Watu wanasali, mabomu yanalia. Je, kuna uhuru wa kuabudu?

Watu wanasali, mabomu yanalia. Je, kuna uhuru wa kuabudu?

Wakuu habari zenu,

Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.

Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?​


Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
View attachment 3388644
Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:​
  • Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao,​
  • Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu,​
  • Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.​
Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.

Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.​

Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu.

Haya bana mimi naishia hapo kwa leo na mpira nawaachia nyinyi wanazuoni​

Huu ni uonevu tu, hamna kingine
 
kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!
pia haya makanisa ya walokole yana matatizo sana kumchukulia mtu mmoja kama ndo kioo cha imani yao(Tatizo kubwa sana hili)

as a lutheran naweza kusali kokote nchini na ibada zetu znaendana hazina tafauti kwenye utaratibu wa ibada,
Huna akili Wala dini
 
Inaonekana huijui katiba au haujalifatilia hili suala vizuri mkuu. Haki ya kuabudu ni huru, hivyo mtu anaabudu vile anavyoona yeye inafaa na anaabudu kile anachokiamini. Kwaio kama wenyew wameamua kuamini katika kufanya ibada wakiwa katika eneo fulani hiyo ni haki yao kikatiba mkuu.​
unachanganya mambo, haki ya kuabudu ipo, tuseme wale wa gwajima wangesema tunaenda kuabudu manyumban kwetu ni haki yao, ila kwenye hilo kanisa limepigwa marufuku nn kigumu apo
 
unachanganya mambo, haki ya kuabudu ipo, tuseme wale wa gwajima wangesema tunaenda kuabudu manyumban kwetu ni haki yao, ila kwenye hilo kanisa limepigwa marufuku nn kigumu apo
Mkuu ni kanisa gani lililopigwa marufuku wakati Mahakama kuu yenyewe ilisema kuwa “kanisa lililofungiwa” kwenye waraka wa Msajili wa Vyama siyo Glory of Christ Tanzania Church la ndugu Askofu, bali chombo kingine tofauti kwa jina (“Glory of Christ Church”) na kwamba waraka huo haukusainiwa, haukuwa rasmi, na haujawahi kutumwa kwa kanisa husika.​


Kwa maneno rahisi:
✅ Kanisa la Askofu Gwajima halijawahi kufutwa rasmi kisheria. Mahakama imethibitisha hilo.
✅ Hakuna amri ya kisheria inayolizuia kanisa hilo kuendelea na ibada.
IMG_4920.jpeg

Sasa kama hakuna amri halali wala iliyo rasmi kutoka kwa Msajili, kwa nini waumini wake wanazuiwa kuingia kanisani, wanatawanywa kwa mabomu, wengine kukamatwa? Hili ndilo jambo la msingi la kujiuliza na kuliangalia kwasasa.

Kama ulivyosema, hata mtu akiabudu nyumbani ni haki yake, ni kweli. Lakini ni haki hiyo hiyo inayopaswa kulindwa hata anapochagua kuabudu kanisani, mradi hakikiukii sheria halali. Na hapa hakuna ushahidi kuwa waliokuwa kanisani walienda kufanya kosa lolote la jinai.
​
 
Back
Top Bottom