Watu wenye Single Room: Leo ngoja tuwasaidie kupangilia Chumba chako

Watu wenye Single Room: Leo ngoja tuwasaidie kupangilia Chumba chako

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
/* insert salam here */

Wengi tumewahi kuishi au tunaishi kwenye single room. Leo tupeane tips z kufanya ghetto lako liwe safi na la kuvutia kwako na kwa wageni.

[Tips zitatofautiana kutokana na size ya room, kipato (tutajitahidi kuweka basic), aina ya room (self au sio self), etx]

1. Size ya Room.

Wakati unatafuta room ya kupanga na dalali, kingezo kingine ongezea kiwe size. Room ikiwa empty inaonekanaga kubwa ila ukianza tu kuweka kitanda, utaona kama imepungua. Kua makini.

Kama umetoka kwenye room nyingine kupanga, pima room uliyotoka (kwa tape measure au ata kama au hatua) urefu na upana, kisha fananisha na unapohamia.

Jitahidi room angalau iwe mita 4.5 urefu na upanda kwenda juu.

2. Igawe room yako kwa sections.

Sawa ni room moja, lakini panga wapi pa kupikia, wapi pa kulala, wapi pa kufanya kazi (mfano mwanachuo una homework au mfanyakazi unafanya kazi zako za jioni), na wapi sebuleni.

Unaweza kuvuka mipaka kwa kuigawa physically kabisa kwa kutumia mapazia especially kama unakuaga na wageni wengi, au fenicha mfano kabati la nguo badala ya kulibana ukutani ukaliweka likawa divider ya mahala pa kulala na pahala pengine.


3. Unavyonunua vitu, consider na size.

Wengine mnaweza msiungane na mimi kwa ili, lakini sidhani kama vyema kununua friji kubwa milango minne, kabati kubwa milango 3, Jiko kubwa, Kitanda 6*6 wakati tuna single room. Itakachotokea room itakua imebanwa.

Unaweza nunua kitanda 4*6 tosha kabisa, kwanza ukilala na mwenza wako mnakua mmebanana hadi raha., friji dogo la Lita 100 mfano (mlango mmoja tosha kabisa), TV ya nchi 40 tosha kabisa, jiko la plate 2 + meza yake.. vinaweza save space, na kochi moja la 2 seats.

4. Fenicha zako ziwe zina save purpose zaidi ya moja.

Hii labda nielezee kwa mfano, badala ya kuchonga kabati la nguo, stendi ya viatu, stendi ya mikoba na stendi ya koti. Basi chonga kabati ambalo linaweza kufanya ivyo vyote kwa pamoja.

5. Usiwe na vitu ambavyo sio necessary.

Kama kuna nguo, viatu, vyombo etc hauvitumii basi gawa kwa wahitaji vinabana tu room yako bila sababu.

6. Kua msafi. Sana.

Kama unapika hakikisha unakua msafi, osha vyombo na usiache mabaki utakaribisha mende na wakiingia hawatoki hao.

Kama una room self-contained hakikisha inakua safi, kavu (maji yasituhame).

Hayo ni baadhi ya mawazo.
images (32).jpeg

Kwahiyo, mfano kuna kijana ni mwalimu wa shule ya sekondari ana single room ya self, anaishi mwenyewe (kataa ndoa) room yake itakuaje:

- Sitting Room: Kochi moja la seat mbili, TV, Showcase ya futi 4-5, subwoofer, carpet na urembo wa zianda mfano picha za ukutani, maua artificial au aquarium.

- Chumbani: Kitanda 4*6, kabati multipurpose, hanger ya mashati na makoti (not necessarily inaweza ikawa ndani ya kabati), na urembo mwingine kama picha.

- Sehemu ya kazi za jioni: Meza na kiti (office table & office chair).

- Jikoni: Jiko la plate mbili, na meza/cabinet yake (vyombo vitakaa kwenye cabinet) na Friji letu dogo.

- Bafuni ndio zitakaa ndoo, jaba, na vitu vingine.

Mfano huu hapa:

images (31).jpeg


Potezea marangi rangi hayo.

PS: Picha hisani ya Google.
 
Hiyo sasa ni taste binafsi na kila mtu na imani yake. Kwa sisi masikini issues za energy flow dah acha tu.

Sema ni jambo zuri kuzingatia, niliwahi kua katika meditation class moja jamaa walihimiza sana hi kitu.
Unaweza jikuta umelala ila ukiamka umechoka mara usipate usingizi kumbe ni mambo madogo madogo hayajakaa sawa.
 
Back
Top Bottom