Uchaguzi 2020 Watu wamefaidi maendeleo haya. Tupaze sauti

Uchaguzi 2020 Watu wamefaidi maendeleo haya. Tupaze sauti

dndagula

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
1,602
Reaction score
1,650
Nianze kwa kusema wazi kuwa maendeleo ya watu huwezi kuyatenganisha na maendeleo ya vitu kwa namna yeyote ile wazungu wanasema (the are interwovened) hivyo maendeleo yaliyofanyika kwa kuzingatia mahitaji ya watu na tumefaidi na tunapaswa kupaza sauti zetu dhidi ya wanaopotosha ni pamoja na:
1. Elimu bure
2. Mikopo ya elimu ya juu
3. Ruzuku ya mbolea na viatilifu
4. Wajasliamali na biashara ndogo ndogo uhuru wa biashara bila ya bughudha ya mgambo
5 Ukarabati wa mashule na ununuzi wa madawati
6. Ujenzi wa vituo vya afya, zahanati hospitali za wilaya na kupandisha hadhi za mikoa kuwa za Rufaa
7. Vifaa vya kisasa na madawa mahospitali yote yakiwemo ya rufaa
8. Kurahisisha usafiri wa majini na angani kwa wananchi kwa Matengenezo ya meli na ununuzi wa ndege
9. Kurahisisha usafiri wa reli kwa wananchi kwa kufufua usafiri huo ulio na gharama nafuu
10. Usafirishaji wa barabara kwa ajili ya mazao na kupunguza msongamano kwa kujenga flyovers kupunguza muda wa barabarani etc ongezeeni.

Sasa nauliza je haya maendeleo hayagusi maendeleo ya watu kwa vile ipo miradi ya maendeleo iliyozalisha ajira na nyingine kuwapatia maji watanzania au umeme hadi vijijini na kuwarahisishia maisha watanzania.

Pamoja na changamoto kadhaa za maendeleo bado tumeona utashi wa kisiasa wa JPM kutuletea maendeleo halisi watanzania.TUWE WAKWELI TUACHE SIASA NA TUPAZE SAUTI ZETU KUTETEA HILI VINGINEVYO WANAOPINGA WANAONA WIVU AU HADAA.TUTAFAKARI SOTE.
 
JamiiForums1130837909.jpg
 
upuuzi toka kwa mpuuzi moja, kama hamna ajira, hamna haki, hamna Uhuru basi jua hayo mengine ni pumba umewanyang'anya kuku haki yao
 
Usalama na uhuru wetu vimekuwa mashakani kipindi cha miaka yake 5.
 
Serikali ipi ya Tanzania haikuwahi kufanya haya? Na hii iliyofanya haya haikuwa wajibu wake?

Sisi tunataka haki na uhuru siyo mtu wa kutufokea kama vile nchi hii ni mali yake binafsi.
Angeweza kufanya yote hayo bila kusimamia utekaji wa watu, kujaribu kuua wapinzani wake, kutofanya ubaguzi kwa watu wa kanda tofauti, kutopendelea maeneo na watu falani fulani
 
Si kweli watu tunakula bata kama kawa nadhani unamaanisha Uhuru wa mashoga
Sasa wewe mtu kama Mo anatekwa na wanaomteka serekali inashindwa kuwabaini na kuwakamata. Hebu niambie "kajampanani" yeyote wakikuamulia nani wa kuwazuia?

Mtu prominent kama Lissu anapigwa risasi na watu ambao serekali inashindwa kuwabaini na kuwakamata, kwa akili yako unaamini wakikutaka wewe itachukuwa sekunde? Bado unafikiri unayo amani? Think broadly.

"Kama wanaitenda vile miti mibichi na mikavu je?.
 
October 28 unachukua unaweka waaa kwa kwa Rais Magufuli na Ccm

Ushindi kwa Rais Magufuli ni 98%
 
Nianze kwa kusema wazi kuwa maendeleo ya watu huwezi kuyatenganisha na maendeleo ya vitu kwa namna yeyote ile wazungu wanasema (the are interwovened) hivyo maendeleo yaliyofanyika kwa kuzingatia mahitaji ya watu na tumefaidi na tunapaswa kupaza sauti zetu dhidi ya wanaopotosha ni pamoja na:
1. Elimu bure
2.Mikopo ya elimu ya juu
3.ruzuku ya mbolea na viatilifu
4.wajasliamali na biashara ndogo ndogo uhuru wa biashara bila ya bughudha ya mgambo
5 ukarabati wa mashule na ununuzi wa madawati
6. Ujenzi wa vituo vya afya, zahanati hospitali za wilaya na kupandisha hadhi za mikoa kuwa za Rufaa
7.vifaa vya kisasa na madawa mahospitali yote yakiwemo ya rufaa
8. Kurahisisha usafiri wa majini na angani kwa wananchi kwa Matengenezo ya meli na ununuzi wa ndege
9.kurahisisha usafiri wa reli kwa wananchi kwa kufufua usafiri huo ulio na gharama nafuu
10.usafirishaji wa barabara kwa ajili ya mazao na kupunguza msongamano kwa kujenga flyovers kupunguza muda wa barabarani etc ongezeeni.
Sasa nauliza je haya maendeleo hayaguzi maendeleo ya watu kwa vile ipo miradi ya maendeleo iliyozalisha ajira na nyingine kuwapatia maji watanzania au umeme hadi vijijini na kuwarahisishia maisha watanzania. Pamoja na changamoto kadhaa za maendeleo haya bado tumeona utashi wa kisiasa wa kutuletea maendeleo halisi watanzania.TUWE WAKWELI TUACHE SIASA NA TUPAZE SAUTI ZETU KUTETEA HILI VINGINEVYO WANAOPINGA WANANAONA WIVU AU HADAA.TUTAFAKARI SOTE.
Mtapigiwa kura na madaraja.
 
Mbona umeyataja machache?? Ngoja nikuongezee mengine.

Utekaji.
Uuwaji.
Kufilisi Wafanyabiashara.
Kupora korosho za wakulima.
Kuharibu bei za mazao.
Kudhulumu mafao ya wastaafu.
Kuwanyima wafanyakazi nyongeza zao.
Wahitimu wa vyuo vikuu wamekandamizwa na marejesho ya mikopo.
Kuminya Uhuru wa vyombo vya habari
Rais kuwa mbabe, dharau, shobo na nyodo.
Na mengine mengi. Nimechoka kuyaorodhesha.
 
Serikali ipi ya Tanzania haikuwahi kufanya haya? Na hii iliyofanya haya haikuwa wajibu wake?

Sisi tunataka haki na uhuru siyo mtu wa kutufokea kama vile nchi hii ni mali yake binafsi.
Angeweza kufanya yote hayo bila kusimamia utekaji wa watu, kujaribu kuua wapinzani wake, kutofanya ubaguzi kwa watu wa kanda tofauti, kutopendelea maeneo na watu falani fulani
Uhuru na haki gani unataka iwapo sasa hivi unasema lolote hapa jamii forum na mahakama zinatimiza wajibu wake. Pia sasa hivi usalama wa raia upo ujambazi umedhibitiwa. What else do you want?Hata hivyo Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka duniani kote.
 
Back
Top Bottom