Watu wasio na sifa humtumikia mtu na siyo nchi

Watu wasio na sifa humtumikia mtu na siyo nchi

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
3,156
Reaction score
3,628
Habari wana jamvi!

Nimekuwa nikifuatilia utendaji wa wateuliwa Wengi wa awamu ya tano nimebaini kwamba karibu wote hujitahidi sana kujua aliye wateua anataka nini na huishi katika hilo. Hawasomi standing orders wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwao wao kumfurahisha 'Kim Jong Un ' ndio kipaumbele.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa hakuna tofauti kati ya UV CCM na TAKUKURU,hakuna tofauti kati ya UV CCM na Tume ya uchaguzi,Hakuna tofauti kati ya Polisi na CCM! Wote adui yao ni mmoja CHADEMA NA MBOWE. Hawalali usingizi kisa Mbowe!

TAKUKURU wanatamani kumhoji Mbowe ambaye Chama kilipata hati safi na kamwe hawatamani kumhoji Magufuli ambaye chama chake kimepata hati chafu.

TAKUKURU hawaja peleka mahakamani faili la Kangi Lugola na kamwe hawatapeleka kwasababu Kangi aliahidi kusema ukweli wote! Ukweli upi! Wenye akili wanaujua.

TAKUKURU hawajawahi kutamani kuchunguza kama teuzi nyingi za awamu ya tano hazina upendeleo au harufu ya UKABILA.

BUNGE linejigeuza tawi la CCM kwa Maneno na vitendo. Ndio maana watu wamelichoka na kulidharau. Hakuna mtu anapoteza muda kusoma wala kusikiliza habari za Bunge.

Wanaona ni bora kumsoma kigogo 2014 kuliko kusikiliza bunge lililo poteza sifa.

Polisi huko ndio usiseme. Kumejiozea kitambo. Ila wanajua wanacho kifanya. Unafikiri wote wana kadi za CCM! Hawatumii akili tena bali wamesoma upepo unako elekea.
Kifupi ni kwamba kati ya hawa wateuliwa wa sasa wote wanawaza jambo moja tu, NITAMFURAJISHAJE KIM JONG UN? Ndio maana tunashuhudia ya ajabu awamu hii kutoka kwa watendaji kuliko awamu zote.

Ni kama hawa kuwa na sifa ila fursa imewakuta.

Ukishangaa ya Ndugai utakutana ya RPC aliye sema yasiyo elezeka.
 
Mtabweka Sana humu.mwambieni Mbowe arudishe bilioni nane aluzochukua
 
Mtu asiyekuwa mwizi haogppi polisi Wala Takukuru wakitaka kumkagua .Hana Cha kuogopa

Mbowe mbona ka panick ? Ku panick huwavutia polisi na Takukuru kuwa huyu mbona ka panick ngoja tumwendee tuone alicho panick Nini? Post zenu ndio zinawatia munkari zaidi Takukuru hamchomoki kadri mnavyozidi kupanick na kuhaha ndivyo mnavyowaamusha zaidi
 
BUNGE linejigeuza tawi la CCM kwa Maneno na vitendo. Ndio maana watu wamelichoka na kulidharau. Hakuna mtu anapoteza muda kusoma wala kusikiliza habari za Bunge.

Wanaona ni bora kumsoma kigogo 2014 kuliko kusikiliza bunge lililo poteza sifa.
Mkuu umeandika mengi kwenye mada yako, na najua unaelewa yapo mengi zaidi ya hayo uliyoamua kuyaelezea hapa ambayo ni machukizo ya utawala huu.

Binafsi nimevutiwa na hiyo mistari miwili na nusu inayowahusu wananchi na sio wateuliwa uliowekea mkazo wa mada yako.

Swali mhimu la kujiuliza sasa ni hili la wananchi wanaoona yote haya, wameyashuhudia Bungeni na kwingineko..., pamoja na kwamba wao sio 'wateuliwa' kwa nini hawaonyeshi kustushwa na mambo haya?

Au wameshtushwa ila hawataki kuonyesha dalili za kushtuka?

Serikali za mitaa, wakanyimwa haki ya kuchagua viongozi wao, wewe umeona sehemu yoyote wanachi walipostuka?

Dalili tayari zipo, kwamba hata uchaguzi mkuu Oktoba, hawa wananchi kura zao huenda zisiwe ndizo zitakazowapatia viongozi wao wa ngwe nyingine ya miaka mitano; wewe unaona dalili zozote zinazokuonyesha kuwepo kwa mfukuto wowote kuikataa dhuruma hiyo?

Kwa hiyo mkuu wangu 'JERUSALEMU' pamoja na kukubaliana na hoja yako kuwahusu hao wateule, jambo linaloshangaza zaidi kwa baadhi yetu ni hili swala la wananchi kuendelea kutostushwa na hayo wanayoyaona na wao kuwa kama hao wateuliwa uliowazungumzia, pamoja na kwamba wao sio wateule.

Au tuseme ni woga, wananchi wanaogopa madhara ya mabunduki na mapolisi?

Kwa nini wasielewe kwamba kwa umoja wao hakuna polisi na mabunduki vinavyoweza kushinda nguvu zao!

Hili kweli hawalijui, wanasubiri mpaka waelimishwe?

Yapo maswali mengi ya kuuliza juu ya hawa wananchi wa Tanzania, lakini hayo yanatosha kwa leo.
 
Huyo jamaa ni polisi, mwanajeshi, hakimu, Bwana jela, Mchungaji, Dr, injinia yaaani kila kitu yeye🔒🔓🔏🔐
Mtaalam wa gonjwa jipya 'COVID-19' hadi akagundua kujifukiza na kupima mapapai/mbuzi,n.k., kuonyesha kwa na wao vipimo vinaonyesha wana coronavirus!
Wataalam ambao ndio wanapaswa kuwa washauri wake wakuu, wakishauri asiyotaka, anafukuza kazi, kama naibu waziri na mkuu wa maabara.

Mtu anayejua kabla ya mashambulizi ya ugonjwa kufahamika, yeye tayari alishaoteshwa kuwa ni "kaugonjwa kadogo, kasitusumbue"; anaamua uchumi ni bora kuliko uhai wa wananchi wake! Bado watu wanashangilia maamuzi ya aina hiyo! Hii ni nchi ya watu wenye akili, au imekuwa nchi ya misukule?
 
Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
 
Mtu asiyekuwa mwizi haogppi polisi Wala Takukuru wakitaka kumkagua .Hana Cha kuogopa

Mbowe mbona ka panick ? Ku panick huwavutia polisi na Takukuru kuwa huyu mbona ka panick ngoja tumwendee tuone alicho panick Nini? Post zenu ndio zinawatia munkari zaidi Takukuru hamchomoki kadri mnavyozidi kupanick na kuhaha ndivyo mnavyowaamusha zaidi
Nina mashaka kuwa hata Mada hujaielewa, wakisema fisiemu mna akili finyu mnakataa lakini ukweli uko wazi kabisa, jaribu kujitafakiri kidogo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeandika mengi kwenye mada yako, na najua unaelewa yapo mengi zaidi ya hayo uliyoamua kuyaelezea hapa ambayo ni machukizo ya utawala huu.

Binafsi nimevutiwa na hiyo mistari miwili na nusu inayowahusu wananchi na sio wateuliwa uliowekea mkazo wa mada yako.

Swali mhimu la kujiuliza sasa ni hili la wananchi wanaoona yote haya, wameyashuhudia Bungeni na kwingineko..., pamoja na kwamba wao sio 'wateuliwa' kwa nini hawaonyeshi kustushwa na mambo haya?

Au wameshtushwa ila hawataki kuonyesha dalili za kushtuka?

Serikali za mitaa, wakanyimwa haki ya kuchagua viongozi wao, wewe umeona sehemu yoyote wanachi walipostuka?

Dalili tayari zipo, kwamba hata uchaguzi mkuu Oktoba, hawa wananchi kura zao huenda zisiwe ndizo zitakazowapatia viongozi wao wa ngwe nyingine ya miaka mitano; wewe unaona dalili zozote zinazokuonyesha kuwepo kwa mfukuto wowote kuikataa dhuruma hiyo?

Kwa hiyo mkuu wangu 'JERUSALEMU' pamoja na kukubaliana na hoja yako kuwahusu hao wateule, jambo linaloshangaza zaidi kwa baadhi yetu ni hili swala la wananchi kuendelea kutostushwa na hayo wanayoyaona na wao kuwa kama hao wateuliwa uliowazungumzia, pamoja na kwamba wao sio wateule.

Au tuseme ni woga, wananchi wanaogopa madhara ya mabunduki na mapolisi?

Kwa nini wasielewe kwamba kwa umoja wao hakuna polisi na mabunduki vinavyoweza kushinda nguvu zao!

Hili kweli hawalijui, wanasubiri mpaka waelimishwe?

Yapo maswali mengi ya kuuliza juu ya hawa wananchi wa Tanzania, lakini hayo yanatosha kwa leo.
Actually tatizo la msingi lipo hapo. Watanzania wamejaa uoga ! Lakini ipo siku wakihakikishiwa ushindi watasimama wataandamana na kuwakomesha viongozi wote wajinga.
 
Ulishajiuliza siku Kafa hao vidampa nini kitawatokea
 
Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
TAKUKURU wamepoteza sifa ya kuanzishwa kwake. Na kiongozi wao kutwa kucha na nguo za JWTZ as if ile ni ofisi ya Jeshi. Ofisi za kiraia unavaaje sare za Jeshi? Hajitambui na ndio maana kazi imemshinda.
 
Tumbo vs njaa...kila mtu anatetea tumbo lake.

Ukipingana na mkuu unatumbuliwa, option inabaki moja tu kumsifia sifia na wewe utaneemeka.

Angalia yule naibu waziri wa afya aliyetumbuliwa...hatujui hata halipo sasa.
 
Actually tatizo la msingi lipo hapo. Watanzania wamejaa uoga ! Lakini ipo siku wakihakikishiwa ushindi watasimama wataandamana na kuwakomesha viongozi wote wajinga.
Na kwa bahati mbaya sana wanaowatia uoga huo wanajua wakiua mmoja, wawili hata kumi kama mfano inatosha kabisa kuwaogopesha waliobaki na mambo yanaendelea kama kawaida.

"Kuhakikishiwa ushindi", hapo ndipo penye shida kubwa, kwa sababu hilo linahitaji uwepo wa uongozi wa kundi linalotaka ushindi. Uongozi huo ndio unaotakiwa kufanya kazi ya ziada kuwaelimisha wananchi kudai haki yao na kuitetea.

Uongozi wa aina hiyo bado haujajitokeza na kuchukua nafasi yao.
 
Back
Top Bottom