Watuhumiwa waliotaka kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) wafikishwa Mahakamani

Watuhumiwa waliotaka kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) wafikishwa Mahakamani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Watuhumiwa sita wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki leo December 06,2024, wakituhumiwa kutaka kumteka Mfanyabiashara Deogratius Tarimo katika eneo la Kiluvya Wilayani Ubungo Jijini Dar es salaam.

Waliofikishwa Mahakamani ni Bato Bahati Tweve, Nelson Elmusa, Anitha Alfred Temba, Isaack Mwaifuani, Fredrick Juma Msatu na Benki Daniel Mwakalebela.

Itakumbukwa December 04,2024 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaaam liliwakamata Watu wanane wanaotuhumiwa kutaka kumteka Mfanyabiashara Deogratius Tarimo katika eneo la Kiluvya, Ubungo Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro akiongea na Waandishi wa Habari alisema Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika Mikoa ya Dar es salaam, Ruvuma na eneo la Mbingu, Mlimba Mkoani Morogoro.

“Pia lilipatikana gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati wa tukio hilo huku ikitumia namba isiyo halisi T 237 EGE na baada ya ufuatiliaji kufanyika imefahamika namba yake halisi ya gari hiyo ni T237 ECF”


Pia, Soma: Polisi: Tumewakamata watuhumiwa waliokula njama ya kutaka kumteka Tarimo - Kiluvya
 

Mahakama ya Kinondoni, Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, kimeweka wazi dhamana ya Washtakiwa sita waliojaribu kumteka Mfanyabiashara Deogratius Tarimo, siku ya Novemba 11, 2024 katika eneo la Kiluvya Madukani.

Washtakiwa sita wote wamekana kutekeleza kosa hilo huku upelelezi ukiwa umekamilika.

Aidha, Mahakama kupitia Hakimu mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalila imetoa dhamana ya kila mshtakiwa yenye thamani ya shilingi milioni 10 ambayo sio fedha taslimu ambapo watatakiwa kusaini hati.

Washtakiwa wote wameshindwa kukidhi vigezo Vya dhamana hivyo wote wamerudishwa rumande huku watakaokidhi vigezo Vya dhamana wataachiwa huru licha ya kuwa hawatakiwi kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam, na kesi yao imeahirishwa mpaka Disemba 19/2024

Waliopandishwa kizimbani hii leo Desemba 6, 2024 ni Fredrick Juma, Isack Kileo, Benk Daniel, Bato Tweve, Nelson Elimusa, Anita Temba
 
Anitha Temba naye alitaka kumteka bwana Tarimo...
 
Back
Top Bottom