GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwa kutokufahamu Maandiko kwa usahihi, baadhi ya watu wanaamini kuwa Mungu aliwalaani watu weusi. Wanawahusisha watu weusi na utomvu wa nidhamu wa Hamu kwa baba yake.
Baada ya Hamu kumchungulia baba yake, Noah alimlaani mtoto wa Hamu. Hakumlaani Hamu, alimlaani mjukuu wake, Kanaani, ambaye ni mtoto wa Hamu.
"Nuhu akalevuka katika ulevi wake...akasema, Na alaaniwe Kanaani" Mwanzo 9:24-25.
Hakumlaani Hamu, alimlaani Kanaani.
Unaweza ukajiuliza kwamba ni kwa nani amlaani mjukuu wake (Kanaani ) asiyekuwa na hatia badala ya mwanaye (Hamu) aliyemkosea?
Jibu ni kwamba kwa kanuni za kiroho, aliyebarikiwa na Mungu halaaniki.
"Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa" Hesabu 22:12.
Baada ya gharika, Mungu alimbariki Nuhu na wanawe watatu aliotoka nao kwenye Safina.
"Mungu akambariki Nuhu na wanawe..." Mwanzo 9:1
Kwa kuwa alishabarikiwa na Mungu, isingewezekana tena kulaaniwa na mwanadamu.
Na kwa kuwa kosa la Hamu lilihitaji kuadhibiwa, huo mzigo alibebeshwa mtoto wa mwisho wa Hamu aitwaye Kanaani.
Hamu alikuwa na watoto wanne: Kushi, Misri, Putu, na Kanaani. Mwanzo 10:6
Tunaona kwamba Kushi, ambaye ndiye mtu mweusi, ana undugu wa karibu na Misri.
Kama wewe ni miongoni mwa watu wenye ngozi nyeusi, usikubali kudanganywa ukaamini kuwa mtu mweusi alilaaniwa. Aliyelaaniwa ni Kanaani, na hiyo laana ilishafanya kazi kwa uzao wa Kanaani kwa uzao wake kupotea. Kwa sasa hakuna "race" inayojinasibu na Kanaani.
Aliyelaaniwa ni Kanaani na si Kushi ambaye ndiye baba wa watu weusi!
Mungu hajawalaani watu weusi!
Nuhu hakuwalaani Waafrika!
Kwa kuwa hawakulaaniwa na Mungu wala na Nuhu, mtu mwingine awaye yote hataweza kuwalaani "Waafrika"!!!