KERO Watumiaji wa Barabara ya Ipoipo - Kihonda Sekondari (Morogoro Mjini) tunaathirika na vumbi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
Watumiaji wa Barabara ya Ipoipo kwenda mpaka Kihonda Sekondari hapa Morogoro Mjini, iliharibika baad aya awali kuwa na lami, Serikali ikachimbua-chimbua kipindi Mwenge unakuja Morogoro na kuiacha hivyo.

Sasa imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hii na wafanyabiashara waliopo pembezoni, kwani inazalisha vumbi jingi sana ambalo linaathiri biashara za watu, bidhaa zinaharibika na hata mama ntilie waliopo kwenye barabara hii vyakula vyao vinakuwa si salama tena.
​
Watumiaji hata ukiwa umepanda bajaji vumbi linatimka mpaka unaweza kuhisi upo porini, Serikali haina hata uratibu wa kumwaga maji kupunguza vumbi na ukizingatia kipindi hichi ni cha kiangazi.

Tunaomba irekebishwe, inatuathiri wafanyabiashara bidhaa zetu zinachakaa kila siku kuzifuta vumbi.
​
 
Jamaa ulivyosema "Tunakula Vumbi Sana" kama vile unafurahia, unafurahia😄😄
 
Ndiyo ujue viongozi waliopo ni wa hovyo kabisa, wanauogopa na kuuheshimu mwenge kuliko binadamu anayelipa kodi inayoendesha nchi, ingekuwepo sheria ya kunyonga wahujumu uchumi na mafisadi hiyo barabara isingejengwa kihuni namna hiyo, tangu ijengwe haikumaliza hata miaka miwili ikaanza kutobokatoboka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…