VIONGOZI waliosimamishwa na Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wataendelea kuwa nje ya nafasi zao za uongozi hadi Mahakama ya Mkoa wa Dodoma itakapotoa uamuzi katika kesi inayowakabili.
Waliosimamishwa ni aliyekuwa Rais wa CWT, Leah Ulaya, Rais Dkt. Suleiman Ikomba, Maganga Japhet, Nashon Kidudu na Joseph Misalaba. Wote wanakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama, huku kesi yao ikiendelea kusikilizwa.
Kaimu Rais wa CWT, Shaban Ambindwile, alisema Baraza la Taifa lilifikia uamuzi huo ili kulinda hadhi ya taasisi na kuhakikisha hakuna hatua inayoweza kutafsiriwa kuwa inaingilia mwenendo wa kesi.
"Hatutaki kutangulia Mahakama. Wajibu wetu ni kuheshimu sheria na kuhakikisha taratibu za chama zinafuatwa wakati mchakato wa haki ukiendelea," alisema.
Alieleza kuwa kusimamishwa kwa viongozi hao si hukumu dhidi yao, bali ni hatua ya muda inayotokana na masharti ya Katiba ya CWT.
Kwa mujibu wa Ambindwile, baada ya Mahakama kutoa uamuzi, vyombo vya chama vitakutana kuamua hatua zinazofuata kwa kuzingatia Katiba na Kanuni za CWT.
Aliongeza kuwa chama hakitatoa maelezo kuhusu ushahidi unaowasilishwa mahakamani wala kujadili hatima ya kesi hiyo nje ya vyombo vya sheria.
Wakati huo huo, viongozi wanaokaimu wameendelea kusimamia shughuli za kila siku za chama ili kuhakikisha huduma kwa wanachama haziathiriki.
Ambindwile alisema uamuzi wa Baraza la Taifa unaonyesha dhamira ya CWT ya kuzingatia misingi ya uwajibikaji na utawala bora bila kuathiri haki za viongozi wanaokabiliwa na kesi.
Aliwataka wanachama kuendelea kuwa watulivu huku wakisubiri mchakato wa Mahakama kukamilika, akisisitiza kuwa uamuzi wa mwisho kuhusu viongozi hao utaongozwa na sheria na taratibu za chama.