Watu wengi wanachanganya haya maneno mawili: best & favorite

Watu wengi wanachanganya haya maneno mawili: best & favorite

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
8,508
Reaction score
15,276
Moja ya vitu vinavyoleta mkanganyiko mkubwa kwenye mijadala ya watu ni matumizi ya maneno mawili “Best” na “Favorite.”

Unapaswa kuelewa kwamba kitu kinaweza kuwa Best kwa maana kwamba unakikubali kuwa ndicho bora zaidi, lakini kisiwe Favorite chako.

Vivyo hivyo, kitu kinaweza kuwa Best na wakati huo huo kikawa Favorite yako. Hapa ndipo watu wengi wanapochanganya hoja.

Labda nitoe mifano michache ili kuweka hoja yangu sawa.

Kwenye muziki wa Bongo Fleva, nakubali pasina shaka kwamba Professor Jay ni mmoja wa wasanii bora kabisa wa rap wa muda wote Tanzania. Lakini kwangu mimi, Albert Mangwea ndiye rapper ninayemkubali zaidi, yaani Favorite Rapper wangu wa muda wote.

Kwenye mpira wa miguu, nakubali kwamba Lionel Messi ndiye Best Player wa muda wote katika ulimwengu wa soka. Lakini kwangu mimi, Cristiano Ronaldo ndiye Favorite Player wangu wa muda wote.

Kwenye Bongo Movie, nakubali kwamba marehemu Steven Kanumba ni mmoja wa waigizaji bora kabisa wa muda wote kwenye tasnia ya Bongo Movie. Lakini pia ndiye Favorite Actor wangu wa muda wote.

Kwa hiyo, kupitia mifano hii mitatu, nadhani nimeweza kuonyesha tofauti ya Best na Favorite.

Best ni yule unayekubali kwamba ni bora zaidi, wakati Favorite ni yule unayempenda au kumpendelea zaidi wewe binafsi.

Na ndio maana mtu anaweza kusema “fulani ni Best, lakini fulani mwingine ni Favorite wangu” bila kuwa anajipinga.
 
Back
Top Bottom