Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 221
- 542
Kwa kauli mzee Makamba aliyoitoa tena tena mbele ya mkutano mkuu kuwa watu wazuri hawafi, inafikirisha na kuhuzunisha.
Ukitizama umri na busara alizotegemewa kuwa nazo mzee huyu bado tunashindwa kuamini kuwa J. K Nyerere alikua mtu mbaya, mzee Mkapa alikua mtu mbaya, hayati Karume alikua mtu mbaya, Allan Kijazi, Mfugale, Augustin Mahiga, JPM, hayati bibi Titi Mohammed, wapigania uhuru wote na wapendwa wazazi wetu, watoto wetu, wake zetu, ndugu na jamaa zetu wote waliotangulia mbele za haki walikua watu wabaya. Kauli hii iliyokosa busara inatufanya tuamini huenda kuondoka kwa baadhi ya watu, Kuna watu nyuma ya hili, ukizingatia watanzania wengi siyo wapumbavu kiasi cha kushindwa kuelewa maana halisi ya haya maneno kwakua yalitamkwa kwa mukusudi na kwa dhamira halisi ya kuaminisha watu kuwa wapendwa wetu walikua watu wabaya kitu ambacho si kweli.
Watanzania tumewasikia vizuri na pamoja Rais Samia aliitolea ufafanuzi kauli hii bado haijafuta dhamira halisi na uhalisia wa kilichokusudiwa na mzee huyu kusimanga wapendwa wetu tena mbele ya wajane, watoto, ndugu na jamaa na marafiki huku akijiona yeye na mzee Kikwete kuwa ndio watu wema na vifo havitawakuta.
Ushauri kwa CCM
Siyo kila mzee anaweza kuwa na busara japo wapo wazee wengi wenye busara na tunawaheshimu kwaiyo CCM tazameni upya bunch ya wazee wenu, wengine wanapaswa kwenda kupumzika mapema ili kupisha vijana maana muda wao umeshapita, mtawaita kwa Ushauri tu pale mnapowahitaji.
Kauli ya Makamba inatengeneza taswira kuwa amefurahia vifo vya baadhi ya watu na pengine inatufikirisha kuwa huenda alitambua au kufahamu vifo vya baadhi ya watu maana kauli yake inafsirika kama mafanikio, furaha, ushindi na accomplishment ya mpango fulani uliofanikiwa vema, kwaiyo hii inamaana hivi vifo ni mafanikio kwa CCM au kikundi kidogo ndani ya CCM.
Na Ushauri wa mwisho kwa SSH, pamoja na urais kuwa taasisisi bado Rais ni wewe, utalaumiwa kwa mabaya yanayoendelea na kusifiwa kwa mazuri na legacy yako itakutaja wewe kama Rais kwaiyo ni wakati sasa wakuangalia washauri wako na watu walokuzunguka maana baadhi yao ni watu wenye interested binafsi hasa za kibiashara kwaiyo hawaoni hatari kukuharibia wewe ili mambo yao yafanikiwe.
Zaidi ya yote, Kuna moto unawaka chini chini na soon utalipuka, swala la kujiuliza ni je moto utakapolipuka bado kutakuwa na nafasi ya kuuzima au itakuwa too late.