Watu wote Waliotajwa na Musiba kwamba wanamkosoa Magufuli Wameshatekwa, je nani anahusika

Watu wote Waliotajwa na Musiba kwamba wanamkosoa Magufuli Wameshatekwa, je nani anahusika

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483



















Wakuu salaam.

Watu wanao daiwa kumkosoa rais Magufuli wanakamatwa kama magaidi huku wanao wakamata wakiwa na uchu wa kuwatoa roho.

Kuna mtu anajiita Cyprian Musiba, kipindi cha nyuma alitaja majina ya watu wanaomkosoa rais Magufuli mitandaoni. Au watu wasiounga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya tano, wanapata tabu sana, roho zao zipo mkononi.

Tangu awataje watu hao, wameishi kama mashetani. Wametekwa, wamepotezwa, wameshitakiwa wengine wanapumlia mashine. (Chini nmeweka video ya Msiba akiwataja) Wote waliotajwa, style ya kukamatwa imekuwa moja. Kwanza wanatekwa kisha wanashikiliwa na Polisi.

Allan Kiluvya ambaye ni msaidizi wa Waziri mstaafu wa Mambo ya Nje ya wa Serikali ya awamu nne Benard Membe, alitekwa na baadaye kuachiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Zuberi Chembela alokanusha taarifa za kukamatwa kwa mwandishi wa habari za kichunguzi Bollen Ngetti, aliyedaiwa kukamatwa Agosti 8 2019 na kupelekwa kituo cha polisi cha Stakishari.

Lakini baada ya siku tatu Jeshi la Polisi likathibitisha kuwa linamshikilia mwandishi wa habari za kiuchunguzi, Bollen Ngetti katika Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumtukana na kumkashifu mke wake kwa njia ya mtandao.

Mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania, Erick Kabendera alidaiwa kuchukuliwa kwa nguvu na watu wanaodaiwa kuwa ni polisi nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni.

Kabendera ambaye anaandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania, ilielezwa alichukuliwa jioni Julai 29, 2019 na watu hao. Lakini Polisi wakakaa kimya huku wakisema hawajamkamata.

Mfanyabiashara wa jijini Dar, Raphael O. Ongangi anadaiwa kutekwa siku ya Jumatatu tarehe 24 Juni, 2019 na watu wenye silaha akiwa anaelekea nyumbani kwake maeneo ya Masaki.

Raphael alikuwa mshauri wa karibu wa ndugu Zitto kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.

Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wake, Mambosasa lilidai linachunguza tukio hili. Lakini baadae aliokotwa Hospitalini Kenya akiwa hajitambui.


Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti, amekamatwa kwa nguvu na watu watano ambao hawakuweza kutambulika mara moja maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaam. Akaanza kutafutwa kila sehemu bila mafanikio. Baadae Polisi wakasema wanaye bila kusema yupo kituo gani ili apelekewe Chakula na Mwanasheria. Siku ya pili yupo ndani.

ZAKARIA NDIO PEKEE ALIYEWATOA JASHO WATEKAJI

Jumamosi Juni 30, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alitoa ufafanuzi kuhusu tajiri huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Zakaria kuwa hajatwekwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Malima alisema mfanyabiashara huyo amekamatwa na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa na kufikishwa kituo cha polisi mjini Tarime kwa ajili ya kuhojiwa, akituhumiwa kuwajeruhi kwa risasi maofisa wawili wa idara hiyo.

Alisema kabla ya tukio hilo, maofisa watano wa Usalama wa Taifa walifika katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Zakaria kwa nia kujaza mafuta kwenye gari lao, “ wenzao wawili walishuka kwenye gari ghafla wakashambuliwa kwa risasi na Zakaria aliyekuwepo eneo hilo.”

"Baada ya wenzao kujeruhiwa kwa risasi, maofisa wengine walifanikiwa kumdhibiti Zakaria na kumtia mbaroni na kumkabidhi kwa polisi wanaoendelea kumhoji.”

Hadi leo Zakaria ana kesi ya kujeruhi watu kwa risasi. Ila hawajasema kwanini walienda kumkamata.

Azory Gwanda alikamatwa na watu wasio julikana hadi leo hajapatikana. Kwa mujibu wa mkewe, Anna Pinoni (35), Novemba 21, 2017 asubuhi watu wanaokadiriwa kuwa wanne wakiwa na gari nyeupe aina ya Toyota Land Cruiser walifika sehemu ambayo Azory hupatikana mara kwa mara iliyo katikati ya mji wa Kibiti na kumchukua.

Katika taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya kumchukua, gari hilo lilielekea shambani kwake saa 4:00 asubuhi na kumkuta mkewe na Azory akaongea naye kuhusu safari ya ghafla kisha kuuliza ulipo ufunguo wa nyumba yao.

Taarifa ilisema Azory alimwambia mkewe kama asingerudi siku hiyo ya Novemba 21, angerudi siku inayofuata, lakini hajapatikana tena kuanzia siku hiyo.

Ansbert Ngurumo baada ya kuona mambo yamekuwa mazito akakimbia nchi.

HOJA YANGU.

Ni njia ipi sahihi ya kukamata mtu anayetuhumiwa?.

Kwanini baada ya kukamata wanaficha ndugu?

Mafunzo yapoje kuhusu kukamata watu kama Magaidi. Mtu anakamatwa kama Gaidi.

Je, watawala wanafurahia hali hii?

Je hii ndo njia ya kiintelejensia ya kukamata watu?

Je, Polisi tuwasifie kwa kazi hii nzuri wanayoifanya? Nini kifanyike ili wajue wananchi tumechoka kukosa uhuru na amani?

Je, wasiojulikana na wanaokamata watu kama magaidi, wanaweza kufanya CCM ipe
ndwe?



Matukio haya UTEKAJI yapo well-organized. Jana nimeona gari (Toyota Land cruiser) ambayo niliitilia shaka. Nikafanya matukio yangu, tukapoteana. Tuendelee kuwa makini sana. Jamaa wapo "more than serious ". Musiba alinitaja kwenye orodha yake ya KUTEKA.. wengine waliotajwa wameendelea kutekwa na kuumizwa.. .
.
1. Semkae Kilonzo
2. Martin Maranja Masese
3. Raphael Ongangi
4. Bollen Ngeti
5. Tito Magoti
6. Fatma Karume
7. Thuwein Makamba
8. Edwin Ndeketela
9. Martin M.M
10. Allan Kiluvia
11. Ansbert Ngurumo
12. Jeffrey Smith .
.
Kwa mujibu wa “mwanaharakati huru wa kumtetea Rais Magufuli”, hiyo ni orodha ya watu anayewatuhumu yeye kumchafua Rais
.
.
Kwenye hiyo orodha, watu kadhaa wamepata msukosuko tayari. The latest target is @titomagoti .. Nani anafuata? Ukweli unaogopwa na watawala
 
Nchi hii sasa hivi wananchi wanaishi kwa hofu kuu juu ya hatima ya maisha yao, huku Jeshi la Polisi likituhumiwa kuwa wapo mstari wa mbele katika kupanga mipango hiyo na kuitekeleza........

Hivi Jeshi letu la Polisi lishaachana na wajibu wake namba moja, ambao ni kuwalinda raia na mali zao?
 
Ni maoni yangu tu maana huyu jamaa anajifanya kuwa master plan wa wasiojulikana. Akitaja mtu, then huyo mtu akapotea au kutekwa, watanzania tuungane kuandamana kumshinikiza msiba amrudiashe

Mwingine ni Mambosasa, huyu naye akiendelea kutumika kinyuma na katiba ya nchi, na ikatokea mtu ametekwa na hajulikani alipo, basi watanzania tuungane kuandamana kumshinikiza mambosasa mpaka amrejeshe.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Ni maoni yangu tu maana huyu jamaa anajifanya kuwa master plan wa wasiojulikana. Akitaja mtu, then huyo mtu akapotea au kutekwa, watanzania tuungane kuandamana kumshinikiza msiba amrudiashe

Mwingine ni Mambosasa, huyu naye akiendelea kutumika kinyuma na katiba ya nchi, na ikatokea mtu ametekwa na hajulikani alipo, basi watanzania tuungane kuandamana kumshinikiza mambosasa mpaka amrejeshe.

Ni hayo tu kwa leo.

Thubutu! Nyie pigeni ukulele JF tu iliyonunuliwa na Chadema.
 
Waraka wa Maafisa wa Staafu wa Jeshi la la Wananchi wa Uzbekistan umemzima kabisa huyu Kijana

Hata yule aliekuwa anatamba kuwa akiondoka hii miradi kuna mtu wa kuimalizia ndio huyo huyo anasema hataongeza hata siku moja madarakani kwa kuwa kuna uzbekistan wengi wenye uwezo wa kuwa Marais na pengine kuwa bora kuliko yeye

Hongereni sana Ma Comrade wastaafu!
 
Huyu mkuu wetu wa jeiefuu jamani nae apewe ulinzi maana hawa ma konyo wanaweza kumpitia asijisahau/kujiamini sana
 
Back
Top Bottom