Labda wewe si mfuatiliaji. Kila siku wapinzani mfano Zitto na akina mbowe wanaombea tupigane vita. Mh. Rais wetu alipoacha kuonekana kwa ajili ya mpumziko Mbowe alifurahi kwelikweli
Siku haya yanayotokea kwa hawa watu yakitokea kwa mtu wa karibu yako unayemfahamu ndo utajua kwanini watu wanalalamikia huu ukatili
Hata kama sio ndugu yako, ila yakitokea kwa mtu ambaye mnafahamiana au hata kama mliwahi kuongea siku moja tu lazima kuna kitu utahisi moyoni mwako
Jambo linapotokea kwa mtu wa mbali si rahisi sana kwa watu kama nyie kuhisi uchungu au maumivu ambayo wengine wanayahisi.
Ukitaka kuamini hili angalia siku kwenye habari yakitangazwa maafa au vifo vilivyotokea nchi nyingine kama Sudan au kwingineko. Mshituko unakuwa sio mkubwa! Ila siku maafa hayo hayo yatokee ndani ya mkoa au wiliya walipo ndugu zako utaona utakavyohangaika kujua kama ndugu zako wako salama
Mfano mzuri ni ile ajali ya moto Morogoro! Watu wenye ndugu, jamaa au marafiki Morogoro unadhani walikuwa na hali gani hasa walipopiga simu halafu wakawa labda hawapatikani kwasababu mbalimbali!?
Mtu anapokamatwa, halafu vituo vyote vya polisi haonekani na polisi hawasemi yuko wapi, hivi unaweza kuvaa viatu vya ndugu, wazazi, jamaa au rafiki zake ukahisi vitakuwaje? Unaweza kula chakula kikashuka vizuri?
Kwa hiyo watu wanapojitokeza kukemea na kupinga vitendo kama hivyo wanahitaji sapoti yetu na wala sio kuhamasisha au kupenda vita kama unavyodhani!
Watu kama hao wanahitaji kuungwa mkono na kupewa nguvu!
Sidhani kama Mbowe au Zitto wanaombea vita vitokee maana vita haiangalii sura ya Mbowe wala Zitto! Vita inapita na yeyeto! Lazima kwa namna moja ama nyingine vitawaathili tu!
Kudai haki itendeke sio kuchochoe vita! Kudai viongozi wafuate na kuheshimu katiba kamwe sio kuwaombea mabaya! Kudai watu waishi kwa uhuru na amani bila wasiwasi wa kutekwa, sidhani kama ni kuhamasisha vurugu!