Usaili wa kuandika katika kada ya afya umefanyika Septemba 3, 2024 nchi nzima ili kuwapta wataalam wa afya watakaojaza nafasi 9, 483 za ajira.
Wakati usaili huu ukiwa unaendelea ilisambaa video mtandaoni ikionesha binti akiwa anasukumwa na Mwanaume akiwa ameshika karatasi kati ya watu wengine walioshika karatasi ndani ya chumba, huku Watu wanaosambaza video hiyo wakidai ni tukio lililotukia kwenye moja ya vituo vya usaili, Tazama( hapa na hapa)
Ukweli ni Upi?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image ili kufahamu uhalisia wa video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya tukio lililotokea kwenye moja ya maeneo yaliyofanyika usaili katika kada ya afya nchini.
Tumebaini kuwa video hiyo si ya Tanzania na haihusiani na usaili katika kada ya afya, video hiyo ni ya Congo na iliwekwa mtandaoni tarehe Agosti 26, 2024 (Tazama hapa) na kuendelea kusambaa, (tazamahapa) ikionesha tukio lililotokea Congo DRC.
Ufuatiliaji wa kimtandao unaonesha tukio hili lilimuhusisha binti wa chuo chaISTA Kolwezi lundi (l’Institut Supérieur des Techniques Appliquées (ISTA)) ambaye alishambuliwa na mwalimu akiwa kwenye mtihani Mwalimu anafahamika kwa jina la Tshipamba Kabwe.
Barua ikionesha kusimamishwa kazi kwa mwalimu aliyemshambulia mwanafunzi huyo
Kwa kuwa aliyepigwa ni Mwanamke basi imeibua HISIA (napenda kuziita za kinafki).
Kauli utakayoitoa kwa mtu mwenye uwezo mdogo wa kuhimili matusi, kejeli na vitimbi vya maneno ya shombo kali ni chachu ya kujiletea matatizo.
Ikumbukwe kulingana na Video huyo Dada ana shida sana.. em tuweke UNAFKI pembeni.. tuangalie hiyo footage kwa jicho la ndani zaidi.
Swala la kupigwa ni mtambuka.. ishu ni nini kilipelekea yote hayo? Je wewe ungeweza kuhimili? Watu wapo desperate na mambo mengi.. unajua anapitia nini? Sometimes hiyo ni catalyst ya watu kufanya mauaji ya kikatili... mtu ana mambo mengi kayahifadhi moyoni ww unakuja kumtukana.
Mnachanganya watu kwenye mihemko, Hata angekuwa mwanaume some of us tunge comment vile vile.
Kwenye social ladder kuna mwenye advantage na mwenye disadvantage, kwenye hili mwenye privilege ni huyo mbaba, aliyeko kwenye disadvantage ni huyo kasichana.
Raia akimchokonoa polisi, polisi akampiga raia, watu wote wenye utimamu wa akili wangesema polisi ana makosa, sababu alikuwa na njia halali za kushughulika na huyo raia mchokonozi, instead akaamua kumpiga,