Watuhumiwa wenzake na Mbowe yawezekana kweli waliteswa na kupigwa, lakini je hawakupanga kushiriki njama za ugaidi?

Watuhumiwa wenzake na Mbowe yawezekana kweli waliteswa na kupigwa, lakini je hawakupanga kushiriki njama za ugaidi?

Tuna mabunduki na akina nani? Tunazunguzia ishu iliyopo mahakamani,sisi ni raia . Je sheria za nchi zinasemaje?
Sheria zinasema uning'nizwe kama popo kwenye bomba la chuma na kula kichapo kwenye nyayo?? Hebu tusaidie mkuu...
 
Umesikia popote mahakamani Polisi wakikiri kwamba "Ni kweli tulikupiga Adamoo ili utupatie ukweli ambao tunaruhusiwa kisheria kuupata kwa njia yoyote?". Kama hao polisi walifanya kwa nia njema kwa nini sasa wanaidanganya mahakama kwamba hawakuwagusa bali walitoa maelezo kwa hiari yao?
Kama hujui kanuni ya Evidence extraction ungeuliza tukwambie inafanya kazi wakati gani na siyo kwenye implication evidence kama inayolazimishwa na Polisi.
Duuuh kumbe kutesa mahabusu kunafanywa kwa nia njema?? Iko kwenye PGO??
 
Makamandoo kudhalilishwa inavyoonekana kwenye kesi ndo ilikuwa main issue kwamba watu wakisikia Mbowe ametumia makomandoo basi public au watu watashituka sana lakini imekuja kinyume chake badala ya watu kuweka taharuki wao wamekuwa upande wa makomandoo kwamba pia wanastahili kufanya kazi popote maana hawapo jeshini Sasa hicho kitu naona ndo kimeweka kesi kuwa ngumu ila watu wangewalaumu makomandoo kwenda kumlinda Mbowe kama ilivyotegemewa basi mashitaka sasahivi yangekuwa na nguvu kubwa kama nguvu iliyoupande wa Mbowe ilivyokubwa.
Inashangaza kidogo maana ata Diamond na Harmonizer nao wanalindwa na watu wababe wenye mafunzo
 
Kifungu cha 29 cha sheria ya ushahidi ya Tanzania kipo wazi kabisa, kuwa mahakama haitakataa kupokea ushahidi wa mtuhumiwa kukubali kutenda kosa hata kama alipata vitisho, mateso na au bakshishi iwapo ni kweli alihusika, ila kama alipigwa na kuteswa na polisi wakageuza uongo uwe kweli hapo ndipo itakataa kupokea huo ushahidi.

Kesi ya Mbowe na wenzake inaendelea naona wafuasi wa CHADEMA wanashupaa sana kudhania kuwa watuhumiwa wenzake na Mbowe kutoa maelezo kuwa walipigwa na kuteswa itakuwa ni sababu ya kutotenda kosa. Ni wazi kuwa mtu anatakiwa akiri kosa kwa hiari kama kifungu cha 27 cha sheria ya ushahidi inavyosema.

Lakini kama akikiri kwa lazima halafu ikawa kweli alitenda kosa basi hapo kuna hatia. Je, wakati hizi kesi ndogo juu ya kesi kubwa zikiendelea na tuhuma za kupigwa na kuteswa zikiibuka, Je hawakushiriki kipanga kulipua vituo vya mafuta?

Factum probandum?
Hapo sasa..wajanja wa chadema kama wanavyojiwaza wanafikiri wakiweza kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliteshwa basi kesi imekufa. Ndio line ya uanasheria wa kilissu kuepa haki kwa mabishano kucheza na sheria badala ya kutumia uanasheria kujua haki iko wapi.
 
mi nadhani ugaidi Tanzania una maana tofauti sio ile tunayoijua
Kuna mwaka nilikuwa ufaransa nilikuwa jirani na jengo ambalo gaidi alivamia humo shughuri ulikuwa namna ya kumtoa ndani ya jengo hilo alikuwa mmoja tu ila shughuri ya kumtoa sikia kwa watu tu,walianza polisi wa kawaida kama kina kingai hawa zilikuwa zinatolewa maiti za polisi badala ya gaidi baadae kilikuja kukosi maalumu cha jeshi hata hivyo walitumia hewa ya sumu japo walifanya siri ndipo walipofanikiwa kumuua ni shughuri ilichukua masaa zaidi ya matano.
 
....wafuasi wa Chadema wanashupalia......usemi huu unaonesha upande ulioko wewe ambao ni wa mashitaka, kitendo hiki kinaondoa hadhi ya mada yako kujadiliwa kwani tayari unao uamuzi wako mfukoni.
Tatizo la kujibu kwa hisia bila kuangalia facts.
 
Back
Top Bottom