Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Wakili Maduhu William ameeleza kuwa kuna mashauri mawili yanayowahusu watuhumiwa watano, ambapo katika shauri la uchomaji wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kivule, watuhumiwa wamepatikana na kesi ya kujibu. Aidha, katika shauri jingine la wizi kwa kuvunja na kuiba, kesi imeshindwa kuendelea leo baada ya shahidi wa Jamhuri kushindwa kufika mahakamani kutokana na dharura. Shauri hilo limeahirishwa na linatarajiwa kuendelea kesho, Machi 3, 2026.
Hata hivyo, watuhumiwa wote wanane wanakabiliwa pia na kosa la uhaini, ambalo Jamhuri bado inaendelea na upelelezi wake. Baada ya kukamilika kwa upelelezi huo, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo. Kutokana na uwepo wa shtaka la uhaini, watuhumiwa hao wataendelea kubaki rumande hadi hatua za kisheria zitakapokamilika.