Ulitafuta wapi?
Mungu wetu yupi?
Wa wapi?
Kitendo tu cha kutafuta Mungu wa fulani ni kosa utawezaje kuthibitisha wakati unatafuta Mungu wa fulani?
Kila nguvu ina kanuni,Mungu nae ni hivyo pia,ulifuata kanuni gani kumtafuta huyo uliyemtafuta?
By the way,kama ulimtafuta Mungu wa fulani na ukaona kama ulivyoona kwanini unadhani ni tatizo la huyo Mungu na sio lako?
Usipoliona embe lililodondoka mtini hilo ni tatizo la macho yako kutokuona au ni la embe?
Embe linaonekana na wengine wewe unadai halionekani huoni tatizo ni lako?
Huyo Mungu uliyemtafuta na hukumuona huenda ni tatizo lako maana wengine hao "wenye" huyo Mungu wanamuona lakini wewe humuoni inawezekana hujafuata kanuni zitakazokufanya umuone
Lakini pia kama amejicontradict huoni tayari unakubali yupo?
Kisichokuwepo kinawezaje kujicontradict?
Na huyo Mungu uliyemtafuta ulijuaje kuwa unamtafuta Mungu na sio kitu ingine?
Unaanza kea ku assume kwamba mungu yupo.
Unaanza ku assume kwamba embe imeanguka mtini hata kabla hujachunguza kama imenunuliwa gengeni na kuwekwa chini!
Nimemtafuta mungu, pande nne za dunia
Nimestuka marungu, mbuzi mee kwa gunia
Mungu huyu ni mzungu, na mtawa jichumia
Na ni kiweka ukungu, wa nakawa kuumia
Mungu huyu mungu gani asiye kwenye mizani?
Kajifichapo kwa ndani? Yupo bara au pwani?
Vitabu vya ugizani, vitawale ukinzani?
Mungu huyu baalani, siwezi weka manani
Mungu chaka la ujinga, pu.mbavu ndani ya mimba
Hata kama Mmachinga, hilo naliweka dimba
Vipi leo mnaimba, kwamba sungura ni simba?
Mungu huyu tampinga, Pangani na Tandahimba
Mungu haendi somoni, kajificha kama mwali
Ushungi hata pomoni, kama binti wa liwali
Ulevi huu komoni, au viloba vikali?
Mungu huyu mdomoni, si kweli wa ilhali
Mungu huyu ni muumba, au bakaji Maumba?
Anavyoua wachumba, tendawili atufumba?
Na kulaani mgumba, hizo rehema mtumba?
Mungu huyu kajidunga, au teja kamtunga?
Mungu anajihadaa, kwa haiba ushujaa
Huku atupa mabaa, kutujazia majaa
Wamsubiri masaa, arudi bila mawaa
Wajitakia balaa, kushinda kutwa salaa
Mungu chungu nungunungu au punguani pungu?
Mboni kajifunga fungu, lisiloisha ukungu?
Mungu huyu Sungusungu, aso silaha ya rungu?
Mboni ashindwa uzungu, kutuweka kwenye gundu?