Watu wazima wanaojitapa kuzaliwa Dar ni mojawapo ya watu wa ovyo sana

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Huwa nikimuona mtu mzima anajisifia kuzaliwa Dar na kuwaita wengine washamba wa kuja namuona kama mtu mwenye akili fyatu, kubwa jingwa fulani hivi.

Kipi hasa cha mtu kujivunia na kutambia wengine kuzaliwa Dar? Mtu mwenyewe anayejitapa unakuta ni chawa wa watu kutoka nje ya Dar au hana hata kibanda hiyo Dar yenyewe.

Halafu ni wapuuzi gani walioanzisha utaratibu wa kuita maeneo yote ya nje ya Dar "mkoani"?!
 
Wengi wao ni mabwabwa na madalali hadi wa mapenzi.Mungu awarehemu.
NB:Huwa wanajinasibu wamezaliwa "Osheni rodi"!Bloody oceans!
 
Eeh haujui au?inawezekana sio wewe ila Kuna asilimia kubwa sana wanatamani

Kuna wengine wanasoma kwa bidii ili elimu iwafikishe dar na wengine wanalima kwa bidii ili wapate nauli ya kwenda dar

Oya japo dar Ina kasoro zake ila dar ni dar tu
Basi kuna Watanzania wana ndoto ndogo sana.
 
Matapeli yasiyo na shughuli rasmi ndo hujitapa kuwa watoto wa mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…