John Magongwe
Member
- Jan 4, 2024
- 71
- 119
Watu Wanatembea na Laana Mwilini bila Kujua
Laana ni Nini
Laana ni bahati mbaya au maneno mabaya ya maapizo yanayotamkwa kumuelekea mtu fulani yeye mwenyewe au kitu fulani kinachomuhusu, kwa makusudi ya kumdhuru mtu huyo au kitu kinachomuhusu. Kwa mfano, kazi, shamba, watoto, masomo n.k. Laana ni kinyume cha baraka.
Laana inaweza ikasababishwa kwa makusudi maalum (mfano: laana ambayo ni matokeo ya dhambi za wanadamu), au pasipo kujua (mfano: laana ya kujitamkia sisi wenyewe). Kwa njia zote hizi mbili, laana inafanya kazi, iwe kwa makusudi au pasipo kujua (kwa bahati mbaya).
Ili laana ifanye kazi, ni lazima iwe imeunganishwa na nguvu fulani zisizo za kawaida. Nguvu za ziada (supernatural powers). Nguvu hizo ni lazima ziwe zinazidi nguvu za mtu au kitu kinacholaaniwa. Maana yake ni kwamba, mdogo hawezi kumlaani mkubwa. Shetani hawezi kumlaani Mungu. Mtu aliyesimama katika kweli na haki ya Mungu hawezi kulaaniwa na shetani kutokana na ile nguvu ya Mungu iliyomo ndani yake.
Maneno yetu wenyewe au ya watu wa karibu nasi na matendo ya maisha yetu, ndiyo sababu kubwa ya laana katika maisha yetu na vizazi vijavyo. Hiyo ni kwa sababu kila tunachokitamka na tunachokitenda kinafuatiliwa kutimilizwa na falme mbili tofauti: ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani. Ufalme wa shetani hufuatilia, hasa mambo ambayo ni hasi, kuyatimiliza katika maisha yetu.
Mwanzo 2:16-17: Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu (Adamu), akisema, matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Wakati Mungu anampa maagizo Adamu kwa habari ya chakula ambacho ni matunda, Biblia haisemi kuwa shetani naye alikuwepo akiyasikiliza maagizo hayo. Lakini kwa hakika shetani alikuwepo, japo Adamu hakumuona, aliyasikia vizuri sana maagizo hayo. Hili tunalithibitisha kutokana na kitendo chake (shetani) cha kumfuata Hawa na kumwambia habari ile ile ihusuyo maagizo waliyopewa na Mungu.
Mwanzo 3:1: Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda yote ya miti ya bustani? Elewa kuwa yule alikuwa ni shetani aliyevaa umbo la mnyama nyoka. Yaani, kila unachokitenda ama kukizungumza, shetani anakuona na kukusikia, na kama Biblia inavyosema kuwa shetani ni mshitaki wetu (Ufunuo 12:10), ndivyo ilivyo, anafanya kazi mchana na usiku kuhakikisha matendo na maneno yetu hasi yanatimia na tunapata mateso. Hiyo ndiyo furaha yake.
Ikiwa tumetamka au tumetamkiwa maneno ya kuyalaani maisha yetu, ufalme wa giza unatuma mapepo yatakayokufuatilia mchana na usiku ili kuhakikisha ile laana iliyotamkwa juu yako inatimia na kukupata.
Laana inasababishwa na nini
MUNGU: Mungu hatusababishii wanadamu laana kama kitu cha furaha kwake, bali ni matokeo ya dhambi zetu. Tunapomkosea Mungu huamua kuachilia laana katika maisha yetu kwa makusudi ya kutufanya tumrudie yeye baada ya kutambua tunataabika kwa sababu tumemuacha Mungu.
Kumbukumbu la Torati 28:15: Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo (ukiamua kutenda dhambi), ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. Malaki 2:2: Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni (amri ya Mungu), ili kulitukuza jina langu, asema Bwana wa majeshi, basi nitawapelekeeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.
SHETANI: Unapoamua kuishi maisha ya dhambi ni kwamba unakuwa umedanganywa (umesababishiwa laana) na ibilisi, ambaye alishalaaniwa kwanza. 2Petro 2:14: Wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana (wana wa shetani, wana wa ufalme wa giza).
MWANADAMU: Mwanadamu akisimama yeye kama yeye hana nguvu wala uwezo wa kulaani. Lakini anaposimama upande mmojawapo, aidha kwa Mungu au kwa shetani, huweza kusababisha laana. Kwa sababu akiwa upande wa Mungu akitamka neno zuri au baya linatokea (Mathayo 21:18-19, 1Wafalme 17:1 na 18:1), kutokana na ile nguvu ya Mungu iliyomo ndani yake. Na mwanadamu huyo huyo, akisimama upande wa shetani laana atakayoitamka itatokea, kwa sababu furaha ya shetani ni kuwaona wanadamu wanapata shida na mateso, lazima atatuma roho chafu (mapepo) ziifuatilie na kuitimiza laana hiyo kwa mhusika.
Warumi 12:14: Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani (mwanadamu ana uwezo wa kulaani). Yakobo 3:9: Kwa huo (ulimi) twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo (ulimi-maneno ya kinywa) twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
Kwa maana hiyo, unaweza kuwa unatembea chini ya laana katika maisha yako, au vitu fulani katika maisha yako vinaweza vikawa vimelaaniwa pasipo wewe kujua. Na laana hiyo inaweza ikawa imesababishwa na Mungu, shetani au mwanadamu.
Laana zinavyosababishwa
1. Laana itokanayo na kuwalaani watumishi wa Mungu waliobarikiwa
Mtu ye yote au kitu chochote Mungu alichokibariki, mwanadamu hawezi kukilaani. Na ikiwa umemlaani au kutamka maneno mabaya juu ya mbarikiwa ye yote wa Mungu, laana hiyo inafanyika kuwa baraka kwa uliyemtamkia, lakini inakurudia wewe kama laana (Hesabu 23:11; Hesabu 24:10). Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa (Mwanzo 12:3). Atakayekulaani alaaniwe, na atakayekubariki abarikiwe (Mwanzo 27:29).
2. Laana itokanayo na kutenda dhambi au kutotii maagizo ya Mungu
Mwanadamu anapofanya dhambi, hasira ya Mungu inawaka juu yake, na Mungu anaagiza laana juu ya mwanadamu huyo kwa makusudi ya kumkumbusha mwanadamu huyo kuwa anatakiwa kurejea kwa Mungu na kuziacha njia zake mbaya.
Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, usiyale (kutotii); ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako (Mwanzo 3:17). Angalieni, naweka mbele yenu hivi leo baraka na laana. Baraka ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, niwaagizayo hivi leo; na laana ni hapo msiposikiza maagiza ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua (Kumbukumbu la Torati 11:26-28). Epuka kutenda dhambi ili kukwepa laana ya Mungu.
3. Laana ya kujitamkia au kutamkiwa kwa kujua au pasipo kujua
Hebu tuone mifano ambapo unakuta mtu anatamka maneno yafuatayo:
“Sisi ukoo wetu ni maskini tu hata tufanyeje”, “kwa hii kozi niliyosoma sijui kama nitapata kazi kwa kweli”, “watoto wa mama fulani hawaolewagi”, “mimi masomo ya sayansi hata nifanyaje siji kufaulu”, “kwa jinsi nilivyo sidhani kama nitaolewa”.
Hiyo ni baadhi ya misemo iliyobeba laana ndani yake. Na lazima kuna nguvu itafuatilia kuhakikisha inatimiza makusudi yaliyopo ndani ya misemo hiyo. Na mara nyingi laana ya namna hii, watu wengi tunajitamkia pasipo kujua kuwa tunachokitamka kitatimia katika maisha yetu (Warumi 12:14, Yakobo 3:9). Unakuta tunatembea na laana mwilini bila kujua.
4. Laana ya wazazi
Hii inapatikana kutokana na jinsi unavyowatendea wazazi wako. Haijalishi wazazi wako ni watu wa namna gani au wamewahi kukukosea nini, watabaki kuwa wazazi wako na ni lazima uwape heshima yao (Kutoka 20:12). Kitu chochote kibaya utakachowafanyia au kuwasemea wazazi wako, Mungu atajilipishia kisasi katika maisha yako au hata uzao wako (Mathayo 15:4).
Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea (alimchungulia na kuuona uchi wake). Akasema, na alaaniwe Kanaani; atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake (Mwanzo 9:24-25). Haijalishi wazazi wako wana tabia gani, laana yoyote watakayoitamka juu yako au manung’uniko yoyote utakayowasababishia, yatafanyika kuwa laana itakayolaani maisha yako. Na alaaniwe amdharauliye baba yake au mama yake, na watu wote waseme Amen (Torati 27:16).
Ili kuifuta laani hii katika maisha yako, inahitaji upate kibali cha wazazi. Hivyo, ikiwa umetambua kuwa uko chini ya laana ya wazazi, huna budi kuwahi kuwataka radhi kwa uliyowahi kuwakosea, kabla hawajatowea duniani.
5. Laana itokanayo na kula/kuiba fungu la kumi la Mungu
Laana hii imewafunika watu wengi sana makanisani. Unakuta mtu anafanya biashara au ni mfanyakazi katika ofisi au shirika fulani, lakini hana maendeleo yoyote. Wengine wanapokea mishahara mikubwa, lakini fedha inapotea katika mazingira yasiyo na maelezo kamili.
Kama wewe ni mmoja wapo, ambaye huoni mafanikio licha ya fedha nyingi unayoipata, biashara yako haikui licha ya kuwa unaitangaza sana, tambua kuwa unatembea chini ya laana kwa kutotoa fungu la kumi. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi (zaka-fungu la kumi), naam, taifa hili lote (Malaki 3:9). Amua kutoa fungu la kumi kila wiki au kila mwezi ili upate mabadiliko katika maendeleo yako.
6. Laana itokanayo na kumwaga damu
Watu wengi sana wanatembea na laana hii pasipo wao wenyewe kujua, kwa kuwaua watu (ili wapate mali na utajiri) au kwa kutoa mimba. Ndiyo maana, utakuta wengine wana mali nyingi lakini hawana amani, na wengine wamehangaika kila sehemu kutafuta watoto, lakini hawapati. Ni kwa sababu wamesahau damu waliyoimwaga miaka mingi iliyopita, damu ambayo bado inadai kisasi juu yao, mbele za Mungu. Mfano wa Kaini na Abeli: Akasema (Mungu), umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako (Mwanzo 4:10-11).
7. Laana itokanayo na kufanya uzinzi na mzazi wako au mzazi wa mke au mume (mkwe) wako au ndugu yako wa damu
Laana hii huwapata hasa wale wanaotimiza masharti ya waganga wa kienyeji, ili kujipatia mali za kishirikina. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe (Kumbukumbu la Torati 27:20, 22-23).
Ni vitu gani vinaweza kulaaniwa
Kwanza wewe mwenyewe unaweza kupokea laana katika mwili wako. Pia, vitu unavyomiliki kama ardhi, nyumba, mifugo n.k huweza kulaaniwa kwa ajili yako.
MWILI WAKO: Unapata magonjwa yasiyo na sababu, ukifuatilia chanzo cha magonjwa au wapi ulipata maambukizo hakuna unakoweza kupata jibu. Na hata ukienda hospitali bado hupati uponyaji. Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni (magonjwa) (2Nyakati 7:13).
UZAO WAKO: Watoto wako wanakuwa wasumbufu haijawahi kutokea. Wana kiburi, wana tabia mbaya. Umetumia upole na ukali kuwakanya lakini hawakusikii. Au hata hawana mafanikio kwa kila jambo wanalolifanya. Utalaaniwa uzao wa tumbo lako (Torati 28:18).
KAZI ZA MIKONO YAKO NA UCHUMI WAKO KWA UJUMLA
Unafanya kazi au biashara ambayo huoni faida yake, zaidi ya kukupatia fedha ya kujikimu tu. Umekuwa na uchumi ule ule miaka nenda rudi na ndiyo kwanza unazidi kushuka chini. Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya (kazi na biashara zako), hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniachia kwayo (Torati 28:20).
ARDHI: Unailima ardhi lakini hupati mazao. Unazingatia kilimo cha kisasa lakini mavuno ni haba. Ndipo ikawashwa hasira ya Bwana juu ya nchi (ardhi) hii, kwa kuleta juu yake (ardhi) laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki (Torati 29:27).
MIFUGO YAKO: Unajitahidi kufuga mifugo kwa njia za kisasa, lakini mifugo haiongezeki. Ikizaa watoto wanakufa, au kila siku unaibiwa wewe. Mifugo yako inapotea pasipo kuonekana.
Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako (mifugo yako) (Torati 28:18).
Je, unaweza kuwa umelaaniwa pasipo wewe kujua
Unaweza kuwa ulifanya uovu au jambo lolote kati ya hayo yaliyoelezwa, yanayoweza kusababisha laana katika maisha yako, na bado hujaona matokeo ya hiyo laana katika maisha (isipokuwa kama ulitubu na kuvunja laana hiyo), kinyume cha hapo laana hiyo bado iko juu yako na inakufuatilia, kama siyo kukupata wewe basi ni uzao wako, kama ilivyo katika laana ya kurithiwa (Kumbukumbu la Torati 28:45-46).
Kuna sababu au vitu vingi vinavyoweza kukusababishia laana katika maisha yako, kazi au biashara yako, ama vitu unavyovimiliki kama shamba au nyumba.
Na kitu kibaya zaidi ni kwamba laana inarithiwa, kutoka kizazi kimoja kwenda kinachofuata. Unaweza usione matokea ya laana katika maisha yako ya sasa na ukaamua kunyamaza ilihali ukijua kuna mambo uliwahi kufanya yanayofanana na hayo yaliyosimuliwa kwenye somo hili. Nakuambia, hiyo laana ni lazima ikufuatilie kama siyo wewe basi ni uzao wako, na kuna watu wanaishi chini ya laana zilizosababishwa na wazazi wao ambao unaweza ukakuta walikwishafariki.
Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukusikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele (Kumbukumbu la Torati 28:45-46).
Nini kifanyike
1. Tutathmini kama tuna laana au la, sisi wenyewe au kupitia makanisa sahihi.
2. Tuepuke kutamka maneno hasi, kwetu wenyewe na kwa watu wengine, hata kwa kutania, kwani shetani hufuatilia na kufanyia kazi na kuharibu maendeleo yetu; ambayo ndiyo furaha yake shetani.
3. Tumtafute Mungu na kufuata maagizo na sheria zake na kuacha kutenda dhambi.