Watu wawili wauawa kwa kuchinjwa kisa wivu wa mapenzi

Watu wawili wauawa kwa kuchinjwa kisa wivu wa mapenzi

Mi mwenyewe hapa nusura nihusishwe katika tukio la wivu wa kimapenzi wakati vijana wawili wakituangana makonde baada ya kijana mmoja anayedai kuwa ni mmiliki wa msichana kumtuhumu kijana mwenzake amemkuta akichati naye. Kijana mwenye binti ndiye aliyeshambuliwa zaidi japo yeye ndiye aliyeonesha wivu kwa kuanzisha ugomvi.

Mimi nilihusishwa kuwa huwa namtongoza binti huyo na tayari nilishapewa onyo kwa kutukanwa vibaya ila sikuacha kumtongoza huyo binti kwa kuwa alinieleza kuwa huyo jamaa yake mwenye wivu ni mpenzi tu na si mume anayetambulika, ndio na mimi nikaona nipambanie kumpata binti huyo. Ugomvi wa vijana hao ulinifanya nijitoe kumtaka binti huyo isiwe taabu.

Ni bora kama mtu ana mpenzi aseme wazi tu ana mtu na hakuna nafasi ya kuchepuka kwa mwingine itasaidia kuepusha wivu na kutokea madhara
Bora umekaa pembeni, kuna watu ni vichaa!
 
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen ( 23) wakazi wa Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikidiwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 19, 2023 katika Kitongoji cha Imbambe, Kijiji Cha Kagwira, Kata ya Kabungu, ambapo marehemu hao wamekutwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa pembezoni mwa barabara.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira, Shila Benedicto amesema marehemu hao walikutwa na madhila hiyo wakiwa njiani kurudi nyumbani wakitokea Kijiji cha Kabungu walikokuwa wakifanyia shughuli zao.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema wanawashikilia watu wawili kwa ajili ya mahojiano, huku akieleza kuwa tukio hilo lina sura ya wivu wa kimapenzi kwa kuwa wamebaini mmoja wa marehemu alikuwa akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake.

Kamanda ngonyani amesema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
Mapenzi![emoji3064][emoji1544] ona sasa wamegawana majengo ya serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi![emoji3064][emoji1544] ona sasa wamegawana majengo ya serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Maafa kwenye mapenzi mara nyingi huletwa na hasira kali ambazo hazikawii kuisha na kufuatiwa na majuto makuu. Mtu anaweza kuumiza au kuumizwa akigombea demu wa kawaida kabisa wakati angeweza kupata mwingine mkali zaidi kama angedharau..
 
shida mikoani mademu wazuri wachache kutokana namaisha duni hadi waje dar ndio wananawiri

serikali iboreshe maisha yavijijini mademu wale na kuvaa vizuri Ili vijana kumi wasigombanie demu mmoja.

au la nichagueni Mimi niwe raisi nitawafanyia yote hayo hakutakuwa na ugomvi
 
Kwa hiyo ukiwasiliana na Mpenzi wako baadae akaja kufia kwa mchepuko wake ambaya wala huna habari naye tayari unawekwa ndani.

Si kuna ile unachati naye huku anaelekea kwa mchepuko kupigwa kambumbu......itokee afie huko sasa ndip utamjua Kamanda wa Mkoa ni nani😆😆
 
shida mikoani mademu wazuri wachache kutokana namaisha duni hadi waje dar ndio wananawiri

serikali iboreshe maisha yavijijini mademu wale na kuvaa vizuri Ili vijana kumi wasigombanie demu mmoja.

au la nichagueni Mimi niwe raisi nitawafanyia yote hayo hakutakuwa na ugomvi
Huu ni ukweli mkubwa sana. Ndio maana wanawake wa Dar karibu wote ni wazuri.

Sababu ya mazingira masafi, lotion, kuoga kwa wingi na mapocho pocho ya kula
 
Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wapenzi Katalina Juma (21) na Athanas Alyen ( 23) wakazi wa Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wamekutwa wakiwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali, huku chanzo kikidiwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 19, 2023 katika Kitongoji cha Imbambe, Kijiji Cha Kagwira, Kata ya Kabungu, ambapo marehemu hao wamekutwa wamefariki dunia kwa kuchinjwa na kutupwa pembezoni mwa barabara.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagwira, Shila Benedicto amesema marehemu hao walikutwa na madhila hiyo wakiwa njiani kurudi nyumbani wakitokea Kijiji cha Kabungu walikokuwa wakifanyia shughuli zao.

Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Kaster Ngonyani amesema wanawashikilia watu wawili kwa ajili ya mahojiano, huku akieleza kuwa tukio hilo lina sura ya wivu wa kimapenzi kwa kuwa wamebaini mmoja wa marehemu alikuwa akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake.

Kamanda ngonyani amesema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mara utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
'akiwasiliana na watu ambao walikuwa wapenzi wake'!? Huyu alikuwa sex machine.
 
Hayo ndio matokeo ya kukimbilia na kuendekeza mapenzi. Maana kizazi cha sasa asilimia kubwa wanaendwkeza mapenzi zaidi kuliko kitu kingine mwishowe ni kifo.
 
Hayo ndio matokeo ya kukimbilia na kuendekeza mapenzi. Maana kizazi cha sasa asilimia kubwa wanaendwkeza mapenzi zaidi kuliko kitu kingine mwishowe ni kifo.
Ni kutokana na kile wanachokiona na kukisikia kwenye jamii.

Na hasa hada kupitia bogo fleva na bongo movie.
 
Wivu wa mapenzi mda mwingine ni kuupa kiki tuu, sio kila kifo kinachohusisha jinsia mbili tofauti ni mapenzi.

Japo hii ya wivu wa mapenzi itabeba wengi sana, Unachati zako na danga huko, wamekurupushana kwa mambo mengine, kala kisu, Wanakuunganisha...
Unachati na Demu umemtaja taja jamaa yake kwenye msg, Kesho jamaa kala chuma mtaani, Namba utaisoma.
 
Back
Top Bottom