SI KWELI Watu wamepigana wakati wa Usaili wa Kada ya Afya nchini Tanzania

SI KWELI Watu wamepigana wakati wa Usaili wa Kada ya Afya nchini Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Watu wanachapana mikono huko, yaani ni noma sana.

Screenshot_20240909-085354_1.jpg



 
Tunachokijua
Usaili wa kuandika katika kada ya afya umefanyika Septemba 3, 2024 nchi nzima ili kuwapta wataalam wa afya watakaojaza nafasi 9, 483 za ajira.

Wakati usaili huu ukiwa unaendelea ilisambaa video mtandaoni ikionesha binti akiwa anasukumwa na Mwanaume akiwa ameshika karatasi kati ya watu wengine walioshika karatasi ndani ya chumba, huku Watu wanaosambaza video hiyo wakidai ni tukio lililotukia kwenye moja ya vituo vya usaili, Tazama( hapa na hapa)

screenshot-2024-09-03-at-23-08-32-devotatweve-on-x-inadaiwa-kafanyiwa-hivi-wakati-wa-usahili-m-png.3086321
Ukweli ni Upi?
JamiiCheck imefuatilia video hiyo kupitia utafutaji wa kimtandao kwa kutumia Google Reverse Image ili kufahamu uhalisia wa video hiyo inayodaiwa kuwa ni ya tukio lililotokea kwenye moja ya maeneo yaliyofanyika usaili katika kada ya afya nchini.

Tumebaini kuwa video hiyo si ya Tanzania na haihusiani na usaili katika kada ya afya, video hiyo ni ya Congo na iliwekwa mtandaoni tarehe Agosti 26, 2024 (Tazama hapa) na kuendelea kusambaa, (tazama hapa) ikionesha tukio lililotokea Congo DRC.

Ufuatiliaji wa kimtandao unaonesha tukio hili lilimuhusisha binti wa chuo cha ISTA Kolwezi lundi (l’Institut Supérieur des Techniques Appliquées (ISTA)) ambaye alishambuliwa na mwalimu akiwa kwenye mtihani Mwalimu anafahamika kwa jina la Tshipamba Kabwe.

1725399147413-jpeg.3086332

Barua ikionesha kusimamishwa kazi kwa mwalimu aliyemshambulia mwanafunzi huyo​
Ukitazama kwa umakini huyo binti kamtukana huyo jamaa, kama mnabisha leta video yenye sauti. Lakini kwa sababu jamii ya kibongo ishakuwa programmed kwenye kuchukia wanaume basi inaonekana binti hana kosa na jamaa ndio kakosea peke yake.

Kesi ya Paulina Gekul kimyaa, kesi ya mkuu wa mkoa wa Geita ikashupaliwa. Makonda kusema ana mke mzuri hadi taasisi za haki za wanawake wakatoa tamko, mmama afande wa polisi kutuma wabakaji hakuna taasisi inayolalamika na wanaume waliohusika wamekamatwa.

Kwanini wanawake wanaonekana hawawezi kosea?
Ingekua na sauti ingependeza sana
 
Hapana mkuu Hana haki ya kumtukana ila hata kama katukanwa hakupaswa ku react namna hiyo na ukizingatia ni Afsa utumishi .
Wote wana makosa, hii tabia ya kulea ujinga wa wanawake ionekane wao ni malaika inawapoteza hata wao wenyewe. Bahati mbaya kakabwa hapo kakata pumzi hapati faida yeyote.

Ndio maana kina dronedrake wameamua hawaoi. Kila jambo likija mbele ya meza baina ya mwanaume na mwanamke, hakuna anayehangaika na kosa la mwanamke, mwanaume ndio anaonekana shetani tu.
 
Kichwa kikubwa akili huna.

Labda nyie mnaofanya kazi huko vichochoroni, mimi kazini kwangu hata Boss wangu haruhusiwi kunigombeza, kama nimekosea anipe onyo la maandishi ambalo consequence yake ni zaidi ya hivyo vibao mnavyotishia navyo watu.

Nguvu nyingi akili kisoda ndio maana kazi haziendi.
Vipi hapo kazini kwako, mnaruhusiwa kumtukana kiongozi/boss wako?

Wewe ukitukana na boss akikuchapa vibao wote mnakosa, na ndiyo mapungufu ya binadamu hayo. Ila sio mmoja aonekane kakosea alafu mwingine apewe excuse.
 
itamcost heavily! Hata mahakamani binti atashinda! Then civil case alipwe fidia. Kesi nzuri sana hii
Najua itamgharimu, point yangu ni kwamba kesi kama hizi tuziangalie pande zote mbili, wakati tunapinga mabinti kufanyiwa vitendo vya kinyanyasaji pia tuwakumbushe wao pia wanawajibika kujilinda wasiwe chanzo cha wao wenyewe kufanyiwa hivi vitendo.

Tukisema tuwakemee tu hawa wanyanyasaji wakati tumewaachia mabinti na wadogo zetu wa kike uhuru wa kutukana watu, kula hela za wanaume na kutembea na waume za watu haya matukio yataendelea kuwepo tu.
 
Busara na hekima zinahitajika sana kwenye haya mambo.

Unakuta dada ana mda mrefu yuko mtaani, kaanza kujiandaa mapema na nauli kakopa au kuomba kwa watu akafanye interview na inawezekana paper imemgonga.

Kwenye hii hope yake labda anaweza akapata kazi msimamizi nae anamletea vikwazo vingine havielewi anajikuta anabishana hovyo. Msimamizi anashindwa kuelewa hali aliyonayo dada nae anatumia nguvu badala ya hekima. Au nae alivurugwa huko nyumbani alipotoka?

Ni huzuni
 
Kichwa kikubwa akili huna.

Labda nyie mnaofanya kazi huko vichochoroni, mimi kazini kwangu hata Boss wangu haruhusiwi kunigombeza, kama nimekosea anipe onyo la maandishi ambalo consequence yake ni zaidi ya hivyo vibao mnavyotishia navyo watu.

Nguvu nyingi akili kisoda ndio maana kazi haziendi.
Point yangu ni ile ile, ukimchokoza mtu kwa kauli chafu akikisha una nguvu za kudhibiti, kama nguvu hauna basi kotakachofuata usianze kulilia maana utakua umejitakia mwenyewe
 
Ujinga wenu waTz ni pamoja na kutokujua adhabu ipi itolewe kwa kosa lipi, Hii long ass paragraph haina utetezi wowote wa maana, umeongea mihemko tu.

Wapi hapo kazini kwako uliambiwa mtu akifanya kosa fulani umpige? Work ethics ndio zinasema hivyo?

To begin with ushahidi uliopo kwenye video, hao wasahiliwa wote wanaonekana wapo desparate na kitu fulani, Ndio maana unaona wanaongea wote kwa mara moja, huyo binti ndiye ameenda extra mile sijui ametukana au ametoa neno gani, ndio huyo baba kumkunja hivyo.

Huyo baba angeweza kuita security wametoe huyo binti, mtihani wake uwekwe alama, na aambiwe kabisa hata akipewa kazi ameshaonesha dalili zote za kukosa adabu hivyo hafai kuwa mtumishi wa umma, Kitendo cha huyo baba kumpiga huyo binti tukienda kisheria huyo binti anashinda mchana kweupe, na hata haki isipotendeka basi huyo baba atapitisha rushwa kila sehemu au atasaidiwa na misogynist kama wewe.

Anyways, sijui hiyo video ninini au ni wapi ila mtu yeyote “sane” ataelewa mfanyakazi unatakiwa kuwa kwenye safe side katika maadili unless ni mzuri kwa rushwa au una watetezi.
Wapi kazini kwako uliambiwa umtukane boss/kiongozi wako? Work ethics ndiyo zinasema hivyo?

Kwanini binti aende extra mile kuliko wengine wote?

Binti kuepusha shari, angeweka mtihani wake asipe mwenyewe bila kuitiwa security. Hii ingeepusha yeye kutamka maneno mabaya. Kisheria pia ni kosa kutoa lugha za matusi, kwahiyo boss akishtaki na ushahidi upo anashinda labda binti atoe "rushwa" au asaidiwe na mtu kama wewe.
 
Vipi hapo kazini kwako, mnaruhusiwa kumtukana kiongozi/boss wako?

Wewe ukitukana na boss akikuchapa vibao wote mnakosa, na ndiyo mapungufu ya binadamu hayo. Ila sio mmoja aonekane kakosea alafu mwingine apewe excuse.
Hawa wanawake wa kisasa wanacheza rafu nyingi sana, tatizo wakikutana na mtu ambae hawezi kuvumilia ujinga ndipo hapo wanaonekana victims kumbe wao wenyewe ndio chanzo.
 
Angekuwa ndiyo wakati wa usaili wa walimu afu hili likatokea ungeona matusi ambayo yangerushwa humu hasa juu ya walimu ,,, lkin kwasababu ni kada ya afya huwezi ona hayo yakitokea
 
Ukijiona unashindwa kuzuia hasira zako hata kwa vitu vidogo ujue we ni dhaifu sana, huyo mzee kwa umri wake ilistahili awe na busara hilo shambulio alilolifanya la kumkaba shingo hakustahili kulifanya
 
Back
Top Bottom