Watumiaji na Wataalamu Hawatumii HDD Tena Wana M.2 SSD, Wewe Je?”

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
136
Reaction score
292
M.2 SSD ni Nini? Fahamu Chanzo cha Kasi Mpya kwenye Kompyuta za Kisasa

Na Maleko GJ

Ikiwa kuna kitu kimoja watumiaji wa kompyuta wanataka zaidi kila siku, ni kasi. Kasi ya kuwasha kompyuta, kufungua programu, kuhifadhi mafaili, na kufanya kazi nzito kama video editing au gaming.
Na jibu la hitaji hilo linapatikana kwenye kifaa kidogo lakini chenye nguvu kubwa: M.2 SSD.

Lakini, M.2 SSD ni nini? Inatofautianaje na SSD ya kawaida? Na je, unahitaji ?

M.2 SSD ni Nini?
M.2 SSD ni aina ya diski ya hifadhi (Solid State Drive) yenye ukubwa mdogo sana, inayounganishwa moja kwa moja kwenye motherboard ya kompyuta kupitia slot maalum inayoitwa “M.2 slot.”

Tofauti na SSD za kawaida au hard disk, M.2 SSD:

➤Haitumii nyaya za power wala data

➤Ni nyembamba sana – kama kadi ya ATM

➤Ina speed ya juu mno, hasa ikitumia teknolojia ya PCIe na NVMe

M.2 SSD: Kwa Nini Inapendwa?

1. Kasi ya ajabu
M.2 SSD za kisasa zinazotumia NVMe protocol kupitia PCIe interface zinaweza kufikia kasi ya hadi 20Gbps, ikilinganishwa na SSD za SATA ambazo hufikia 6Gbps tu.


2. Ubunifu wa kisasa:
Kwa sababu ni nyembamba, M.2 SSD zinapendwa sana na watengenezaji wa laptop nyembamba (ultrabooks).


3. Hakuna nyaya, hakuna usumbufu:
Unaiweka moja kwa moja kwenye motherboard — ni rahisi, ni safi, na ni salama.

Aina za M.2 SSD

Kuna aina kuu mbili za M.2 SSD:

1. M.2 SATA SSD

➡ Inatumia interface ya zamani ya SATA.
➡ Kasi yake ni ndogo kuliko NVMe.
➡ Ni nafuu, lakini si chaguo bora kwa watumiaji wa nguvu.

2. M.2 NVMe SSD (PCIe)

➡ Inatumia njia ya PCIe na protokali ya NVMe (iliyojengwa mahsusi kwa SSD)
➡ Kasi kubwa, uwezo wa multitasking, boot time ya chini sana
➡ Bora kwa gamers, content creators, programmers, na watumiaji wa heavy software

Je, Kila Kompyuta Inaweza Kutumia M.2 SSD?

Hapana.
Sio kila motherboard ina M.2 slot.
Unapaswa kuangalia spec za motherboard yako kabla ya kununua M.2 SSD.

➤ Ikiwa unajenga PC yako au unataka kuboresha laptop yako, hakikisha inao uwezo wa kuunga M.2 — hasa PCIe/NVMe.



Kwa Nani Hii Inafaa?

➤Wanaohamisha mafaili makubwa mara kwa mara

➤Gamers wanaotaka loading speed ya sekunde chache

➤Content creators wanaofanya kazi za picha, sauti na video

➤Programmers na developers wanaotumia IDE na virtual machines

➤Mtu yeyote anayetaka kompyuta yenye mwitikio wa haraka sana

➤Kasi, Ufanisi na Ukombozi kutoka kwa HDD

Ikiwa bado unatumia HDD au hata SATA SSD, umebaki nyuma kwa kasi.
M.2 NVMe SSD ni zaidi ya storage ni msingi wa utendaji bora wa kompyuta ya kisasa.

Ni wakati wa kuboresha. Na ukifanya hivyo kwa kutumia M.2 SSD bora, kompyuta yako itakushukuru kwa kila sekunde.

Unahitaji M.2 SSD, Laptop Bora au Vifaa Vyake?

Tunapatikana kwa ajili ya kukufanikishaa ikoo hivi

Tunauza
Laptops mpya na refurbished zenye M.2 SSD

Yaani kuanzia M.2 NVMe SSDs (256GB hadi 2TB) Bei zetuu ni #kamabure

Pia tuna Laptop stands, cooling pads, external keyboards & mice

Huduma ya kufunga na kusanifu SSD/RAM/software


📞 WhatsApp: 0675 031 229
📍 Tunapatikana Dar es Salaam | Tunatuma mikoani
📦 Tunatoa ushauri wa kitaalamu kulingana na bajeti yako

Wakuu
Usibaki na kompyuta inayoanza polepole. Badilisha kasi yako anza leo na M.2 NVMe SSD.
Search me on X As @GoodluckMalekoJ
 
NI KWELI SSD NI BOR KULIKO HDD ILA KWA DUNIA YA PILI NA YA TATU BADO HDD INA MSAADA MKUBWA TU
 
Yote haya unayapata ktk matoleo mapya ya PC. Angalia mzigo mpya wa PC kutoka china.
 
Natumia SSD kwenye laptops lakini bado HDD kwenye NAS.

Mfano eight bay NAS ya 24 TB each bay ni 192 TB.

You can't get that with SSD at a reasonable cost.
 
Natumia SSD kwenye laptops lakini bado HDD kwenye NAS.

Mfano eight bay NAS ya 24 TB each bay ni 192 TB.

You can't get that with SSD at a reasonable cost.
Bingwa una host ma cloud VM humo nini ?
Hiyo ni data centre kabisa
 
Bingwa una host ma cloud VM humo nini ?
Hiyo ni data centre kabisa
Huku kwetu tatizo internet inaonekana kama ni Luxury na si basic need, tutafika huko na sisi tuta anza kuwa na NAS pia,
NB: Its possible kuwa nayo hapa bongo, ila changamoto ya umeme na Slow internet connection ni inafanya iwe Useless.
 
Hizo ziko mbili halafu kuna za 5 bay 3 na Dell Servers za 12 bay kama 6 hivi.

Kuzi organize/backup tu is a full time job.imi nikipata
Huku mtaani raia wananishangaa nimewezaje kuijaza 2Tb

Walipaswa kuiona hii
 
Nice
 
Nimeingia mitamboni hapa naanza kuhesabu mpaka naona aibu mwenyewe.
Nikiwa na hiyo capacity nang'oa kabisa na button ya delete kwenye PC

Kwangu mimi hiyo storage ni lifetime.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…