Watu wazuri hawafi 😳

Watu wazuri hawafi 😳

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
221
Reaction score
542
Kwa kauli mzee Makamba aliyoitoa tena tena mbele ya mkutano mkuu kuwa watu wazuri hawafi, inafikirisha na kuhuzunisha.

Ukitizama umri na busara alizotegemewa kuwa nazo mzee huyu bado tunashindwa kuamini kuwa J. K Nyerere alikua mtu mbaya, mzee Mkapa alikua mtu mbaya, hayati Karume alikua mtu mbaya, Allan Kijazi, Mfugale, Augustin Mahiga, JPM, hayati bibi Titi Mohammed, wapigania uhuru wote na wapendwa wazazi wetu, watoto wetu, wake zetu, ndugu na jamaa zetu wote waliotangulia mbele za haki walikua watu wabaya. Kauli hii iliyokosa busara inatufanya tuamini huenda kuondoka kwa baadhi ya watu, Kuna watu nyuma ya hili, ukizingatia watanzania wengi siyo wapumbavu kiasi cha kushindwa kuelewa maana halisi ya haya maneno kwakua yalitamkwa kwa mukusudi na kwa dhamira halisi ya kuaminisha watu kuwa wapendwa wetu walikua watu wabaya kitu ambacho si kweli.

Watanzania tumewasikia vizuri na pamoja Rais Samia aliitolea ufafanuzi kauli hii bado haijafuta dhamira halisi na uhalisia wa kilichokusudiwa na mzee huyu kusimanga wapendwa wetu tena mbele ya wajane, watoto, ndugu na jamaa na marafiki huku akijiona yeye na mzee Kikwete kuwa ndio watu wema na vifo havitawakuta.

Ushauri kwa CCM
Siyo kila mzee anaweza kuwa na busara japo wapo wazee wengi wenye busara na tunawaheshimu kwaiyo CCM tazameni upya bunch ya wazee wenu, wengine wanapaswa kwenda kupumzika mapema ili kupisha vijana maana muda wao umeshapita, mtawaita kwa Ushauri tu pale mnapowahitaji.

Kauli ya Makamba inatengeneza taswira kuwa amefurahia vifo vya baadhi ya watu na pengine inatufikirisha kuwa huenda alitambua au kufahamu vifo vya baadhi ya watu maana kauli yake inafsirika kama mafanikio, furaha, ushindi na accomplishment ya mpango fulani uliofanikiwa vema, kwaiyo hii inamaana hivi vifo ni mafanikio kwa CCM au kikundi kidogo ndani ya CCM.

Na Ushauri wa mwisho kwa SSH, pamoja na urais kuwa taasisisi bado Rais ni wewe, utalaumiwa kwa mabaya yanayoendelea na kusifiwa kwa mazuri na legacy yako itakutaja wewe kama Rais kwaiyo ni wakati sasa wakuangalia washauri wako na watu walokuzunguka maana baadhi yao ni watu wenye interested binafsi hasa za kibiashara kwaiyo hawaoni hatari kukuharibia wewe ili mambo yao yafanikiwe.

Zaidi ya yote, Kuna moto unawaka chini chini na soon utalipuka, swala la kujiuliza ni je moto utakapolipuka bado kutakuwa na nafasi ya kuuzima au itakuwa too late.

Hawa wazee ni miongoni mwa familia za walamba asali ambao wamelewa kiburi cha uzima na madaraka. Kuwa na genge la aina hii ya viongozi ni miongoni mwa laana kuu ambazo nchi hii imewahi kuzipata.
 
Nilishangaa sana sana kusikia kasema vile live on record. Lazima kutakua na consequences.
 
Bila kupindisha maneno Jiwe alikuwa mtu mbaya sana kwa Taifa la Tanzania
 
Kwa kauli mzee Makamba aliyoitoa tena tena mbele ya mkutano mkuu kuwa watu wazuri hawafi, inafikirisha na kuhuzunisha.

Ukitizama umri na busara alizotegemewa kuwa nazo mzee huyu bado tunashindwa kuamini kuwa J. K Nyerere alikua mtu mbaya, mzee Mkapa alikua mtu mbaya, hayati Karume alikua mtu mbaya, Allan Kijazi, Mfugale, Augustin Mahiga, JPM, hayati bibi Titi Mohammed, wapigania uhuru wote na wapendwa wazazi wetu, watoto wetu, wake zetu, ndugu na jamaa zetu wote waliotangulia mbele za haki walikua watu wabaya. Kauli hii iliyokosa busara inatufanya tuamini huenda kuondoka kwa baadhi ya watu, Kuna watu nyuma ya hili, ukizingatia watanzania wengi siyo wapumbavu kiasi cha kushindwa kuelewa maana halisi ya haya maneno kwakua yalitamkwa kwa mukusudi na kwa dhamira halisi ya kuaminisha watu kuwa wapendwa wetu walikua watu wabaya kitu ambacho si kweli.

Watanzania tumewasikia vizuri na pamoja mhe SSH aliitolea ufafanuzi kauli hii bado haijafuta dhamira halisi na uhalisia wa kilichokusudiwa na mzee huyu kusimanga wapendwa wetu, kujiona yeye na mzee Kikwete kuwa ndio watu wema.

Ushauri kwa CCM

Siyo kila mzee anaweza kuwa na busara japo wapo wazee wengi wenye busara na tunawaheshimu kwaiyo CCM tazameni upya bunch ya wazee wenu, wengine wanapaswa kwenda kupumzika mapema ili kupisha vijana maana muda wao umeshapita, mtawaita kwa Ushauri tu pale mnapowahitaji.

Kauli ya Makamba inatengeneza taswira kuwa amefurahia vifo vya baadhi ya watu na pengine inatufikirisha kuwa huenda alitambua au kufahamu vifo vya baadhi ya watu maana kauli yake inafsirika kama mafanikio, furaha, ushindi na accomplishment ya mpango fulani uliofanikiwa vema, kwaiyo hii inamaana hivi vifo ni mafanikio kwa CCM au kikundi kidogo ndani ya CCM.

Na Ushauri wa mwisho kwa SSH, pamoja na urais kuwa taasisisi bado Rais ni wewe, utalaumiwa kwa mabaya yanayoendelea na kusifiwa kwa mazuri na legacy yako itakutaja wewe kama Rais kwaiyo ni wakati sasa wakuangalia washauri wako na watu walokuzunguka maana baadhi yao ni watu wenye interested binafsi hasa za kibiashara kwaiyo hawaoni hatari kukuharibia wewe ili mambo yao yafanikiwe.

Zaidi ya yote, Kuna moto unawaka chini chini na soon utalipuka, swala la kujiuliza ni je moto utakapolipuka bado kutakuwa na nafasi ya kuuzima au itakuwa too late.
Acha nikujulishe kuwa hakuna watu wapumbavuu katika ccm kama hao wazee. Hao wakina nape ni chamtoto
 
Bila kupindisha maneno Jiwe alikuwa mtu mbaya sana kwa Taifa la Tanzania
Mzee Makamba kasema watu wazuri hawafi ndo maana yeye na mzee Kikwete bado wapo, je sisi watanzania wengine tuliofiwa na ndugu, jamaa na marafiki zetu walikua watu wabaya? Siyo Habari ya Jpm.
 
Ccm kiukweli hakuna mwema wote niwabaya na ni watu makatili sanaaa ukitaka kujua kuwa nimakatili ingia kwenye anga zao wakati wa uchaguzi wako radhi kukuuwa ilichama na mgombea wao ashinde kwahiyo mm sishangai hiyo kauli ya huyo mnufaika wa ccm
 
Maneno ya Makamba ya maana kubwa sana... think beyond.. Na maneno ya JK ni mazito... Kuna jambo...linakuja. kwa ufupi Nivitisho kwa Mheshimiwa SSH..
 
Haya ni matunda ya mfumo mbovu alioujenga Nyerere
Nyerere mimi alinishangaza kitu kimoja. Alijua fika kuwa katiba yetu ni mbovu na inaweza kumfanya hata kiongozi mzuri kuwa dikteta lakini pamoja na influence kubwa aliyokuwa nayo hakutaka kuibafilisha. Matokeo yake hadi leo tunateswa na mambo aliyoyaanzisha yeye
 
Maneno ya Makamba hayana shida, kwa kuwa yamekidhi malengo. Wala hakulengwa JK Nyerere au Benjamin Mkapa kama watu wanavyotaka tuelewe. Aliyelengwa ni Magufuli, period. Na Magufuli deserves this kwa UFEDHULI aliowafanyia hawa wazee.

Unapoona wapenzi wa Magufuli wamechafukwa Big Time basi ujuwe ujumbe umefika sawa sawa by 100%.

Ukipanda ubaya utavuna ubaya, ukipanda mema utavuna mema.

Ulikuwa ni UHAYAWANI na USHAMBA kwa Magufuli kuwa rekodi mazungumzo ya faragha wale wazee kisha kuyaweka public kwenye mitandao ya jamii. Kwani walichosema kibaya kwenye zile voice notes ni nini? Kumuita mshamba? Kwani hakuwa mshamba? Ingekuwa wanataka kupindua nchi kweli hapo ingekuwa TREASON. Ni nani hasemwi duniani? Hata mitume akina Yesu na Muhammad walisemwa lakini yule Pimbi wa Chato akaona ngoja awadhalilishe.

Nasimama na Mzee Makamba
 
Mzee Makamba kasema watu wazuri hawafi ndo maana yeye na mzee Kikwete bado wapo, je sisi watanzania wengine tuliofiwa na ndugu, jamaa na marafiki zetu walikua watu wabaya? Siyo Habari ya Jpm.
Makamba ni nani kwani ili maneno yake ndiyo yako sahihi? Kifo ni lazima kwa kila binadamu, ila ukiwa muovu kama Jiwe watu wanaweza kukuombea kifo chako kiwahi kama Watanzania walivyofanya kwa Jiwe
 
Matendo ya Magufuli yalikuwa ya HOVYO sana na yalikuwa hayamfurahishi Mungu. Kwa mfano anawatoa kazini wenye vyeti FEKI na kuwanyima mafao, huku unambakiza Makonda mwenye cheti feki kama Mkuu wa mkoa.

Unawabomolea nyumba bila kuwalipa watu wa Kimara, halafu nyumba za wasukuma wa Mwanza unasema zisibomolewe.

Watu wanatoa Kodi lakini wana mbunge wa UPINZANI Magufuli anasema hapekeki maendeleo.

Anawanyanga'anya matajiri fedha kwa kisingizio cha ufisadi kisha kuwatupa rumande.

Halafu Jumapili anakwenda Kanisani na kusema "niombeeni". Tukuombee nini shetani mkubwa Magufuli?

Kwa kweli tulimuombea afe na Mungu akatusikia, DUBWASHA LIKAFA
 
Mkuu umeongea fact na kwa uchungu sana.
 
Back
Top Bottom