Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Sakata la mtoto wa kiume (3) kudaiwa amelawitiwa na watoto wenzie Jijini Arusha, limekuwa na sura mpya baada ya kesi kushindwa kufikishwa Mahakamani kwa madai kuwa waliotenda tukio hilo hawawezi kukabiliwa na kesi ya jinai kutokana na miaka yao kuwa chini ya umri wa kushtakiwa kwa kosa hilo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo amethibitisha kuwa kesi hiyo haijafikishwa mahakamani kutokana na umri wa watuhumiwa hao kuwa mdogo kushtakiwa kwa kosa la jinai, mmoja akidaiwa kuwa umri wa miaka 5, na mwingine miaka 9.
"Kulingana na sheria za nchi watuhumiwa wale walikuwa chini ya umri wa kushtakiwa, mmoja alikuwa na miaka mitano na mwingine miaka tisa, mtoto wa miaka mitano huwezi kumshtaki kwa jinai, hilo shauri linashughulikiwa kinamna nyingine wakishirikiana na Ustawi wa Jamii" Kamanda Justine.
Aidha, Mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa mtoto wake anaendelea kujisaidia damu na amekuwa na maumivu makali huku madaktari wakimwambia hamna dawa za kuweza kumponya mtoto wake.
"Madaktari wananiambia dawa hamna zinazoweza kumponya mtoto, wananiambia labda waje madaktari bingwa, nimeshachoka" Mama wa mtoto.
Pia soma: Arusha: Mtoto wa miaka 3 adaiwa kulawitiwa