Pre GE2025 Watu Wasiojulikana: Malisa aelezea tukio la kutekwa kwa Deus Soka na vijana wengine wawili wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yeye aniwaiga kina Mbowe wale wanajuwa siasa ya nchi na ile Chadema ni mradi wake wakupigia tu ndani ya nafsi anajuwa fika hawezi kuchukuwa nchi ila anatumika tu kama wengine. shida watu wanawaamini hawa watu.
"Huu ndio ukweli mchungu hawataki kuusikia" (Heijah )

Vijana wanatumika bila kujijua, ukiwashauri unaonekana ni mtetezi wa CCM Kalamu
 
Mkuu 'Stuxnet' naomba usiniingize kwenye haya makundi yenu, nilisha malizana nayo muda mwingi uliopita.

Kwa mfano, sioni hapa unataka nijadili "ukweli" upi hasa!
Kwamba waTanzania watake wasitake ni halali yao CCM kuwatawala milele?
Mawazo ya namna hii mimi sinayo kabisa.
 
1000033226.jpg
 
Nimetafakari na kulinganisha uanaharati wa Soka,kijana wa Bavicha Temeke,nikafanya ulinganifu na yaliyompata Steve Beko wa Afrika ya kusini wakati wa kupigania uhuru je vinalingana? au ni uhalifu kama uhalifu mwingine. Tujadili
 
Tanzania ilishajipatia uhuru wake 1961....

Uhuru gani tena mwingine ?!!

Hisia za KIHAINI nini ?!! [emoji44][emoji44]
 
Huu siyo utamaduni mzuri, tujifunze kustaarabika - siasa, dini kwa nn zitujengee ukuta hivyo?
  • Mbn ni kawaida MTU kushindwa!
  • Mbn ni kawaida chama kushindwa!
  • Mbn Mungu katoa njia nyingi za kuishi - kwamba siasa ikigoma utalima, utafanya biashara nk nk

Kutekana na kuuana si utamaduni mzuri
 
Wanaharakati wa haki za binadamu na wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakipaza sauti kupitia X kijana wao Deusdedith Soka kuchukuliwa na wanaosemekana na polisi na mpaka sasa hajulikani alipo.

Vijana wengine kutoka CHADEMA ambao ambao hawajulikani walipo baada ya sekeseke la maandamano ya BAVICHA ni Jacob Mlay na Frank Mbise.

Malisa ameandika haya;

Leo ni siku ya 5 vijana watatu wa Chadema wanaodaiwa kutekwa huko Temeke hawajulikani walipo. Deus Soka, Jacob Mlay na Frank Mbise.

Siku ya tukio Soka alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari akimtaka afike polisi Chang'ombe kwa utambuzi wa pikipiki yake iliyoibiwa mwaka 2023.

Soka alikua anamiliki pikipiki, akampa mshkaji wake Frank Mbise aendeshe, lakini ikaibiwa. Wakatoa taarifa Polisi Chang'ombe ambapo lilifunguliwa jalada la uchunguzi.

Pia soma: Kuelekea 2025 - CHADEMA yadai Viongozi wake Wilayani Temeke wameshikiliwa, Polisi wakana

Kwahiyo alipopigiwa simu kwamba pikipiki imepatikana ilikua habari njema. Akamjulisha Frank waende pamoja maana ndiye aliyekua na pikipiki wakati inaibiwa. Akampigia pia Katibu wa Chadema Wilaya ya Temeke, Jacob Mlay kumjulisha kuhusu wito wa Polisi. Mlay akamshauri waende pamoja. Kwahiyo ikawa timu ya watu watatu; Deus Soka, Frank Mbise na Jacob Mlay.

Wakiwa wanaelekea kituoni kupanda gari ilitokea Noah nyuma yao. Ghafla wakatoka watu wenye silaha na kuwaamuru kuingia. Kabla hawajafanya lolote wakaporwa simu zao na kisha gari ikaondolewa kwa kasi.

Baadhi ya Mashuhuda wanasema waliona vijana watatu wanatembea na ghafla ikaja Noah wakatoka watu wenye makoti, kisha wale vijana wakaingia ndani. Hawakuelewa kama lilikua tukio la utekaji.

Taarifa imetolewa Polisi lakini wamekanusha kuwashikilia na wamekanusha kumpigia simu Soka akafuate pikipiki yake.

Lakini familia haina imani na Polisi kwa sababu, Polisi walikanusha kumshikilia Kombo Mbwana, lakini baada ya siku 29 wakakiri yupo mikononi mwao. Pia ni Polisi haohao waliokanusha kumshikilia Robert Mushi lakini baada ya siku 10 mwili wake ukakutwa hospitali ya Polisi Kilwa Road.

Familia ya Soka inadai ndugu yao amekua akipokea vitisho kutoka kwenye vyombo vya Dola. Tar 10 August vijana wa Chadema Temeke walikamatwa wakielekea Mbeya kwenye kongamano la Bavicha, wakapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe, lakini Soka alipelekwa Kilwa Road. Tar.12 Soka alitolewa Kilwa Road na kupelekwa Chang'ombe ili akapewe dhamana pamoja na wenzie.

Soka aliwaeleza ndugu zake kwamba akiwa kwenye gari la Polisi kutoka Kilwa Road kwenda Chang'ombe, askari mmoja mwenye marasta alimwambia "muda si mrefu tutamalizana na wewe mazima."
Vijana wanatumika vibaya kwa manufaa ya wanasiasa. Eti anaitwa Steve Biko. Na hizo sifa za kipumbavu wanazivaa na kujitosa mazima kwa vitu ambavyo havipo. Deusdedith Soka alitamka kuwa anaipigania nchi yake hivyo ndugu zake wamuache tu. Ni nchi gani Soka anaipigania? Badala ya kuhangaika kupata mkate wake kwa shughuli za uchumi, eti yuko kwenye maandamano, mitandao na maneno mazito ya kukera wanasiasa
 
kila Mtu ana haki ya kufanya siasa, siyo kila neno linalotamkwa na wanasiasa watawala linawafurahisha wananchi wote. kutekana ni jambo baya sana
 
Wanaharakati wa haki za binadamu na wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakipaza sauti kupitia X kijana wao Deusdedith Soka kuchukuliwa na wanaosemekana na polisi na mpaka sasa hajulikani alipo.

Vijana wengine kutoka CHADEMA ambao ambao hawajulikani walipo baada ya sekeseke la maandamano ya BAVICHA ni Jacob Mlay na Frank Mbise.

Malisa ameandika haya;

Leo ni siku ya 5 vijana watatu wa Chadema wanaodaiwa kutekwa huko Temeke hawajulikani walipo. Deus Soka, Jacob Mlay na Frank Mbise.

Siku ya tukio Soka alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari akimtaka afike polisi Chang'ombe kwa utambuzi wa pikipiki yake iliyoibiwa mwaka 2023.

Soka alikua anamiliki pikipiki, akampa mshkaji wake Frank Mbise aendeshe, lakini ikaibiwa. Wakatoa taarifa Polisi Chang'ombe ambapo lilifunguliwa jalada la uchunguzi.

Pia soma: Kuelekea 2025 - CHADEMA yadai Viongozi wake Wilayani Temeke wameshikiliwa, Polisi wakana

Kwahiyo alipopigiwa simu kwamba pikipiki imepatikana ilikua habari njema. Akamjulisha Frank waende pamoja maana ndiye aliyekua na pikipiki wakati inaibiwa. Akampigia pia Katibu wa Chadema Wilaya ya Temeke, Jacob Mlay kumjulisha kuhusu wito wa Polisi. Mlay akamshauri waende pamoja. Kwahiyo ikawa timu ya watu watatu; Deus Soka, Frank Mbise na Jacob Mlay.

Wakiwa wanaelekea kituoni kupanda gari ilitokea Noah nyuma yao. Ghafla wakatoka watu wenye silaha na kuwaamuru kuingia. Kabla hawajafanya lolote wakaporwa simu zao na kisha gari ikaondolewa kwa kasi.

Baadhi ya Mashuhuda wanasema waliona vijana watatu wanatembea na ghafla ikaja Noah wakatoka watu wenye makoti, kisha wale vijana wakaingia ndani. Hawakuelewa kama lilikua tukio la utekaji.

Taarifa imetolewa Polisi lakini wamekanusha kuwashikilia na wamekanusha kumpigia simu Soka akafuate pikipiki yake.

Lakini familia haina imani na Polisi kwa sababu, Polisi walikanusha kumshikilia Kombo Mbwana, lakini baada ya siku 29 wakakiri yupo mikononi mwao. Pia ni Polisi haohao waliokanusha kumshikilia Robert Mushi lakini baada ya siku 10 mwili wake ukakutwa hospitali ya Polisi Kilwa Road.

Familia ya Soka inadai ndugu yao amekua akipokea vitisho kutoka kwenye vyombo vya Dola. Tar 10 August vijana wa Chadema Temeke walikamatwa wakielekea Mbeya kwenye kongamano la Bavicha, wakapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe, lakini Soka alipelekwa Kilwa Road. Tar.12 Soka alitolewa Kilwa Road na kupelekwa Chang'ombe ili akapewe dhamana pamoja na wenzie.

Soka aliwaeleza ndugu zake kwamba akiwa kwenye gari la Polisi kutoka Kilwa Road kwenda Chang'ombe, askari mmoja mwenye marasta alimwambia "muda si mrefu tutamalizana na wewe mazima."

"We were forced to form a Paramilitary Wing of uMkhonto we Sizwe within the ANC because the Government of Whites Minorities of South Africa was terrorising us by using the State Security Forces."

Oliver Reginald Tambo, former President of African National Congress (ANC) from 1967 to 1993.
 
Back
Top Bottom