Watu wengi hawana furaha na maisha yao

Watu wengi hawana furaha na maisha yao

Blue-ish

Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
63
Reaction score
120
Mengi huja kwa njia tofauti tofauti katika haya maisha,Kila kinachokuja na kutokea katika maisha yako kichukulie kama njia moja wapo ya kujifunza kwako.

Maisha mazuri ni yale yakukubaliana na hali uliyo nayo,kuridhika na kile ulichonacho kile ambacho kila ufunguapo macho unakutana nacho na sio kile unachokitamani ikiwa hakipo karibu yako.
 
Mara nyingi tamaa ndo huwa zinawaponza watu wengi.
Unakuta mtu anashindwa kuzidhibiti tamaa zake anaanza kutamani vitu vya watu wengine wakati anajua uwezo wa kuvimiliki Hana.
 
Mengi huja kwa njia tofauti tofauti katika haya maisha,Kila kinachokuja na kutokea katika maisha yako kichukulie kama njia moja wapo ya kujifunza kwako.

Maisha mazuri ni yale yakukubaliana na hali uliyo nayo,kuridhika na kile ulichonacho kile ambacho kila ufunguapo macho unakutana nacho na sio kile unachokitamani ikiwa hakipo karibu yako.
Maisha haya tunaangaika sana kutafuta furaha kwenye vitu ambavyo hatuna uwezo navyo. Na hali inachochewa sana na mfumo wa maisha wa siku hizi ya kidigitali, mf. Kwenye mitandao ya kijamii watu wengi wanajiaminisha kuwa wanamaisha mazuri, yakitajiri na yenye furaha sana lakini uhalisia ni tofauti, jaribu kuangalia ndugu jamaa na marafiki wanaotuzunguka kuna utofauti sana kati ya maisha wanayo jaribu kuonyesha kwenye mitandao ya kijamii na maisha yao ya kweli. Hivyo hali hii hupelekea watu wengine hususani vijana kutokubali maisha yao na kuanza kuishi maisha ya kuigiza.

Ndio maana watu wengi hawana furaha na maisha yao kutokana na unyonge wanao upata wakiangalia maisha yasio na uhalisia mitandaoni

ISHI MAISHA YAKO YA UKWELI, MUDA MWINGINE KUFANIKIWA KUNAKUJA NA KUKUBALI HALI ULIO NAYO KWANZA
 
Back
Top Bottom