SI KWELI Watu wamepigana wakati wa Usaili wa Kada ya Afya nchini Tanzania

SI KWELI Watu wamepigana wakati wa Usaili wa Kada ya Afya nchini Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Watu wanachapana mikono huko, yaani ni noma sana.

Screenshot_20240909-085354_1.jpg



 
Tunachokijua
Usaili wa kuandika katika kada ya afya umefanyika Septemba 3, 2024 nchi nzima ili kuwapta wataalam wa afya watakaojaza nafasi 9, 483 za ajira.

Wakati usaili huu ukiwa unaendelea ilisambaa video mtandaoni ikionesha binti akiwa anasukumwa na Mwanaume akiwa ameshika karatasi kati ya watu wengine walioshika karatasi ndani ya chumba, huku Watu wanaosambaza video hiyo wakidai ni tukio lililotukia kwenye moja ya vituo vya usaili, Tazama( hapa na hapa)

screenshot-2024-09-03-at-23-08-32-devotatweve-on-x-inadaiwa-kafanyiwa-hivi-wakati-wa-usahili-m-png.3086321
Ukweli ni Upi?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image ili kufahamu uhalisia wa video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya tukio lililotokea kwenye moja ya maeneo yaliyofanyika usaili katika kada ya afya nchini.

Tumebaini kuwa video hiyo si ya Tanzania na haihusiani na usaili katika kada ya afya, video hiyo ni ya Congo na iliwekwa mtandaoni tarehe Agosti 26, 2024 (Tazama hapa) na kuendelea kusambaa, (tazama hapa) ikionesha tukio lililotokea Congo DRC.

Ufuatiliaji wa kimtandao unaonesha tukio hili lilimuhusisha binti wa chuo cha ISTA Kolwezi lundi (l’Institut Supérieur des Techniques Appliquées (ISTA)) ambaye alishambuliwa na mwalimu akiwa kwenye mtihani Mwalimu anafahamika kwa jina la Tshipamba Kabwe.

1725399147413-jpeg.3086332

Barua ikionesha kusimamishwa kazi kwa mwalimu aliyemshambulia mwanafunzi huyo​
Whatever the case haikutakiwa kuwa hivyo.

Lakini na nyie wanawake ifike wakati mjifanyie tafakari maneno mnayotamka kwa watu wengine aidha mpenzi, mume au swahiba kazini kuna muda mtu anashindwa kuhimili yale maneno mwisho yanatokea ya kutokea. Anakuja kulaumiwa na tutamlaumu kweli mtendaji wa tukio kama huyo jamaa hapo. Wote tujifunze kulinda midomo yetu sio kulopoka lopoka tu.
Sawa mkuu
 
Tunampa hiyo benefit! Eleweni hawa watoto wako katika hali gani.

Baba mzima, mtumishi wa umma, ana mshahara, ana marupurupu anashindwa kumanage stress ya kamjinga kamoja kalichotukana?

No wonder tuna maendeleo ya namna hii kama watumishi ndio hawa 🗑️🚮
Mkuu unaweza kuta kazi yenyewe ni stress tosha kwa kuzingatia mazingira kama hayo unayoona. I believe in judgement everything should be put fairy not in favor to benefit the less
 
Tunampa hiyo benefit! Eleweni hawa watoto wako katika hali gani.

Baba mzima, mtumishi wa umma, ana mshahara, ana marupurupu anashindwa kumanage stress ya kamjinga kamoja kalichotukana?

No wonder tuna maendeleo ya namna hii kama watumishi ndio hawa 🗑️🚮
Binti umesota mtaani, ajira ngumu, umepata bahati kuitwa interview unaropoka maneno ya kijinga kijinga tena kwa kiongozi wako.

No wonder tuna maendeleo ya namna hii kama waajiriwa wemyewe ndio hawa🚮🛃
 
nimepatwa na hasira, nmejikuta namhurumia dada tuu... ningekuwepo huyo msimamizi ningemsubiria atoke 😕 nje nimpe mkono asingeamini yaani
 
Si ndio alitakiwa akashitaki? Hapo ameshitaki au amehukumu.

Punguza mihemko hapo nani yuko katika position ya kupoteza kisheria?

Usifikiri hapa kuna mtu nashindana nae au najaribu kutunishiana misuli na mtu.
Wote kisheria wanapoteza
Mmoja kashambulia, mwingine amedharirisha kwa lugha chafu
 
Hakuna mtu huwa anapewa ruhusa ya kupiga mtu au kutukana mtu ila lazima tukumbushane kwamba ukiwa kiongozi haimaanishi kwamba Hasira na hisia zako zinakufa Hapana,

Ndomaana ni vibaya kutukana mtu au kupiga mtu lakini kuna namna huwez kudhibiti hisia haswa pale tukio linapogusa Utu wako wa ndani,

Ndomaana hata Rais Samia juzi alisema "Kuna Mbwa mpumbavu anabwekea maendelea yetu" kauli hii si sahihi kutoa kiongozi lakini baada ya kupata Hisia za hasira alishindwa kujizuia na kuitoa.... Hivyo kuna namna huwezi kuzuia baadhi ya maneno au matukio haswa pale Utu wako wa ndani unapoguswa.

Naam, huu ndio uhalisia wenyewe.

Haswa hawa viumbe ndio wenye kauli mbovu sana pasi na kujali utu wa mtu.

Kuna namna tujiwekee mipaka wenyewe heri kumuadabisha ili wengine waweze kuheshimu.
 
Tatizo wazazi tumesahau wajibu wetu kuwafundisha watoto nidhamu na adabu, hata wale waliofundishwa adabu bado wengi ni vichomi. Inasikitisha, hasa kama mzazi kuona binti yako anapitia udhalilishaji wa namna hiyo wakati akiwa na msongo wa kupata ajira.

Japo, huyo mwamba alitakiwa kutawala hisia zake, haijalishi aliambiwa kitu gani.
 
Binti umesota mtaani, ajira ngumu, umepata bahati kuitwa interview unaropoka maneno ya kijinga kijinga tena kwa kiongozi wako.

No wonder tuna maendeleo ya namna hii kama waajiriwa wemyewe ndio hawa🚮🛃
Huwa tunawapa huruma wale walioko kwenye disadvantage, Hii haiapply kwa watu ambao hawana empathy kama wewe na wenzio.

It was nice having a conversation with you, bye.
 
Back
Top Bottom