Watu wameendekeza tamaa kwa kisingizio cha usasa

Watu wameendekeza tamaa kwa kisingizio cha usasa

Baki hapo hapo mkuu, kuendekeza usasa ni kujirudisha nyuma kiutamaduni na sio maendeleo

Wapewe heko wamang'ati, maasai, wahadzabe kwa kuonesha jitihada za maendeleo ya kiutamaduni

Pia walaaniwe wasanii wa kizazi kipya, bongo movies na wahuni wote kwa kutuletea mila na tamaduni za kigeni zinazopoteza asili yetu
Asili yako inakusaidia nini mzee?? Wamasai wanafaidika nini na umasai wao??
Faida ya kulinda huo utamaduni wako ni ipi??
 
Asili yako inakusaidia nini mzee?? Wamasai wanafaidika nini na umasai wao??
Faida ya kulinda huo utamaduni wako ni ipi??
Kwani maendeleo maana ake ni nini mkuu?

Ukijua maana ya maendeleo hiyo ndio faida yenyewe
 
Jibu swali, nani kwakwambia uwe mzungu na hiyo ngozi yako nyeusi
Kwanini asa na ngozi yangu nyeusi nione maendeleo ni kuiga mila na tamaduni za kizungu

Mila na tamaduni zangu ndio maendeleo yangu
 
Sawa mkuu kaa na mila zako.
Mnaoiga mnatuharibia kizazi chetu tunawaasa mbadilike tufuate mila na tamaduni zetu sote kwa pamoja ili kukijenga kizazi chema chenye maendeleo ya kitamaduni na kimaadili
 
Mfano ? Kwamba Tanzania / Afrika ni Kisiwa ? Developing countries haziendelei sababu ya marginalization na kunyonywa pamoja na upuuzi wa watawala wa huku na tamaa za kuweza kuuza na kugawa rasilimali kwa mgongo wa vijizawadi...; Hakuna eneo ambalo ni kisiwa wala hakuna teknolojia ya ulaya per se bali teknolojia inachukuliwa sehemu moja na kuboreshwa..... (If I have seen further is by standing on the shoulders of the Giants) mambo ya industrial revolution na vitu kama internal combustion engine zimeitoa dunia katika hatua moja mpaka nyingine ni kwa thinkers kufikiria na kuboresha jambo ambalo linamtoa mwanadamu kama kiumbe katika hatua moja mpaka nyingine ya kupambana na mazingira....

Kuhusu maadili / fashions sio kwamba zinapingwa hapa tu hata kule / popote kuna watu conservative ambao wanaona kwamba vazi hili halifai..., kwahio kwa watu wanaokwenda ufukweni Bikini kwao inavaa sababu hawawezi kwenda kule na baibui (vyote ambavyo sio mavazi ya muafrika asilia) lakini hata hio bikini huwezi kusema aliigundua mtu wa kule sababu vazi la kufunika sehemu za siri na kwenye kifua lilikuwepo tangu enzi na enzi...

Uhuru na Haki ni nini ?

Kwamba vice versa ya uhuru na haki ndio asilia yetu na ni bora kuliko uhuru na haki ya mtu ? Kwamba enzi za utumwa zilikuwa bora kuliko sasa hivi ambapo mtu hauna haki ya kumiliki binadamu mwenzako ?

Machifu ni kwamba kuna sehemu ilikuwa mtu unakuwa kiongozi sababu ya uzao wako (na kwa taarifa yako hii haikuwa Afrika tu bali duniani kwa ujumla) sasa unaona hio ilikuwa bora ?!!!

Kwahio ulaya ni ushoga ? Na vilevile narudia tena mara nyingine sio kweli kwamba civilization ilianzia ulaya..., kwahio mkuu wewe amini unachoamini ila usipindishe facts kujaribu ku-paint picha unayotaka wewe wakati mambo hayapo hivyo yalivyo....

Hivi unaujua hata UK Allan Turing Mmoja wa Magwiji wa Hesabu na alieyesaidia sana katika mambo ya Artificial Intelligence alikufa vipi kutokana na kuwa Gay....

Turing was prosecuted in 1952 for Homosexual Acts. He accepted hormone treatment with DES, a procedure commonly referred to as Chemical Castration, as an alternative to prison.

Prosecution hio ikapelekea mwisho wa siku kuondoa uhai wake....; Kwahio mkuu wewe unachosema kwamba utamaduni wa ulaya ni ushoga nashindwa kukuelewa issue ni kwamba hawawi prosecuted kama wewe unavyotaka labda wapigwe risasi au kuuliwa au kuchinjwa (jambo ambalo hata mimi binafsi sitaki kuishi kwenye eneo la watu kuchukua sheria mkononi) mfano mtu akiiba sijui akatwe mkono au mwingine apofushwe macho n.k. (sababu mataifa ya hivyo pia yapo)
Historia chungu
 
Back
Top Bottom