Watu wengi sana hawapendi kula kwa mama ntilie Uzi maalum kwa nini uliacha

Watu wengi sana hawapendi kula kwa mama ntilie Uzi maalum kwa nini uliacha

Tairus

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
676
Reaction score
1,056
Ndio Mimi nakula sana kwenye haya mabanda umiza yani sio kwamba napenda sema Nina sababu zangu binafsi.Sasa kama wewe ulikuwa kama Mimi ebu tupe sababu zilizokufanya uache kabisa yaan usitamani hata na kama unakula basi kuna dharura.

So hapa teremka na fact sio Maelezo ya darasani sijui kipindupindu hilo liko wazi sanaaa na sidhan kama inaweza kuwa main reason.
 
Ni wengi mkuu ule msosi huwa haubaki chelewa kidogo tuu unalala njaa
 
Wametuleta duniani, wametupa matunzo, malazi, elimu na mapenzi yote..
Tutawapenda daima..
DcDTUhmWAAE-AWf.jpg
 
Wengi kinachowakimbiza ni suala la usafi

Wakuta chapat tamu sana ila sasa usiombe kuja kushuhudia mapishi yake maana ni shiida. Kwa walioangalia kihind cha three idiots wana picha yake nzuri tu

Ukute muosha vyombo ana mafua atapenga huko asuuzia mikono kwenye maji anayooshea bila wasi wasi

Pongezi kwa mama ntilie wasafi wanaojali afya za wateja wao
 
12907244_1041715339233780_927847960_n.jpg kuna siku unakula fresh, kuna siku unakula tumbo lajaa gesi hata kupumua huwezi kama umekula ulimbo na hata ukienda haja kitu hakitoki labda umogoe mogoe nusunusu, kuna siku supu taamu, kuna siku ikifika ktk mdomo mdomo unaganda, kuna siku wali unakuwa poa kuna siku unanukia gunia, na mbaya zaidi ukiona maji yanayosuuziwa hizo sahani kwa baadhi ya vibanda umiza unahamia kwingine, uzuri wake huku unakopeshwa, unakunywa asubui unalipa jioni hata kesho, wengine ndio hawalipi kabisa
 
Kuna siku nilikula ugali wa mhogo na samaki pale ziwa nyasa mbamba bay nimeshatafuna samaki nusu kuja kumchambua nakuta funza kibao, nimetema kile chakula ni funza tupu..... Niliishia kucheka tu kwa hasira...
By the way nilimlipa na kusepa maana kutafuta riziki kugumu na pia siwezi kuacha kuufinya wa mama ntilie nikipata chance...
Hizi mboga za kutia viungo kibao huwa wanaficha harufu...
 
Kiukwel chakula cha mama ntilie sikiamin kabisa kutokana na uchafu ktk maandalizi,pia ubora wa chakula chenyewe mm siuamin kabisa,yaan kama nakula wali nyama bhc ile nyama nakuwa siiamin kabisa kama n ya mnyama halali kuliwa
Kingne tena n kupunguza gharama za chakula,ukipika gharama inapungua kwa kias fln tofaut na ukiwa unakula kwa mama ntilie na ni rahis hata kuwamanage wageni kimaakuli pale unapotembelewa ,kiukweli mm napika sana na kwa mama ntilie sili kabisa labda kwa dharura isiyokwepeka
 
Wapo mama ntilie wengine ni wasafi na wana chakula kizuri tu,

Maana wakati mwingine mazingira ya kazi yanakubana inakuwa ngumu kwenda kwako kula na kurudi hasa wakati wa mchana,hivyo hatuna budi kula kwa Mama ntilie
 
Kiukweli Mama Ntilie Vyakula vyao vingi vinaandaliwa katika mazingira ya uchafu,Vyakula vizuri ni vile vilivyo kwenye mabanda yanayoeleweka CANTEEN ......Waandaaji wa kuleta chakula nao ni wachafu,anachukua kitambaaa anafuta meza kisha anaenda kuchukua chapati na mikono bila hata kunawa na kuvaa nylon(gloves) anashika na miuchafu yake.

Ukitaka kula kwa mama ntilie nenda mida ile chakula kikiwa cha moto.
 
Maji mnayonawia mikono yana kwenda kuoshea vyombo
kuna sehemu tulikuwa tunaenda kunywa supu ya kongoro kila siku jioni kipndi tupo chuo siku ya siku mara ndo tunatoka kunywa supu mara maji ya kunawa yakawa yamejaa wanaenda kumwaga tukasema ngoja na tuone wanamwaga kweli au ndo wanapeleka wapi heeeeeee bwana we wakayamwagia kwenye vyombo vya kulia tulihisi kutapika tukaondoka wapole kama tumemwagiwa maji baridi
 
kuna sehemu tulikuwa tunaenda kunywa supu ya kongoro kila siku jioni kipndi tupo chuo siku ya siku mara ndo tunatoka kunywa supu mara maji ya kunawa yakawa yamejaa wanaenda kumwaga tukasema ngoja na tuone wanamwaga kweli au ndo wanapeleka wapi heeeeeee bwana we wakayamwagia kwenye vyombo vya kulia tulihisi kutapika tukaondoka wapole kama tumemwagiwa maji baridi
Kumbuka dumu 500
 
Kumbuka dumu 500
hahah sawa bwana wasilazimishe kufanya biashara watupe matumbo ya kuhara maana unashangaa unaenda class kesho yake unahisi kukimbiza kimbiza mwenge hivi kumbe bwana ni chemistry ya jana ya vyombo na kongoro
 
Mamalishe wengi ni wachafu!
Halafu wanakuwa na visilani hawataki kuulizwa wala kuelekezwa!
Pia wengi wao wanaamini ktk ushirikina ili kuvuta wateja!
Hata Kama kuna mtaro wa Maji machafu unaotema harufu mbaya wao hakiwasumbui kuandaa Chakula ktk mazingira machafu!
Maji ya kunawa hawayamwagi wanaoshea vyombo!
Ni risk kubwa sana kula Kwa mamalishe!
Hata Kwenye baadhi ya hotel na migahawa wengi wachafu
 
Nchi za wenzetu wana zingatia kanuni Kwamba jikoni ambako Chakula kinaandaliwa kunapaswa kuwa sehemu ya wazi ili iwe rahisi kufikika na Hata wateja ili waweze ku observe jinsi Chakula kinavyoandaliwa pamoja na usafi!
 
Sijajua hawa Mabwana na mabibi afya wa halmashauri zetu wanafanya kazi gani?
Nilizani kazi mojawapo ni pamoja na kushuhulikia maswala Kama Haya !
Ukirudi Kwenye swala la vyoo ndo usiseme [emoji108]
 
Back
Top Bottom