Watu wenye kiburi wanapofanya makosa huwa hawakubali kuwa wamekosea

Watu wenye kiburi wanapofanya makosa huwa hawakubali kuwa wamekosea

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Huwa wapo tayari kufa njaa kuliko kuomba msaada.

Huwa wapo tayari kufurushwa katika nyumba zao wenyewe kuliko kwenda kuomba msaada wa dhamana kwa ndugu zao,kwa sababu huona kwenda kuomba msaada ni ishara ya udhaifu.

Wenye kiburi ni wabinafsi sana kuanza kufanya mapenzi na wenza wao. Wana vichwa vikubwa sana vya kuweza kumwomba samahani mwenza wao. Hupendelea talaka kuliko kwenda kwa mshauri wa ndoa kupata ushauri kuhusu mizozo yao.

Wapo tayari kufukuzwa kazi kuliko kwenda kuomba msamaha kwa bosi. Huwa hawawezi kukiri kuwa kuna mtu mwingine bora zaidi kuliko wao. Kwao ni heri zaidi kukaa bila kazi kuliko kuonekana wakienda kutafuta kazi kwa mtu.

Kiburi chao huharibu maisha yao, kazi zao, ndoa zao, afya zao hatimaye kuwapeleka kuzimu. Biblia inasema "Kiburi huja kabla ya anguko". Mithali 16:18.

Unyenyekevu sio kuonyesha mahitaji yako katika uwanja wa umma - na kuulizia misaada kwa kila mtu.
Unyenyekevu ni kutambua mapungufu yako na kisha kuomba msaada kutoka kwa wale wanaweza kukusaidia.

Unyenyekevu ni kukiri makosa yako na kuomba msamaha unapokosea.

Unyenyekevu ni kutambua uwezo wa wengine. Biblia inasema.. "Mungu huwapinga wenye kiburi lakini huwapendelea wanyenyekevu". Yakobo 4:6

Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom