Watu wanasali, mabomu yanalia. Je, kuna uhuru wa kuabudu?

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
778
Reaction score
1,592
Wakuu habari zenu,

Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.

Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?​

Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
IMG_4903.jpeg

Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:​
  • Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao,​
  • Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu,​
  • Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.​
Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.

Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.​

Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu.

Haya bana mimi naishia hapo kwa leo na mpira nawaachia nyinyi wanazuoni​
 
View attachment 3388644

Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu. Tafakari hizi hazipaswi kuchukuliwa za uchochezi, bali za kujenga. Mpira nawaachia nyinyi wanazuoni​

Kwenye familia mzazi (baba au mama) akikosea ni lazima ashughulikiwe yeye bila kuingilia au kuwanyima haki watoto wake.

Jambo hili linaloendelea kwa sasa kwa hao wananchi haliko sawa hata kidogo. Najiuliza ni nani anayelisimamia! Na wanaofanya wanafikiri taifa litapata faida gani?

Je mahakama zetu ziko wapi? Kwa nini hatusikii kauli ya mahakama kuhusu hili. Tunaona mahakama kwenye nchi jirani kama Kenya zikiwa mbele kukemea haraka ukiukwaji wa aina yoyote wa haki za raia wao na katiba yao. Hapa kwetu kuna nini kwenye mahakama zetu, kwa nini mambo kama haya yatokee na hakuna hatua za kimahakama za kukemea au kuyatolea maamuzi ya haraka ili kuepusha uminywaji wa haki za raia wasiona hatia?

Kama haya mambo yataendelea hivi taifa letu halitakuwa salama.

Je haya wanayofanyiwa hao ndugu zetu kweli yana maslahi mapana na afya kwa taifa letu?

Inasikitisha sana,
 
Mkuu maswali yako ni halali kabisa na yanapaswa kusikika si tu mitandaoni bali pia kwenye meza za maamuzi ya dola.

Kwa kutazama kisheria na kiuhalisia, hoja yako kuhusu “mzazi akifanya kosa, watoto wasiadhibiwe” ni kiini cha haki ya asasi na mtu binafsi kutobeba mzigo wa makosa ya wengine. Ni msingi wa rule of law duniani kote, ambapo uwajibikaji ni wa mtu binafsi (individual liability) na si wa makundi kwa jumla (collective punishment).

Kwa bahati nzuri, na hapa ndipo hoja yako ya kuhoji ukimya wa mahakama inapopata mwanga. kanisa husika kupitia “Registered Trustees of Glory of Christ Tanzania Church” tayari walifungua kesi Mahakama Kuu, Miscellaneous Civil Application No. 13189 of 2025, wakilalamikia kile walichokiita amri ya kimyakimya kutoka kwa Msajili wa Vyama kuhusiana na kufutwa kwa usajili wao ama kusimamishwa kwa shughuli za kidini.

Lakini cha kushangaza Mahakama yenyewe imesema kuwa, nanukuu:​
Waraka unaodaiwa kufuta au kusimamisha kanisa haukuwa rasmi, haukusainiwa, na hata haukuelekezwa kwa jina rasmi la kanisa hilo. Kwa kifupi, “kanisa lililofutwa si hili linalolalamika.”​
Kwa tafsiri rahisi: hakuna ushahidi wa kisheria kuwa Glory of Christ Tanzania Church ya ndugu Askofu imefutwa. Mahakama imeona hali hiyo kama ya kutatanisha na isiyojitosheleza kuhalalisha uingiliaji wa uhuru wa ibada. Lakini sasa swali kuu: Kwa nini bado waumini wanazuiwa kuabudu? Kwa amri ipi? Kwa msingi gani wa kisheria?

Hali hii, kwa hakika, ni mfano hai wa kile wanazuoni huita de facto suppression of rights — hali ambapo mamlaka hutumia nguvu za kiutendaji (executive discretion) kwa namna inayozalisha athari zinazokwenda nje ya mipaka ya sheria iliyo wazi. Kwa maneno mengine: ni hali ambapo uhuru wa raia unaminywa bila mwavuli wa haki wala uhalali wa kisheria.

Ndio maana hoja yako ya kutaka Mahakama zetu ziingilie kati mapema ni ya msingi. Kama ilivyo Kenya, Afrika Kusini, ama Ghana, mahakama huwa ni kimbilio la haraka dhidi ya ukiukwaji wa haki za kikatiba. Lakini hapa kwetu, bado kuna mwanya kati ya haki iliyoandikwa na haki inayolindwa kwa vitendo.

Kwa sasa, wananchi wanapaswa kufahamu kuwa haki ya kuabudu ni ya kikatiba (Ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania), na haiwezi kuondolewa kimyakimya au kwa sababu ya shutuma zisizothibitishwa dhidi ya mtu mmoja. Hata kama Askofu angekuwa na kesi binafsi, hilo haliwezi na halistahili kugeuzwa kuwa adhabu ya kiroho kwa maelfu ya waumini.

Tukumbuke, hili si suala la kiongozi mmoja au dini moja. Ni jaribio la mifumo yetu ya utawala dhidi ya misingi ya katiba yetu. Tunapokubali ukimya wa mamlaka za kisheria mbele ya vitendo vya wazi vya kukiuka haki, tunaandaa mazingira hatarishi kwa vizazi vijavyo.​
 
Huo siyo uhuru.

Uhuru siyo kufanya unachotaka sababu kuna muda unaweza ukataka visivyo sahihi ila Uhuru wa kweli ni kutokulazimishwa kufanya jambo fulani.
 
Inaonekana Serikali inataka Gwajima aombe msamaha. Na Gwajima amegoma kwa sababu hakuna kosa amefanya. Serikali haijamshitaki na wala Kanisa lake halijashitakiwa.

Ni kwa vile wamekataa kuwapigia magoti watawala. Hicho ndicho kinawauma sana Watawala. Nawashauri wafoji barua waseme Gwajima kaandika kuomba msamaha ili roho zao ziridhike na hao waumini waendelee kusali. Hii ya kila Jumapili kuwapiga hawa waumini kuna kitu kibaya sana kitatokea
 
Wakuu habari zenu,

Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.

Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?​

Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
View attachment 3388644
Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:​
  • Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao,​
  • Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu,​
  • Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.​
Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.

Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.​

Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu.

Haya bana mimi naishia hapo kwa leo na mpira nawaachia nyinyi wanazuoni​

kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!
pia haya makanisa ya walokole yana matatizo sana kumchukulia mtu mmoja kama ndo kioo cha imani yao(Tatizo kubwa sana hili)

as a lutheran naweza kusali kokote nchini na ibada zetu znaendana hazina tafauti kwenye utaratibu wa ibada,
 
Huo siyo uhuru.

Uhuru siyo kufanya unachotaka sababu kuna muda unaweza ukataka visivyo sahihi ila Uhuru wa kweli ni kutokulazimishwa kufanya jambo fulani.
Hao waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima wana kosa gani hadi wazawadiwe vipigo na kanisa lao kufungwa huku Mahakama ikithibitisha barua ya zuio iliyotolewa ni batiri?
 
kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!
pia haya makanisa ya walokole yana matatizo sana kumchukulia mtu mmoja kama ndo kioo cha imani yao(Tatizo kubwa sana hili)

as a lutheran naweza kusali kokote nchini na ibada zetu znaendana hazina tafauti kwenye utaratibu wa ibada,
Hao waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima wana kosa gani hadi wazawadiwe vipigo na kanisa lao kufungwa huku Mahakama ikithibitisha barua ya zuio iliyotolewa ni batiri?
 
Hao waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima wana kosa gani hadi wazawadiwe vipigo na kanisa lao kufungwa huku Mahakama ikithibitisha barua ya zuio iliyotolewa ni batiri?
serikali ndo msajili wa makanisa, wakisema sitisha shuhuli kwann unakua mkaidi?
 
Mwenye mamla ya kutoa adhabu ni Serikali au Mahakama?
aliesajili ndo mwenye mamlaka! yeye ndo anaamua uendelee kuwepo ama usiwepo kwan yeye ndo ana database ya makanisa yote
 
Hakuna uhuru wa kuabudu na anae sababusha ni Mama Samia hii inaonyesha kuwa hafai kuwa Raisi wa watanzania.
Na mimi nazani mwenye hadhi ya kumkosoa Rasi wa kwanza kabisa ni Mtumishi wa Mungu.
PIli ni wananchi kwakuwa wao ndio waliomuweka madarakani ila chaajabu ameonyesha kuwa hawezi kuwa Raisi kwakuwa analeta chuki ya udini. Leo nikimuona muislaam najisikia vibaya sana kwa sababu Raisi ni muislaam na ndio maana waislam hawasemi chochote kuhusu wenye imani ya kikristo kuonewa kupigwa na kujeruhiwa na jeshi la Samia.
 
Wakuu habari zenu,

Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.

Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?​

Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
View attachment 3388644
Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:​
  • Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao,​
  • Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu,​
  • Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.​
Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.

Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.​

Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu.

Haya bana mimi naishia hapo kwa leo na mpira nawaachia nyinyi wanazuoni​

Hapo wanaposali ni eneo limeidhinishwa kuwa eneo la ibada?
 
kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!
pia haya makanisa ya walokole yana matatizo sana kumchukulia mtu mmoja kama ndo kioo cha imani yao(Tatizo kubwa sana hili)

as a lutheran naweza kusali kokote nchini na ibada zetu znaendana hazina tafauti kwenye utaratibu wa ibada,
Je huo ndio msimamo wa serikali, mbona hakubugudhiwa kipindi hajaanza kusema UTEKAJI.

Haya mambo tusichague upande kisa dini, ama siasa.
Binafsi mie muislam lakin kinachofanyika si sawa, aliyekosea ni gwajima, kama nyie mnaona gwajima kazingua basi achukuliwe hatua yeye.

Kama makanisa ya kilokole ni hovyo, yafungiwe yoote.
 
makanisa ya kilokole mtu ndo anamiliki kanisa ni tafauti na haya mfano kkkt lutheran ama vatican roman, walokole makanisa ni ya mtu binafsi ni property yake!
However kuna sheria na kanuni katika uendeshaji wa makanisa ambayo serikai ndo msimamizi mkuu kuanzia huduma inavoendeshwa mpaka vyeti vya ndoa serikali ndo inatoa hata kama umefungia kanisan, hivo basi huezi kuachia kanisa likajiendea linavotaka!

Kwenye biblia kuna mstari unasema "Heshimu mamlaka yaliopo juu yako" sasa kama kanuni kama hii unashindwa kufuata unadhan una stahili kuendesha huduma?
 
Back
Top Bottom