Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha likishirikiana na wananchi limewakamata vijana wanne wanaotuhumiwa kujihusisha na matendo ya wizi.
Watuhumiwa hao walitiwa mbaroni mchana wa leo katika Kijiji cha Naurei, Mkoa wa Arusha, baada ya jaribio lao la kufanya wizi katika duka moja la eneo hilo kushindikana na njama zao kugundulika.
Akizungumza wakati akiwa chini ya ulinzi katika Ofisi ya Kijiji cha Naurei, mmoja wa watuhumiwa hao ambaye ni mzaliwa wa Mkoa wa Arusha na mkazi wa Arumeru, alikiri kujihusisha na matendo ya wizi kwa takriban miaka mitatu maeneo ya stendi.
Mtuhumiwa huyo alieleza kuwa msukumo mkubwa wa kujiingiza kwenye uovu huo ulitokana na ugumu na changamoto za maisha, ingawa alikiri kuwa njia hiyo imemchosha. Wananchi walikusanyika katika ofisi ya kijiji kushuhudia tukio hilo kabla ya maafisa wa polisi kufika na gari la doria na kuwapakia watuhumiwa wote wanne kuelekea kituo cha polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi na hatua za kisheria.