicho, tatizo lenu nyie mnamdhihirisha baada ya kuona hawezi kujidhihirisha!
 
na mimi nangoja hicho, tatizo lenu nyie mnamdhihirisha baada ya kuona hawezi kujidhihirisha!

Sidhani kama umenipata vizuri mkuu, nimesema kazi yangu mimi sio kumdhihirisha Mungu, huyo atakua mungu dhaifu sana!

Na wala simtaki mungu wa kudhihirishwa kwa logical arguments, eti kama mungu anauwezo wote anaweza kutengeneza jiwe asiloweza asilolibeba? au mambo ya bang, sijui evolution, mara saa na mtengenezaji na vitu vinavyofanana na hayo. Huyo atakuwa mungu wa watu wachache sana tena wenye ufahamu na wasomi.

Kwa mtazamo wangu mimi, Mungu anatakiwa kuwa sawa kwa watu wote. Cha ajabu ukichukua watu wachache kutoka maeneo tofauti tofauti duniani ukawauliza Mungu ni kitu gani, utashangaa majibu utakayoyapata. Na hapo ndio nnaposema Mungu inabidi mwenyewe ajionyeshe uwezo wake kwa watu wauone na wasadiki kwamba yupo.
 
Naona hujayafuatilia vizuri niliyoyaandika kaka, naomba upitie tena.

Ni swali dogo tu, jibu lake ndiyo, kwa sababu hii, au siyo, kwa sababu hii.

Kama umeandika, nimesoma, sijaelewa, naweza kurudia kusoma mara elfu moja nisielewe.

Kwa sababu litu kimoja hichohicho kinaweza mumaanisha hivi kwako na vingine kwangu.

To London, "down" is the Antipodes.

To the Antipodes, "down" is London.

So discussion is due, in order to remove confusion.
 

Jambo la kwanza, nimesema huenda nikawa na maswali mengi na magumu juu ya huyu Mungu kuliko wewe.
Pili nikasema pamoja na hayo maswali, bado hadi sasa hivi imani yangu juu ya Mungu kuwepo inaizidi ile ya Mungu kutokuwepo.

Nikaendelea kwa kuongeza kwamba, hata kama watu wote watasema Mungu yupo (Nikataja baadhi ya members, na wewe ukiwepo) haitamaanisha ndio itakuwa mwisho wa kutafuta majibu ya maswali yangu kwa sababu simtaki Mungu wa kupatikana kupitia mabishano.

Mungu hana haja ya kutetewa au kudhihirishwa na watu, huyo atakuwa mungu dhaifu na siyo kazi yangu kumdhirisha au kumtetea, cha msingi kwangu nafikiri ni kusema kwa nini namini yupo.

Nikirudi kwenye swali lako,
Kama nilivyosema hapo juu, kwangu suala la uumbaji na uwepo wangu hapa duniani kwa uchache vinathibitisha uwepo wa Mungu na huenda ni baandhi ya vitu vinavyonifanya nibaki na imani hiyo licha ya maswali yangu mengi kuhusu Mungu.
 

Kwanini uwepo wako hapa duniani unathibitisha kuwepo kwa mungu?

Kivipi?

Na kwa nini uwepo wako uwe umetokana na mungu, na mungu tu? Si kingine chochote.

Tena kwa nini mungu huyo lazima awe mungu wako na si mwingine?

Kama una maswali magumu kuliko yangu, sitegemei ushindwe kuyajibu haya yangu rahisi.
 

duuh!:redface:
 

Ulinielewa niposema Mungu wa kupatikana kwa arguments simtaki? Siamini kuhusu uwepo wa mungu mwingine zaidi ya huyu nnayemwamini kwa sasa. Maswali yangu magumu sio kwako, ni juu ya Mungu na sio kwako.

Kama ulivyosema hapo juu, kila kitu kina maana tofauti kwa kila mtu. Kwako kama uumbaji na uwepo wako sio viashiria vya uwepo wa Mungu, kwangu vinamaanisha. Unataka kunirudisha kulekule kwenye mungu wa kupatikana kwa bang theory na evolution. Uthibitisho wa hicho kitu kingine haupo na ni dhaifu sana kuliko huu wa uwepo wangu na uumbaji kwa Mungu nnayemwamini.

Kwa hiyo wewe umejileta mwenyewe, kwa mipango na makusudi yako binafi na unajua mfumo na utaratibu wako wote wa kuwepo kwako hapa duniani? Kujua tu huhusu wewe mwenyewe ni topic nyingine.
 

Basically unachosema ni kwamba huna interest ya kumjua mungu.

Ndicho kiini kila unaposema mungu wa argument humtaki.

Halafu hapo hapo unaji contradict kwa kusema una maswali magumu kwa mungu.

Huwezi kuwa na maswali magumu kwa mungu bila ya kuwa na argument.

Inawezekana siyo tu humuelewi huyo mungu wako, bali pia hujielewi wewe mwenyewe unataka nini.

You are contradicting yourself.
 

Nikirudia tena kwamba hujanielewa sidhani kama ntakua nakosea.
Nimesema simtaki Mungu wa argument, ungeniuliza kivipi badala ya kusema najichanganya.
Sina haja ya kumjua Mungu kivipi wakati nimeshakwambia namwamini Mungu muumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo anayejidhihirisha mwenyewe?

Na nikasema mungu wa kutetewa na wanadamu simtaki.

Kama hujaelewa nilichokisema haimaanishi nnaji contradict.
 

Mkuu nimependa sana namna msimamo wako ulivyo

Kimsingi kama ulivyosema ni bora kila mmoja amtafute huyu Mungu mwenyewe bila kumuuliza mtu mwingine na ajiridhishe

Unaposhindwa kumuelewa Mungu na unakwenda kuuliza kwa watu kuwa Mungu ni nini/yupo au hayupo unakuwa huna tofauti na wale waumini wa dini wanaoamini kuwa bila mchungaji kuwaombea maombi yao hayawezi kufika kwa Mungu

Inaendaje kumuuliza binadamu wenzako kuwa Mungu ni nini/yupo/hayupo wakati milango atakayoitumia kueleza "uwepo" wake ni kama yako?

Kitendo cha kutarajia mtu akupe maelezo yatakayokuridhisha kuwa Mungu yupo ni tatizo

Kitendo cha kufikiri kwakuwa binadamu ameshindwa kumuambia binadamu mwingine namna Mungu alivyo ni ishara ya kutokuwepo Mungu nayo ni tatizo tena tatizo kubwa

Kila binadamu amtafute Mungu kivyake na kila mmoja atapata jibu
 

Sasa kama mtu anakuuliza, Mungu mwenye uwezo wote anaweza kufanya 2+2=6?
Au anaweza kuumba jiwe kubwa asiloweza kulibeba?

Kwa hiyo mimi Samaritan nikiweza kutengeneza logic za kutetea hizo sentensi na zikaonekana sawa ndio itakuwa uthibitisho wa Mungu? Very interesting, huyo atakua ni mungu wa kubadilika na wakutegemea watu wanauwezo gani wa kufanya mabishano. Ndio maana nikasema, kama naendelea kumwamini Mungu, haijalishi nani amesema yupo au hayupo, ntaendelea kumtafuta na kumjua zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Shangaa na wewe ndugu yangu

Watu tumepewa uwezo wa kufikiri na hatuutumii

Kama umeshindwa kumjua Mungu kwa milango yako mitano ya ufahamu na unakwenda kwa mtu mwenye ufahamu kama wako na pia anatumia milango mitano kama yako hapo utakuwa na tatizo kubwa sana

Kwanza utakuwa unadhani binadamu huyo ni mkuu kuliko wewe kwenye suala la kufikiri
Pili utakuwa umejiweka chini sana ki utu

Kama umeshindwa kumjua Mungu kwanini uende kuuliza watu kama wewe?

Unapotengeneza maelezo ya kumuelezea Mungu utakuwa unamuelezea Mungu wako wewe na huenda akawa sio halisi aliyeumba kila kitu

Binadamu hatujaweza hata kujua mwanzo wetu kwa kutumia sayansi
Sayansi imeshindwa kuthibitisha uchawi ambao kila uchao tunaushuhudia mitaani

Halafu binadamu huyu unatarajia aje akuambie kwa hakika kabisa Mungu ni 1,2,3,4 n.k?

Inabidi tujiulize sana

Mantiki ya kibinadamu inakataa kabisa binadamu kuwepo hivihivi tu halafu anakuja mtu anakuambia binadamu hajaumbwa au kuwekwa duniani na mtu huyo anasema anatumia mantiki,inashangaza sana!
 

Swali langu la kwamba as long as una maswali kwa mungu, huwezi kusema uko beyond argument, hujalijibu.

Aliye beyond argument hana swali. Anaamini tu.

Which I have no qualms about. Kwa sababu imani si ujuzi.

My beef is with those who say they know, or worse still, equate belief / faith with knowledge.
 

Sijaelewa sijakujibu sehemu gani mkuu,

Kutumia logical statements na kuelezea unazoziita contradictions za Mungu kwa mtazamo wangu sidhani kama zinadhihirisha uwepo wa Mungu.

Kwa mfano, mtu anakwambia kama Mungu ni mwenye upendo na muweza yote kwa nini amwache shetani, na kwa nini aruhusu mabaya yawapate wanadamu? au Mungu mwenye uwezo wote anaweza kufanya 3+6=7? Je, mtu akiweza kujibu au kuelezea vizuri hayo maswali kwa hoja ndio uthibitisho wa uwepo wa Mungu?

Mfano mwingine ni wa hizo porojo kwenye huu uzi, eti haya matukio ya vifo ndio viwe vitu vya kuonyesha namna wanavyomkufuru Mungu wanavyokufa vifo vibaya, kuna watu wamekufa vifo vibaya kuliko hao na hawakumkufuru Mungu hadharani na kuna watu wamemkufuru Mungu kupindukia na wamekufa softly. Hizi hoja nyepesi za kuonyesha uwepo wa Mungu siziafiki.
 

Nishatoka huko kwenye ku uphold argument kabisa. Umesema uko beyond argument, nimekubali.

Sasa sielewi kwa nini unarudi kurudia kusema uko beyond argument wakati mimi nishakukubalia kwamba uko beyond argument.

In fact ulichokisema, kwamba uko beyond argument, ndiyo perfect definition ya perfect faith.

Na mimi kwa kweli sipo interested na faith, because that is arbitrary and not fact based.

Faith does not need arguments, it allows someone to take anything as the truth without questioning.

Mpaka hapo nimekuelewa.

Tatizo linakuja unapojikanganya na kuanza kusema una maswali magumu kwa mungu kuliko mimi.

Ukishasema hutaki argument ili kumkubali mungu, maana yake mungu ni unquestionable.

Ukishasema una maswali magumu ya kumuuliza mungu, maana yake mungu ni questionable.

You are unwiqittingly taking two opposing positions at the same time and creating a contradiction.

Is your god questionable or unquestionable?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…