Watu wengi wameonewa sababu ya Swali hili la Polisi

Ndo maana unashauriwa kutomtishia mtu hadharani...ukisema Tu "ntakuonesha"...akaja mtu mwingine akamua huyo mtu...Hadi uje upatikane huna hatia usishangae miaka kumi imepita
Hii ilishawahi kumtokea mtu ninayemjua, walizinguana na mwenzie eneo la kazi akamwambia "nitakuonesha ama zako ama zangu, ndugu zako watalia na kusaga meno..." baada ya wiki mbili jamaa akavamiwa na wezi wakamuua, kila mtu akasema mshukiwa ni fulani alisema hivi na vile, alijutaaa alikaa mahabusu miaka 7 hadi kupatikana wauaji halisi,

Tujitahidi sana kuchunga ndimi zetu tukiwa na hasira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…