Sasa kama Mungu wangu anajitetea mwenyewe, na anajidhirisha mwenyewe, na maswali yangu namuuliza mwenyewe. Huyo unayetaka nikwambie kwamba ni questionable au sio questionable namtoa wapi? Kama unamaanisha huyu Mungu nnayemwamini mimi, rahisi sana muulize kwa sababu anaweza kujibu mwenyewe.
Mimi nakuuliza wewe
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Je, kama mtu akatoa logic, argument au maelezo yoyote kuhusu Mungu kiasi cha wewe kuridhika, itakua ni sababu ya wewe kukubali uwepo wa Mungu?
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Bado hujajibu swali kama mungu wako ni questionable au si questionable.
Tofauti kati yako wewe na mimi ni kwamba mimi natafuta majibu ya maswali ya msingi, na wewe unajifurahisha unavyotaka wewe kwa imani yako tu.
Swali kama "is god questionable" ni swali la msingi kabisa lisilojali any special circumstance.
Kwa sababu mungu wenu mnamsema ni primary mover, haifai kuuliza maswali ambayo si fundamental, hivyo suala zima la "inategemea" linamfanya mungu wenu awe kama mdoli ambaye anategemea mabetri.
Nikiuliza mdoli huyu anaimba, naweza kujibiwa "inategemea kama ana betri".
Sasa mungu naye anategemea nini?
Swali lako la kwamba kama nikipewa logic kuonesha mungu yupo nitakubali ni zuri sana.
Linaonyesha uongo na kujikanganya kwamfumo wa Judeo-Christian.
Kwa msingi, kama mtu ninayeongozwa na logic natakiwa nikipewa logic ya kuonyesha kwamba mungu yupo 100% bila shaka, natakiwa nikubali.
Si nimepewa logic ninayotaka?
Lakini hapo hapo kuna kitu kinachoitwa "Catch 22".
Mungu wenu alivyoandikwa na kuwa designed, ni mungu ambaye hahakikishiki.
Kwa sababu, ukiweza kutumia logic na ku prove kwamba mungu yupo 100%, utakuwa tayari umekwishaweza kutumia logic ku prove kwamba mungu hayupo 100%
Kwa sababu kwa jinsi mlivyomsuka mungu wenu ni kwamba, hawezi kuwa contained na system yoyote ile, kwa sababu yeye ndiye muunda systems zote.
Kwa hiyo mpaka hapo utaona ni jinsi gani ujanja ujanja uliotumiwa kumsuka huyu mungu umemfanya awe katika nyanja za imani daima, hakuna mtu atakayeweza kuthibitisha kwamba mungu yupo.
Kwa sababu ukithibitisha tu kwamba mungu yupo, kuthibitisha huko kwamba mungu yupo kutakuwa kimsingi ni kuthibitisha kwamba unayemsema mungu si mungu, kwa sababu ameweza kuthibitika kwa mfumo fulani.
Matahalani, ukiweza kupiga hesabu mpaka ukafikia sehemu hesabu zikakupa uhakika wa 100% kwamba mungu yupo, huyo uliyemthibitisha atakuwa si mungu tena, kwa maana kaweza kuthibitishwa 100% na hesabu, amekuwa contained na kanuni za hesabu.
This goes in line with your argument kwamba hutaki mungu wa argument (ingawa hata ukisema hutaki mungu wa argument ushachagua kwenda na mungu wa argument kwamba mungu kapita level ya argument, kwa hiyo essentially bado unaye mungu wa argument, the argument being god transcends all arguments)
Kwa hiyo si tu unakwepa swali la "is your god questionable" bali pia tunaona unajidanganya kwamba unamtambua mungu aliye beyond arguments wakati kumtambua mungu huyo ni to make an argument that god is beyond arguments, and in making that argument, you are dragging god in the realm of non-argument argument like a passive aggressive maniac.