Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Sanaa🤐Hii kitu inatuchafua kimataifa
Wakuu habari zenu,
Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.
Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?
Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
View attachment 3388644
Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:
Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao, Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu, Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.
Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.
Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu. Tafakari hizi hazipaswi kuchukuliwa za uchochezi, bali za kujenga. Mpira nawaachia nyinyi wanazuoni
Kwenye familia mzazi (baba au mama) akikosea ni lazima ashughulikiwe yeye bila kuingilia au kuwanyima haki watoto wake.
Jambo hili linaloendelea kwa sasa kwa hao wananchi haliko sawa hata kidogo. Najiuliza ni nani anayelisimamia! Na wanaofanya wanafikiri taifa litapata faida gani?
Je mahakama zetu ziko wapi? Kwa nini hatusikii kauli ya mahakama kuhusu hili. Tunaona mahakama kwenye nchi jirani kama Kenya zikiwa mbele kukemea haraka ukiukwaji wa aina yoyote wa haki za raia wao na katiba yao. Hapa kwetu kuna nini kwenye mahakama zetu, kwa nini mambo kama haya yatokee na hakuna hatua za kimahakama za kukemea au kuyatolea maamuzi ya haraka ili kuepusha uminywaji wa haki za raia wasiona hatia?
Kama haya mambo yataendelea hivi taifa letu halitakuwa salama.
Je haya wanayofanyiwa hao ndugu zetu kweli yana maslahi mapana na afya kwa taifa letu?
Inasikitisha sana,
Waraka unaodaiwa kufuta au kusimamisha kanisa haukuwa rasmi, haukusainiwa, na hata haukuelekezwa kwa jina rasmi la kanisa hilo. Kwa kifupi, “kanisa lililofutwa si hili linalolalamika.”
kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!Wakuu habari zenu,
Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.
Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?
Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
View attachment 3388644
Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:
Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao, Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu, Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.
Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.
Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu.
Haya bana mimi naishia hapo kwa leo na mpira nawaachia nyinyi wanazuoni
Hao waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima wana kosa gani hadi wazawadiwe vipigo na kanisa lao kufungwa huku Mahakama ikithibitisha barua ya zuio iliyotolewa ni batiri?Huo siyo uhuru.
Uhuru siyo kufanya unachotaka sababu kuna muda unaweza ukataka visivyo sahihi ila Uhuru wa kweli ni kutokulazimishwa kufanya jambo fulani.
Hao waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima wana kosa gani hadi wazawadiwe vipigo na kanisa lao kufungwa huku Mahakama ikithibitisha barua ya zuio iliyotolewa ni batiri?kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!
pia haya makanisa ya walokole yana matatizo sana kumchukulia mtu mmoja kama ndo kioo cha imani yao(Tatizo kubwa sana hili)
as a lutheran naweza kusali kokote nchini na ibada zetu znaendana hazina tafauti kwenye utaratibu wa ibada,
serikali ndo msajili wa makanisa, wakisema sitisha shuhuli kwann unakua mkaidi?Hao waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima wana kosa gani hadi wazawadiwe vipigo na kanisa lao kufungwa huku Mahakama ikithibitisha barua ya zuio iliyotolewa ni batiri?
Mwenye mamla ya kutoa adhabu ni Serikali au Mahakama?serikali ndo msajili wa makanisa, wakisema sitisha shuhuli kwann unakua mkaidi?
aliesajili ndo mwenye mamlaka! yeye ndo anaamua uendelee kuwepo ama usiwepo kwan yeye ndo ana database ya makanisa yoteMwenye mamla ya kutoa adhabu ni Serikali au Mahakama?
Kila la heri🦍aliesajili ndo mwenye mamlaka! yeye ndo anaamua uendelee kuwepo ama usiwepo kwan yeye ndo ana database ya makanisa yote
Hapo wanaposali ni eneo limeidhinishwa kuwa eneo la ibada?Wakuu habari zenu,
Kiukweli nimekuwa nikifuatilia kwa utulivu kinachoendelea kuhusu baadhi ya viongozi wa dini nchini, hususan tukio linalomhusu Askofu mmoja ambaye kwa sasa jina lake limekuwa gumzo lakini kwa kweli kinachonigusa si jina lake, bali kile kinachowakumba waumini wake.
Leo nimeona video zinasambaa: watu wakitawanywa kwa mabomu ya machozi, wengine wakikamatwa au kuzuiwa kuingia kwenye ibada. Swali la msingi: wao kosa lao ni nini? Je, kwenda tu kwenye ibada kwao sasa ni kosa la jinai🤔?
Sitaki kujifanya mjuzi wa kila kitu na wala siko hapa kama mwanasiasa wala mfuasi wa upande wowote. Naandika kama raia anayejua kwamba Katiba ya Tanzania — Ibara ya 19(1) na (2) inatamka kuwa kila mtu ana haki ya kuamini, kufanya ibada na kueneza dini yake kwa hiari na bila kuingiliwa na mamlaka ya dola, isipokuwa kama kuna sheria halali na ya haki inayotoa sababu maalum.
View attachment 3388644
Lakini hata hiyo sheria, haipaswi:
Kuwahukumu watu wote kwa sababu ya tuhuma dhidi ya mtu mmoja au kiongozi wao, Kuingilia uhuru wa mtu binafsi wa kuabudu, Kuzuia haki ya ibada kwa makundi yasiyohusishwa moja kwa moja na jambo linalodaiwa kuwa kosa.Swali gumu kwetu kama jamii: tunaelekea wapi tunapofikia hatua ya kudhibiti ibada kwa misingi ya kisiasa au tafsiri ya kauli za mtu mmoja? Tukikubali hali hii leo, kesho inaweza kuwa dini nyingine, kiongozi mwingine, au hata sisi wenyewe.
Naamini usalama wa taifa ni jambo la msingi. Lakini usalama huo haujengwi kwa hofu wala mabavu, bali kwa kuheshimu haki, kuwasikiliza raia, na kulinda misingi ya kikatiba hata pale tunapopishana kimtazamo.
Nchi inayojivunia kuwa ya haki lazima itafakari namna inavyolinda uhuru wa watu hata inapokinzana na mitazamo yao. Tusiruhusu tofauti za maoni au imani kuwa sababu ya kuyumbisha misingi ya haki ya kila mtu.
Haya bana mimi naishia hapo kwa leo na mpira nawaachia nyinyi wanazuoni
Je huo ndio msimamo wa serikali, mbona hakubugudhiwa kipindi hajaanza kusema UTEKAJI.kma shida ni kusali makanisa mengi yapo, pia unaweza kusali nyumban kama mtu mwenye akili timamu!
pia haya makanisa ya walokole yana matatizo sana kumchukulia mtu mmoja kama ndo kioo cha imani yao(Tatizo kubwa sana hili)
as a lutheran naweza kusali kokote nchini na ibada zetu znaendana hazina tafauti kwenye utaratibu wa ibada,
makanisa ya kilokole mtu ndo anamiliki kanisa ni tafauti na haya mfano kkkt lutheran ama vatican roman, walokole makanisa ni ya mtu binafsi ni property yake!Je huo ndio msimamo wa serikali, mbona hakubugudhiwa kipindi hajaanza kusema UTEKAJI.
Haya mambo tusichague upande kisa dini, ama siasa.
Binafsi mie muislam lakin kinachofanyika si sawa, aliyekosea ni gwajima, kama nyie mnaona gwajima kazingua basi achukuliwe hatua yeye.
Kama makanisa ya kilokole ni hovyo, yafungiwe yoote.