"Watu wasikamatwe kabla ya uchunguzi," Waziri Mkuu Majaliwa haimuhusu?

Zile no siasa tu watu wanakamatwa kila leo bila uchunguzi kufanywa wanasota rumande wakati uchunguzi unaendelea usiamini matamko ya wanasiasa hayana mashiko
 
Hii nchi kweli ina laana toka kwa Mwenyezi Mungu

Ni kwanini, huyo Waziri Mkuu, anakomalia hicho kibanda cha milioni 11, wakati tulimuona akikaa kimya, wakati ule CAG alipotoa taarifa kuwa pesa ya kiasi cha Shs trillion 1.5 ikiwa "imechotwa" toka hazina?🥺
 
Atupe kwanza ripoti za kuungua kwa masoko
 
Hizi gharama zinanzoonekaba kubwa inaweza kuwa ni kubwa kweli au may be sio kweli , na si rahisi sana kujua kwa macho bila kuangalia details.
Katika ujenzi kama huo unaotumia nguvu kazi gharama zinaweza kuwa kubwa kwa sababu zifuatazo:
1.Manunuzi ya vifaa kununuliwa kwa bei kubwa kuliko kawaida. _taratibu za manunuzi ziangaliwe
2.Ununuzi WA vifaa hewa. - kamati ya mapekezi ilifanya kazi yake?
3.Bei kubwa ya nguvukaza (labour) taratibu za manunuzi
 
Chain ya pesa za miradi huanzia mbali juu kabisa lakini wanaokuja kuwajibishwa ni hawa vidagaa wa mwisho.. Haki ikiamua kutendeka ikafuatiliwa chain yote wataondoka wengi na itakuwa ni kashfa kubwa kwakuwa kisu kitagusa mpaka mfupa
 
Zile no siasa tu watu wanakamatwa kila leo bila uchunguzi kufanywa wanasota rumande wakati uchunguzi unaendelea usiamini matamko ya wanasiasa hayana mashiko
Wanasiasa wenye kauli za majukwaani pekee hawatufai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…