Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Watu waliomkufuru Mungu wakafariki dunia

Hakuna sehemu kwenye msaafu kulikoandikwa Mungu alotengeneza dhambi. Sijui labda mie si msomaji sana wa vitabu vya dini wataalam watusaidie juu ya hilo japo kubishana juu ya ukuu wa Mingu si vyema.
 
Kwa tafsir yako hii inamaanisha nini?
Kwamba yesu ni Mungu au Malaika?
Pengine tuanzie hapo Yesu Ni Neno La Mungu(Neno Linaumba ), Yesu Ni Roho Wa Mungu, Yesu ni Masia, Yesu Ni Mkombozi. Yesu atakuja kuhukumu wazima na wafu. Huko vijiweni mnapodanganyana wakisikia haya watajua unaelekea wapi.
 
hivi kuna watu wanaomkashifu yesu kuzidi wakristo na wayahudi?..hivi we jamaa intanet unaitumia kuingia jf peke,maana ni kama vile hujui hasa what is going on.maandiko ya wakristo kwa mamilioni yapo online yanamkashifu yesu,kuna hadi picha zinamwonyesha yesu as a gay,zote source ni huko kwa nduguzo wazungu.kuna mabilioni ya article we google,lakini huwezi ona site toka kwa waislamu ikimpaint yesu kwa dharau.

Unajua talmud ya wayahudi inasema nini kuhusu yesu?..GOOGLE
Teh teh..Hizo fikra zinafaa huko kwa watu kila kitu "...nasikia,nasikia...". ukiwauliza umesikia wapi?Nimeambia na ....msomi aliyekubuhu sijui aliyebobea?Huko kubobea umepimaje?Wanaanza vita. Wewe kwa akili yako wakristu wanaokiri na kumshuhudia Kristu wanamkufuru?Itakuweje kwa wale wanaopoteza hadi uhai ili kumfunika na kumtoa ktk maisha ya binadamu? Pole.Kuna watu wameshamchagua shetani, wanalala na kuamka ktk levi wake.Ni ngumu sana kuwa watu wa maana. Ghaddafi is gone kwa style ya maneno aliyoongea UGANDA, Saddam is gone kwa Style ya babu yake, aliyejisifu kuwa aliwatawala wayahudi naye atafanya hivyo. Hitler nae kaondoka vibaya, km alivyokashifu Ukristu kuwa ni dini nyanya sana ktk vita.Bora ya watu duni waliofanikiwa kutawala dunia kwa vita.
 
Hao walimkufuru tuu mbona kuna wanaoshindana na MUNGU?
 
1. Mtengenazaji meli ya titanic.
Baada ya kutengeneza meli ya TITANIC, mwandishi wa habari alimuuliza ni kiasi gani ilikuwa salama, nae akajibu " Ni salama sana na haiwezi kuzama na hata mungu hawezi kuizamisha".
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu TITANIC

2.AZUZA (mwanamuziki brazil)
Alipokuwa kwenye show yake ndani ya jiji la Rio dejeneiro , alichukua sigara akaanza kuvuta, akachukua nyingine kisha akairusha juu na kusema " Mungu na hiyo yako , chukua na wewe uvute. Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, ambayo iliharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote.

3.Christina hewt (mwandishi)
Huyu alikaririwa akisema " Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya kama biblia, siku chache baada ya kusema maneno hay, mwili wake ulikutwa umeunguzwa moto ambao haijajulikana hadi Leo umesababishwa na nini.

4. John Lennon (muimbaji)
Wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari la gazeti la america alinukuliwa akisema " ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwas na hilo kwa kuwa Nina uhakika nalo. Huyu naye baada ya mda alikutwa amekufa nyumbani kwake

5. Tancredo neves (rais wa brazil)
Alisema kwamba endapo angeshinda kura laki tano katika uchaguzi mkuu Brazil na kuwa rais , hata mungu asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa akapata kura zaidi ya laki tano akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa akafariki dunia.

Kibinadmu ni kweli kuna makosa hasa unapojikweza dhidi ya mwingine haijalishi ni mwenzako ama laa!

Hata hivyo habari hizi za vifo tajwa hapo juu wala sioni uhusiano wavyo na kukufuru kwao kama msemavyo.


Mbona hata hao wanaoitwa mitume wa Yesu/Mungu wengi wao walikufa vifo vya uchungu sana na pengine kuliko hata hao?

Tazama hapa chini.

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA,

1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Marko
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Luka
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

6.#Yakobo
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe. Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadei)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

NOTE:
13. #Thadayo (au Mathia) ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka (A.D).

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.
 
Mtoa mada;
Ingekua fair ungeleta pia na wale waliomsifia Mungu Wakapata kuishi milele.
 
Ngoja nifute kauli kabla Sir God hajamwelekeza ziraili pande hizi.

Nimekosa mimi, nimekosa mimi Nimekosa sana. Ee Mungu nihurumie na unisamehe.

Amina.
Yaan unaogopa kufa[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Mtoa mada;
Ingekua fair ungeleta pia na wale waliomsifia Mungu Wakapata kuishi milele.
Sio nkuishi milele bali sema waliobarikiwa utawaona ni wengi sana.
Kwa mfano utaona wale waliomwamini Yesu namna walivyobarikiwa mfano kuponywa vilema, kuona kwa vipofu, kusikia kwa viziwi yapo matukio mengi sana.
 
1. Mtengenazaji meli ya titanic.
Baada ya kutengeneza meli ya TITANIC, mwandishi wa habari alimuuliza ni kiasi gani ilikuwa salama, nae akajibu " Ni salama sana na haiwezi kuzama na hata mungu hawezi kuizamisha".
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu TITANIC

2.AZUZA (mwanamuziki brazil)
Alipokuwa kwenye show yake ndani ya jiji la Rio dejeneiro , alichukua sigara akaanza kuvuta, akachukua nyingine kisha akairusha juu na kusema " Mungu na hiyo yako , chukua na wewe uvute. Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, ambayo iliharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote.

3.Christina hewt (mwandishi)
Huyu alikaririwa akisema " Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya kama biblia, siku chache baada ya kusema maneno hay, mwili wake ulikutwa umeunguzwa moto ambao haijajulikana hadi Leo umesababishwa na nini.

4. John Lennon (muimbaji)
Wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari la gazeti la america alinukuliwa akisema " ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwas na hilo kwa kuwa Nina uhakika nalo. Huyu naye baada ya mda alikutwa amekufa nyumbani kwake

5. Tancredo neves (rais wa brazil)
Alisema kwamba endapo angeshinda kura laki tano katika uchaguzi mkuu Brazil na kuwa rais , hata mungu asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa akapata kura zaidi ya laki tano akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa akafariki dunia.
Hivi JF imeanza upotoshaji muda mrefu tu..... Kuna story hapo nimejaribu kuzifanyia uhakiki.
2. Huyo AZUZA hakufa kwa lung Cancer bali kwa UKIMWI sasa sijui hizi propaganda mnazitoa wapi.
4. John lennon hiyo kauli aliifuta tokea mwaka 1966 na akaomba radhi alafu ilichukua miaka 14 baadae ndio yeye akafa sasa sijui kwanini mtoa mada anataka kuaminisha watu uongo humu alafu wana JF badala ya kuhoji wanashabikia tu propaganda.

5. Tancredo Neves hakufa siku moja kabla ya kuapishwa alikuwa anaumwa tu muda mrefu sana hata kabla hajagombea urais.... Hivyo operation yake ilipangwa kabla ya siku ya kuapishwa hivyo akamuachia madaraka kwa muda makamu wa Rais na yeye Neves alifariki siku 39 baadae na sio kama mtoa mada anavyopotosha..... By the way hakuna ushahidi kuwa aliwahi toa hiyo kauli maana nimesaka sana kote hakuna mainstream media inayokubali hili jambo sasa cjui mtoa mada katoa wapi hii propaganda.

Anyway labda nitoe rai kwa dini zote humu kuwa Mungu ni wa neema kama angekuwa anakasirika kisa watu kumsema vibaya sidhani kama wote tungekuwa hai.... Maana kuna wanasiasa wanaiba kura ila wanatoa shukrani kwa MUNGU kushinda urais ila wapo hai, kuna watu wanashinda kwa waganga ila jumapili wanaingia kanisani, kuna watu wanakashifu maneno ya Mungu hasa ukikuta mijadala kati ya waislam na wakristu kila mmoja anakashifu kitabu cha mwenzie ila sijawahi sikia mmoja wao kwenye mabishano akafa. Tena nafikiri Mungu watu wa hivyo ndio huwa anawaacha waishi muda mrefu ili waone makuu yake na wabadilike na sio kuwaua tu sasa nashangaa kuna watu wanashabikia mtu anayemkashifu Mungu/Allah akifa ilihali maandiko yanasema mmoja ya wenye dhambi akiokoka basi mbingu nzima inashangilia

Tubadilike wanaJF tuwe na positive attitude hata kwa wale wasio wa upande wetu wa kiimani.
 
Mfano Kanye west amekuwa akimkufuru Mungu kwa miaka mingi sasa ila hajafa


Na hapa chini akiperform ngoma yake ya IAM A GOD.... Yaani MIMI NI MUNGU..... Hapo bila kusahau anajiita Yeezus na kammock sana tu Jesus kwenye hiyo ngoma


Ila toka aimbe ni miaka kibao imepita ila bado yuko hai ila kuna mamilion waliosimama kwenye imani zao ila wamekufa.....!!!
 
Kama mungu wako alikufa na akatundikwa na nepi ili nyie msiwe na dhambi unashangaa binadamu kufa akipigania haki za wengine.
Ubishi kama huu ndo unawarahisishia wapinga uwepo Wangu,yaan kila mtu ana Mungu wake....[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom