OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Kwa utafiti wangu usio rasmi, kuna wale watu wanaongea sana, ukiwakuta kwenye kikundi cha watu au popote pale wao mara nyingi hupenda kudominate mijadala, mara nyingi waongeapo huongea kwa sauti ya juu sana, hujifanya wanajua kila kitu, pia hawa watu hupenda kuzoeana haraka na kila mtu ndani ya muda mfupi, mara nyingi huwa hawana aibu pia ni wachangamfu sana.
Hawa watu huwa hawana siri, pia huwa wanapenda kuhamisha maneno kutoka point A kwenda B kisha kuyarudisha point A.
Hawa watu wapo kila mahali kuanzia mashuleni, vyuoni, kwenye nyumba za kupanga, nyumba za ibada, .mtaani, nyumbani kwako n.k
Wanaweza kuwa ndugu zako, wadogo zako, kaka zako, mke wako n.k
Kama unajambo hutaki lijulikane kwa watu wengi basi epuka kuwashirikisha hawa watu.
Kuwa makini, chukua tahadhari.
Nawasilisha.