Mungu alifanya kisasi na mwanadamu
1 aliwaua wana wa israel jangwani
2 alishindwa kumsamehe adamu na mkewe bustanini
3. Alishindwa kuwasamehe watu enzi za nuhu na kuwaangamiza kwa gharika
4. Alishindwa kuwasamehe watu wa sodoma na gomolah na mke wa Ruthu kumgeuza nguzo ya chumvi
Japokuwa anadai yeye ni mwingi wa rehemu anasamehe dhambi zote na kufuru zote za wanadamu
Lakini ni mungu mwenye kisasi asiye na huruma kwa watu wake
Anasema mimi ni mungu mwenye wivu nawapatiliza mbali wana maovu wa. baba zao kizazi cha kwanza cha pili cha tatu na cha nne cha wanichukiao
maana yake baba alifanya dhambi mtoto ataadhibiwa na mjukuu ataadhibiwa na kitukuu kitaadhiwa ni hadi kizazi cha nne je hicho si kisasi?
Hamna kisasi hapo.
Adamu alishaambiwa,
"ukila tunda la katikati hakika utakufa"
Kipindi cha ghalika Mungu alishawaonya watu kuwa anachukizwa na atawaua wakosaji.
Sasa nani mwenye makosa hapo ?
Sodoma na Gomola wala usiwatetee
Huko Saudi Arabia mashoga wanachinjwa hadi leo, hii tabia haivumiliki, Mungu alishawaonya wakaasi.
Kuhusu kuangamia kwa Waisraeli jangwani, kumbuka Mungu alishawapa Amri kumi.
Mojawapo inasema "usichonge sanamu na kuiabudu"
Wao wakachonga sanamu na kuziabudu Musa alipokaa mlimani siku arobaini.
Watu elfu tatu wakaangamia.
Wengi sijui kwanini mnashindwa kuelewa ngoja niwape mfano.
Anayetengeneza gari anakupa maelezo kuwa,
Usiweke maji kwenye tenki la petroli.
La sivyo utaliua gari nk.
Mbona wenye magari mnazingatia hii tabia ?
Je ukikosea kuweka maji na ukaliuwa gari lako utamlaumu mtengeneza magari ?
Mungu amekuumba na amekupa masharti ili wewe uyafuate ili uishi vizuri.
Na amekuambia ukivunja masharti haya (amri zake) hakika utakufa.
Mungu anapo amua kumwua mwanadamu hatendi dhambi hata akikuwa kwa maji, moto, ugonjwa, ajali nk.
Kwani alipokuumba mlikubaliana uishi mda gani ? na ufe kwa kitu gani ?
Ukiona unaishi ujue unaishi sio kwa matakwa yako bali Mungu ndo anaye amua uishi hadi lini na akiamua anakuchukua mda wowote bila hiari yako na huwezi kumlaumu.
Mungu ni mwenye rehema kwasababu mtu ukimkosea amekupa muda wa kutubu.
Ukikaidi kutubu anakuangamiza kwa jinsi anavyoona yeye inafaa, sasa unamlaumuje hapo, si amesha kuambia mapema.
Wewe kama unaona unapenda kutenda dhambi na hutaki kutubu kama alivyokuagiza, basi mwombe Mungu akuuwe ili uiepuke adhabu ambayo yeye ataiamua juu yako baadae
Na kwasababu umeshazaliwa inakupasa utubu kwanza halafu umwombe akuchukue usijeanguka kwenye dhambi tena.
Ni kama chumba cha mtihani, ukishaingia basi ni lazima upate matokeo ya Zero au Pass.
Mwanadamu usinge wekewa sheria na adhabu na Mungu hii dunia isinge kalika.
(Angalia madai ya Mashoga)
Sio Mungu pekee hata wewe unasheria na adhabu ulizoziweka hapo nyumbani kwako.
Serikari nayo ina sheria na adhabu.
Mungu ndiye mwanzilishi wa sheria na adhabu.
Hebu ishi kwa kufuata sheria za Mungu. ndipo utakapoziona rehema na upendo wake, tena utafurahia maisha bila ghalama yoyote, ni raha kwa kwenda mbele milele daima.
Umesikia ?
Mungu amesema
hivi
"Asema BWANA ; lakini mtu huyu ndiye nitakaye mwangalia, mtu aliye myonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu"
Isaya 66 : 2
Hata hapo mtaani kwako kama hufuati sheria ndogondogo za mtaa, na ukaamua kuwaibia majirani zako, hakika watakuchoma moto na kukuuwa kabisa.
Sijui utamlaumu nani.
Fata sheria, hata huyo Lusifer anayekudanganya kuwa Mungu ni mwonevu, ana sheria zake, na ukimkosea anakuua vilevile. tatizo la Lusifer ni kuwa hana jambo la manufaa kwa wafuasi wake, ni kiumbe dhaifu kilicholaaniwa na Mungu.
Kama unataka haki ndugu yangu.
Inabidi ujitegemee.
Yaani ujiumbe mwenyewe,
Ujipe uhai na chakula,
Ujitengenezee dunia yako,
Ukae peke yako bila kiumbe kingine chochote,
Uwe mwenye nguvu za kujilinda na nguvu nyingine yoyote itakayotaka kukufisha.
Kama huwezi hayo fata Amri za aliye kuumba maana ndiye mwenye nguvu na wajibu wa kukulinda na kuamua uishi hadi lini
Pole kwa mfadhaiko.