Watu wengi wanapenda uchawi (shiriki)

Watu wengi wanapenda uchawi (shiriki)

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Hi,

Watu wengi hapa Tanzania wanapenda uchawi mambo ya kulogana na wanaamini ivyo na wengi washaliwa hela zao nyingi na waganga wa Dar hakuna mganga bali kuna waganga njaa ambao watatoa utabili wa uongo.

Mtu kama anataka kufanikiwa afwate au zingatia sana ushauri wa kinyota kuijua siku yako ya bahati rangi gani inavuta pesa kwako ukivaa au ukipaka nyumba yako kingine pete ya kinyota.

Acheni kuwaamini waganga wa Dar hapa.
 
Mie nilipitia visanga sana uswazi mwisho wa siku nikaamua kumuita sheikh. Ila kwa imani yangu imekuwa ni doa sana kwangu. Ila naamini kabisa wengi wanaoingia kwenye maswala haya sio kwa kupenda, mda mwingine inabidi. .
Lakini mganga unae muita ukiona ana tanguliza pesa mbele huyo mpigaji.

Nachojua dar hakuna mganga na mganga ajitangazi wale alio wahudumia ndio wanamtangaza.

Zanzibar kuna kisiwa kinaitwa tumbaty kama sikosei huko ukifika unaongea na jini uso kwa uso na shida yako inatatuliwa hapo hapo ila unatakiwa uwe na ela za zamani.
 
Mie nilipitia visanga sana uswazi mwisho wa siku nikaamua kumuita sheikh. Ila kwa imani yangu imekuwa ni doa sana kwangu. Ila naamini kabisa wengi wanaoingia kwenye maswala haya sio kwa kupenda, mda mwingine inabidi. .
Wanaingia huko KWA sababu hawana elimu ya kutosha kuhusu ulimwengu wa ROHO unavyofanya kazi pia saikolojia ya maisha ilivyo.
 
Wanaingia huko KWA sababu hawana elimu ya kutosha kuhusu ulimwengu wa ROHO unavyofanya kazi pia saikolojia ya maisha ilivyo.
Nii wachache wanatambua hualisia haupo ivyo ata kidogo kupambana na ulimwengu wa roho ni ngumu sana
 
Lakini mganga unae muita ukiona ana tanguliza pesa mbele huyo mpigaji

Nachojua dar hakuna mganga na mganga ajitangazi wale alio wahudumia ndio wanamtangaza

Zanzibar kuna kisiwa kinaitwa tumbaty kama sikosei huko ukifika unaongea na jini uso kwa uso na shida yako inatatuliwa hapo hapo ila unatakiwa uwe na ela za zamani
Ndo nakueleza sijakataa na sijui kuhusu kazi zao za Uganga ila ukweli ni kuwa wanaoenda huko wameshachoka. Kuna watu wanapambana wanaenda kila kona kutafuta majibu mwisho wa siku wanajikuta kwa waganga. .
 
90% ya watz wanaamini upumbavu huo, Ingekuwa inasaidia pasingekuwepo na masikini nchini
Ni kwasababu ndio maana wana amini
Mm kuna kipindi nililazimika kufanya maombi ya vita unaamka saa saba mpa saa nane ila vita ilikuwa kali ase shetani anapandikiza chuki hadi kwa ndugu zako nilichukiwa sana pasi na sababu nikasema ngoja niache haya maombi mpaka leo amani ipo kubwa sana
 
Wanaingia huko KWA sababu hawana elimu ya kutosha kuhusu ulimwengu wa ROHO unavyofanya kazi pia saikolojia ya maisha ilivyo.
Wewe uliyeelimika kuhusu ulimwengu wa Kirohi tusaidie sisi wenye elimu ndogo tutoe tongotongo. .
 
Wangewaua waganga na wachawi wote na kupiga maarufuku mambo yote ya shirki kama walivyofanya waarabu na wazungu thus wakapata kizazi kinachofikiri kwa kutumia akili zao thus wanamaendeleo.

Ushirikina unadumaza uwezo wa kufikiri. Ndumba upunguza uwezo wa kufikiri. Sehemu zote zenye imani hizo zipo duni sana. Pia tazama hata thinking capacity ya mshirikina yeyeto huwa ipo down sana hasa kwenye general thinking.
 
Wewe uliyeelimika kuhusu ulimwengu wa Kirohi tusaidie sisi wenye elimu ndogo tutoe tongotongo. .
Ni elimu pana na endelevu sio ya dakika moja.
Tafuta maarifa uwe huru usiwe mtumwa wa waganga na mitume na manabii.
 
Back
Top Bottom