Watu wenye uwezo wa Ajabu Duniani

Watu wenye uwezo wa Ajabu Duniani

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
JIONEE WATU WENYE UWEZO WA AJABU NA KUSHANGAZA

Je, unafahamu kuwa watu wenye nguvu za ajabu kuliko uwezo halisi wa kibinadamu wapo? Ni kweli watu hao wapo na wengine wanaishi hadi sasa. Ni watu ambao wana vitu vya ajabu kama uwezo, nguvu na kuwa imara madhubuti. Wafuatao ni baadhi ya watu hao

1. WIM HOF

20160329092201.jpg

Huyu ana uwezo wa kukaa muda mrefu sana eneo la baridi kali sana bila kupata madhara yoyote yale. Huyu ni mtu halisi anaweza kukaa muda mrefu sana eneo la baridi kali sana. Anazo tuzo 21 za Guinness ikiwemo ya kuoga kwenye maji ya barafu kwa muda mrefu. Huyu anaweza kukaa kilele cha mlima kilimanjaro kifua wazi kwa muda mrefu.

2. KELVIN RICHARDSON

20160329092157.jpg

Huyu ana uwezo mkubwa sana wa kuwaelewa wanyama. Ana uwezo mkubwa sana wa kufanya urafiki hata na wanyama wakali zaidi duniani bila tabu yoyote. Ana uwezo wa kuwa na urafiki na chui, simba na fisi. Huwafanya marafiki na hata kulala nao pia.

3. CLAUDIO PINTO

20160329092152.jpg

Huyu anajulikana kama MACHO YA DARUBINI. Ana uwezo wa kuyatanua macho yake kipimo cha 7mm ambapo ni kiasi cha 95% ya mzunguko wa jicho lake.

4. HAROLD WILLIAMS
Anajulikana kama MWALIMU WA LUGHA. Huyu anasifika kwa kuwa na uwezo wa kujua lugha nyingi sana duniani. Je, wewe una uwezo wa kujua lugha ngapi katika maisha yako yote? Huyu anafahamu lugha zaidi ya 58 ambazo anaziongea na kuandika bila shida yoyote ile.

Sio peke ake alie na kipaji hiki,pia wapo John Browning,Joseph Caspar na Doktar Carlos do Amaral Freire.

5. TIBETAN MONKS

20160329094713.jpg

Wana uwezo wa kuweka sawa JOTO la miili yao kwa kutumia akili au ufahamu wao.Wana uwezo qa kubadili joto la miili yao kwa kutumia akili yao tu.Wamewahi kurekodiwa wakibadili jotoridi lao kufikia kiasi cha nyuzi joto 8 za sentigredi.


6. RATHAKRISHNAN VELU

20160329094719.jpg

Anajulikana kuwa na meno ya ajabu yenye nguvu sana maarufu kama 'steel teeth'.Ana uwezo wa kuvuta treni ya mabehewa saba akitumia meno yake kuivuta kwa kutumia kamba ya chuma.Anajulikana pia kwa jina la KING TOOTH.

7. DANIEL BROWNING SMITH

20160329094722.jpg

Huyu anajulikana kama 'The rubber boy' ana uwezo wa kujipinda zaidi katika mikao mbali mbali.

8. STEPHEN WILTSHIRE

20160329094726.jpg

Ana uwezo mkubwa sana wa kukumbuka. Huyu ana uwezo wa kutazama kitu mara moja tu na kuweza kukichora kwa ufasaha kabisa. Ni maarafu sana kwa kuchora picha za miji mbali mbali kwa kuiangalia mara moja tu. Kama watu wengine hutizama mara kwa mara katika uchoraji huo, yeye hutizama mara moja tu na kuchora sehemu kubwa ya mji husika.

9.JESUS ACEVES

20160329094734.jpg

Huyu ni mtu mwenye nywele nyingi zaidi za usoni. Anapatikana katika familia ya kimexico yenye wanafamilia 24 ,huwa anazunguka duniani kuonesha watu muonekano wake huo.

10. DANIEL TAMMET

20160329094914.jpg

Ni mtaalamu sana wa mahesabu na hesabu kwa ujumla. Hufanya kwa kutumia akili yake hesabu nzito nzito tena kwa speed ya hali ya juu sana. Pia ana uwezo wa kuongea lugha saba bila shida.

11. GARRY TURNER

20160329095232.jpg

Je, ngozi yako ina uwezo wa kujivuta kwa kiasi gani? Kutana na jamaa huyu ambae ngozi yake hujivuta kama mpira. Huivuta ngozi yake kwa namna mbali mbali. Hii inatokana ngozi yake kupungua 'Collagen'

12. NOORSYAIDAH
Ni mwanamke wa kiindonesia ambae anasema kuwa mwili wake una tabia ya kuota waya kwa muda usiopungua miaka ishirini sasa.
Waya hizo huwa kiasi cha sentimita 10 hadi 20.

13. AL HERPIN
Kwa kawaida baada ya kukaa siku chache bila kulala kabisa mwili HUZIMIA.Lakini kwa mtu huyu AL, hajawahi kabisa kulala katika maisha yake na hivi sasa ana miaka 94.

Wanasayansi wanaamini kuwa inawezekana hali hiyo ilisababishwa na jeraha alilopata mama yake siku chache kabla ya kumzaa.

14. LIEW THOW LIN
Anajulikana kama MAGNETIC MAN,raia huyu wa Malaysia ana uwezo wa ajabu sana amabpo mwili wake una uwezo wa kuvuta vitu vya chuma.


20160329092201.jpg
 
John jiwe mtu pori toka chattle mabatini ndie binadamu pekee kutoka Tanzania aliyeweka rekodi ya kujua idadi ya samaki na mazalia wake katika maziwa mito na bahari,

Pia alipokua rais aliweza kuokota vichwa vya treni bandarini

Kwa Sasa ni mwendazake!
Rest in hell!


Nadanganya wadau?
Ila John kaexit kiboya sana;eti kafia hospitali ya Mzena
 
Ila John kaexit kiboya sana;eti kafia hospitali ya Mzena
mkuu siku zote madikteta uchwara hufa vifo vya kiboya Sana harafu utakuta kitu kilichomuua ndio alikua anakichukulia poa
Hata Hitler alikua anawachukulia poa warusi akajua kua strong weapon zake zitawafyeka ndani ya wiki ajabu alisota nao mbaka akajuta kuwachukulia poa pale staringard battle jeshi lake lilikua linakula kichapo na vikundi vya mademu wabishi wa kirusi mbaka akaamua atumie silaha za maangamizi
Imagine mkuu unatumia AK 47 machine gun kumuulia panya ndani kwako what a joke!
😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom