Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

Lakini makontena yadhahabu wanayo chukua huyaoni,shibe yao njaa yako hujui
Kibaya zaidi hutaki kuikubali hali yako, kufanya tathmini yamapungufu na nguvu yako, na kuchukuwa hatuathabiti zakujikwamua
Mimi ndiye nimekubari hali yangu na kuacha kujipa moyo, kuwa hawa jamaa ni wajanja na wana uwezo kuliko sisi. Sasa baada ya kukubari hilo na kuacha kujipa moyo na sifa za uongo hapo ndipo ninatafakari nifanyeje kwenda nao sawa.
Ukipigana na mtu aliyekuzidi nguvu kutokubari kwamba kakuzidi hakukufanyi ushinde pambano kwanza kubari kuwa jamaa ananizidi nguvu halafu tafta udhaifu wake ulipo
 
Asante,mtafuta maisha,hatimaye nimemuekuelewa,, unakubali kwanza kisha unaanza kutafuta jinsi ya kupenya
 
Swali sasa udhaifu wao hawa uko wapi, na tunafanya nini collectively as a nation and continent?
 
Mkuu a
Mkuu achana nao hao. Hao ndio wanaotaka kwenda ulaya kupitia Libya. Na huwambii kitu wakakuelewa mpaka yatakapowakuta. Na wengine watazidi jipanga kwenda wakiamini waarabu wastaarabu sana
 
Mtu anaweza akapora Mali yako, wanawe akawasomesha kwa Mali yako, na wanao wakawa vijakazi wa watoto wa huyo mporaji. Je mporaji alikuwa na akili kuliko WeWe?
Asante Mwanitu, kwa watu wengine Mali ni akili hIjalishi zimepatikana vipi. Iba,uwa nk. ,cha msingi umepata basi una akili. Bila shaka ni upeo hafifu sana wa kufikiri
 
Hiyo mifupa tu, na bado, mpaka nyama tutaitafuna
 
Huwezi Toka kwenye hilo shimo kama hujitambui. Historia inakuonyesha uwezo wako ili uweze jiamini kuwa kumbe unaweza.
 
Mojawapo ya tatizo letu waafrika ni kutoku wajibishana. Viongozi huweza fanya lolote bila wasiwasi. Mchina akikamatwa na rushwa ya kiwango flani adhabu yake ni kifo, na inatekelezwa kweli. Katika hali hiyo mtu utaingia mikataba ya kifisadi? Kwetu unaachiwa ufaidi Matunda ya dhulma, bila kujali athari kwa Jamii. Hosp zinakosa dawa watu wanakufa, mwizi anapeta tuu.
 
Huwezi Toka kwenye hilo shimo kama hujitambui. Historia inakuonyesha uwezo wako ili uweze jiamini kuwa kumbe unaweza.
Hiyo historia gani ambayo haipo ni ya kuokoteleza... hata hizo jamii za wetu weusi zilizoko Australia, India bado wanaishi maisha ya zama za mawe.
Kuna kisiwa kiko kwenye bahari ya Hindi kiko kwenye miliki ya nchi ya India inaishi jamii ya watu weusi na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia kwa maana serikali ya India imeweka zuio kutokana na sababu kwamba wanashambulia kila mgeni anayeingia japo mara kadhaa watu kadhaa eamejaribu ku interact nao lakini imeshindikana.
Wenyeji wa kisiwa hicho mpaka leo 2018 wanaishi kwa kukusanya matunda, hawavai nguo wako zama za mawe na katika uchunguzi ni kama hata hawatumii moto.
Nenda Australia kaangalie maisha ya hao wenyeji wa kiafrika bado wanaishi maisha ya zama za ajabu sana..
Leo hii mnatoka huko mnadai Mwafrika alikuwa juu kiuwezo kimaendeleo kuliko Mzungu ama kweli ni kituko maana jamii zote zilizowahi kuwa juu historia yake haijawahi kufutika hata kwa hira. Wahindi historia yao ipo, wachina ipo, Wairaq ipo hata falme na nchi za kiafrika zilizowahi kujitutumua kama Egypt, Ethiopia na enzi Mansa Mousa historia ipo.
Tuache kujipa moyo tupambane tu kama wenzetu wa Asia walivyoweza kupambana na kufika walipo siyo kulialia
 
Kumbe unatambua Egypt ya kale ilikuwa ya weusi. Egypt ndio chanzo cha maendeleo yote duniani. Kumbe Mkuu una macho, ila hutaki kuona Wala kusikia
 
Kumbe unatambua Egypt ya kale ilikuwa ya weusi. Egypt ndio chanzo cha maendeleo yote duniani. Kumbe Mkuu una macho, ila hutaki kuona Wala kusikia
Nielezee historia inayosema wa Egypt walifika Ulaya wakatawala huko?
Ukisoma historia utaona walikuwa na interaction na mashariki ya kati.
Kuna mtu kaongelea kuhusu chuo kikuu cha kwanza kuwa Afrika huko Mali. Hizi zama Afrika ya Kaskazini ilikuwa tayari na mahusiano na waarabu na hata tamaduni zao zilikuwa za waarabu mpaka leo. Uislamu ulikuwa umetawala tayari Afrika ya Kazini mwa jangwa la Sahara hata hao akina Mousa Musa walikuwa Waislam hata hiyo Mali empire hivyo hivyo na yaliyokuwa yakifundishwa pale ni elimu waliyopata toka kwa Waarabu na siyo Mwafrika.

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Na kwa akili yako unaamini kwama ni makosa kwao kuwa hivyo!!!!!!???
Kama ambavyo unaamini wamasai lazima wavuliwe rubega wawe Kama wewe mvaa suti,lakini hujui wahindi asili yao Ni watu weusi, na mmoja was miungu yao mikuu Shiva ji ni Mungu mweusi kabisa
Huijui maana ya maendeleo ndugu
Science na technology Ni kipengele tu,viko 72
Mtafuta maisha wewe na wenzio mnakata ushahidi was kisayansi, badala yake mnaamini weusi tunalaana, na jwahivyo mnamsubiri Myahudi ashuke kutoka mbiguni, Kisha akupelekeni huko mbiguni
 
Hata wamasai wenyewe wameadapt mema ng'ombe wanatibiwa kwa dawa, wanatumia simu.
Haiwezekani miaka yote uishi maisha ya zama za mawe halafu useme una akili... akili inabidi uitumie kurahisisha maisha kama mpaka leo unatembea km 10 kufuata maji wakati mwenzako anafungua bomba yanatoka na kumwagika wakati chanzo chake kiko km 70 away kati yenu nani ana akili?
kama mpaka leo ukitaka kupeleka ujumbe kwa mtu unamtuma mtu atembee km 50 kufikisha ujumbe wakati mwenzako in just a second amekwisha ufikisha across atlantic ocean nani mwenye akili na maendeleo hapo?
Tuache kujipa moyo hakuna kitu kinachodhihirisha maendeleo kama science na technology kwanza ndiyo ina determine level ya civilization.

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
 
Hata wamasai wenyewe wameadapt mema ng'ombe wanatibiwa kwa dawa, wanatumia simu.
Haiwezekani miaka yote uishi maisha ya zama za mawe halafu useme una akili...

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
Mkuu unamaana We We una akili sana kuliko mmasai aliyevaa lubega au Jamii ya wa san walioko Kalahari au gypsies walioko ulaya. Je unafahamu nguvu ya marekani ni multiculturalism na sio mzungu pekee? Wengine tumesoma nao hao watu, hawana cha kutisha darasani wala practical application. Kinachowasaidia ni mfumo
 
Kwanini sisi tumeshindwa tengeneza mifumo imara mnayodai inawasaidia?
Jibu jepesi ni kwakuwa hatuna maarifa.
Kama mazingira unayoishi yanakutawala umeshindwa kuyatawala jibu ni kwamba yes ambaye ameweza kutawala mazingira ana akili zaidi.
 
Asante ndugu, nimekaa marekani , Seattle miaka saba, moto wa mtafutamaisha, ndio anguko LA mweusi, yani kujidharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…