JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,156
- 3,628
Mkuu umeandika mengi kwenye mada yako, na najua unaelewa yapo mengi zaidi ya hayo uliyoamua kuyaelezea hapa ambayo ni machukizo ya utawala huu.BUNGE linejigeuza tawi la CCM kwa Maneno na vitendo. Ndio maana watu wamelichoka na kulidharau. Hakuna mtu anapoteza muda kusoma wala kusikiliza habari za Bunge.
Wanaona ni bora kumsoma kigogo 2014 kuliko kusikiliza bunge lililo poteza sifa.
Mtaalam wa gonjwa jipya 'COVID-19' hadi akagundua kujifukiza na kupima mapapai/mbuzi,n.k., kuonyesha kwa na wao vipimo vinaonyesha wana coronavirus!Huyo jamaa ni polisi, mwanajeshi, hakimu, Bwana jela, Mchungaji, Dr, injinia yaaani kila kitu yeye🔒🔓🔏🔐
Nina mashaka kuwa hata Mada hujaielewa, wakisema fisiemu mna akili finyu mnakataa lakini ukweli uko wazi kabisa, jaribu kujitafakiri kidogo tu.Mtu asiyekuwa mwizi haogppi polisi Wala Takukuru wakitaka kumkagua .Hana Cha kuogopa
Mbowe mbona ka panick ? Ku panick huwavutia polisi na Takukuru kuwa huyu mbona ka panick ngoja tumwendee tuone alicho panick Nini? Post zenu ndio zinawatia munkari zaidi Takukuru hamchomoki kadri mnavyozidi kupanick na kuhaha ndivyo mnavyowaamusha zaidi
Actually tatizo la msingi lipo hapo. Watanzania wamejaa uoga ! Lakini ipo siku wakihakikishiwa ushindi watasimama wataandamana na kuwakomesha viongozi wote wajinga.Mkuu umeandika mengi kwenye mada yako, na najua unaelewa yapo mengi zaidi ya hayo uliyoamua kuyaelezea hapa ambayo ni machukizo ya utawala huu.
Binafsi nimevutiwa na hiyo mistari miwili na nusu inayowahusu wananchi na sio wateuliwa uliowekea mkazo wa mada yako.
Swali mhimu la kujiuliza sasa ni hili la wananchi wanaoona yote haya, wameyashuhudia Bungeni na kwingineko..., pamoja na kwamba wao sio 'wateuliwa' kwa nini hawaonyeshi kustushwa na mambo haya?
Au wameshtushwa ila hawataki kuonyesha dalili za kushtuka?
Serikali za mitaa, wakanyimwa haki ya kuchagua viongozi wao, wewe umeona sehemu yoyote wanachi walipostuka?
Dalili tayari zipo, kwamba hata uchaguzi mkuu Oktoba, hawa wananchi kura zao huenda zisiwe ndizo zitakazowapatia viongozi wao wa ngwe nyingine ya miaka mitano; wewe unaona dalili zozote zinazokuonyesha kuwepo kwa mfukuto wowote kuikataa dhuruma hiyo?
Kwa hiyo mkuu wangu 'JERUSALEMU' pamoja na kukubaliana na hoja yako kuwahusu hao wateule, jambo linaloshangaza zaidi kwa baadhi yetu ni hili swala la wananchi kuendelea kutostushwa na hayo wanayoyaona na wao kuwa kama hao wateuliwa uliowazungumzia, pamoja na kwamba wao sio wateule.
Au tuseme ni woga, wananchi wanaogopa madhara ya mabunduki na mapolisi?
Kwa nini wasielewe kwamba kwa umoja wao hakuna polisi na mabunduki vinavyoweza kushinda nguvu zao!
Hili kweli hawalijui, wanasubiri mpaka waelimishwe?
Yapo maswali mengi ya kuuliza juu ya hawa wananchi wa Tanzania, lakini hayo yanatosha kwa leo.
TAKUKURU wamepoteza sifa ya kuanzishwa kwake. Na kiongozi wao kutwa kucha na nguo za JWTZ as if ile ni ofisi ya Jeshi. Ofisi za kiraia unavaaje sare za Jeshi? Hajitambui na ndio maana kazi imemshinda.Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Na kwa bahati mbaya sana wanaowatia uoga huo wanajua wakiua mmoja, wawili hata kumi kama mfano inatosha kabisa kuwaogopesha waliobaki na mambo yanaendelea kama kawaida.Actually tatizo la msingi lipo hapo. Watanzania wamejaa uoga ! Lakini ipo siku wakihakikishiwa ushindi watasimama wataandamana na kuwakomesha viongozi wote wajinga.