Maisha haya tunaangaika sana kutafuta furaha kwenye vitu ambavyo hatuna uwezo navyo. Na hali inachochewa sana na mfumo wa maisha wa siku hizi ya kidigitali, mf. Kwenye mitandao ya kijamii watu wengi wanajiaminisha kuwa wanamaisha mazuri, yakitajiri na yenye furaha sana lakini uhalisia ni tofauti, jaribu kuangalia ndugu jamaa na marafiki wanaotuzunguka kuna utofauti sana kati ya maisha wanayo jaribu kuonyesha kwenye mitandao ya kijamii na maisha yao ya kweli. Hivyo hali hii hupelekea watu wengine hususani vijana kutokubali maisha yao na kuanza kuishi maisha ya kuigiza.Mengi huja kwa njia tofauti tofauti katika haya maisha,Kila kinachokuja na kutokea katika maisha yako kichukulie kama njia moja wapo ya kujifunza kwako.
Maisha mazuri ni yale yakukubaliana na hali uliyo nayo,kuridhika na kile ulichonacho kile ambacho kila ufunguapo macho unakutana nacho na sio kile unachokitamani ikiwa hakipo karibu yako.