Watumiaji wa gesi asilia kwenye magari wamefikiwa, wawekewa tozo ya 382 kwa kila kilo

Watumiaji wa gesi asilia kwenye magari wamefikiwa, wawekewa tozo ya 382 kwa kila kilo

Unaweza kupata elimu ya juu hadi ngazi ya Phd lakini ikakufanya ukawa mjinga zaidi ya ulivyokuwa haupo nayo. Nilikuwa nasikia watu wanasema kuwa huyu mtu elimu yake ni ya mashaka makubwa sana na kuna uwezekano kuwa ni ya kupewa, na sasa ninaweza kuyasadiki yale maneno.

Huyu mtu sijui vilitumika vigezo gani kumuweka hapo alipo, upuuzi ni mwingi sana aisee.
Hakuna mahala hapa Duniani Finance Minister akawa popular,haipogo hiyo mtakuja na Kila narrative.

Hoja ya Mwigulu Iko wazi,na Kwa kukuongezea tuu ni kwamba hiyo tozo haiwezi fika hata nusu ya bei ya Lita ya Mafuta.

Kwa hiyo ndio itafanya wewe uache gesi ukomae na Mafuta?
 
Mkuu Mwigulu is good at terrorizing the common man!! He has no clue on stimulating the economy growth!
Hiyo biashara Bado haijachanganya sana wangeipa nafasi isambae Walau nusu ya nchi ndio waanze hayo makodi haraka ya Nini?
 
Bajeti ya Mwigulu Nchemba inayosomwa leo imependekeza tozo ya Tshs 382 kwa kila kilo ya gesi asilia inayotumika kwenye magari ikiwa na lengo la kuchangia mfuko wa kutengeneza barabara na kuleta usawa kwa magari yanayotumia mafuta.

Swali langu kwa Mwigulu, kwanini ahangaike na kuleta usawa na kitu ambacho hakizalishwi nchini? Wewe unazalisha gesi halafu unataka iwe sawa na mafuta usiyozalisha, hadi baba wa demokrasia Marekani kila siku anadhibiti bidhaa asizolisha kutoka China japo kinyume na sera ya biashara huru!

Haitapunguza morali ya kuhamia kwenye gesi na ambayo inapunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagizia mafuta ambazo sasa zinatafutwa kwa tochi! Hata watu binafsi wanaoanza kuwekeza kwenye vituo vya kujazia gesi vilivyo haba wataanza kutafuta biashara nyingine kwani huku hakuna ishara njema tena.

Napendekeza waache watumiaji waongezeke, wakiwa wengi waweke tozo ndogo isiyo na athari ya chini ya tshs 100, kwasababu watakuwa wengi wakati ujao wakiichangia kidogo kidogo itakuwa kubwa kuliko kuharibu sasa na kuendelea kuhangaika na uhaba wa dola.
Kwa hiyo CNG inazalishwa Tanzania?
 
Sasa 382 ndio itafanya watu wasihamie kwenye gesi Waendelee kipa bei kubwa ya Mafuta? 😂😂

Hoja ya msingi ni hela ya Barabara imepatikana,hata kwenye Sgr kote huko Kuna tozo za kuchangia.

Ni ajabu sana hii Nchi watu wanataka vitu vizuri na hawataki kulipa Kodi/tozo 😂😂
Punguza ujinga hiyo sio hela ndogo kama unavyofikiri…kati ya jambo la kijinga kutokq kwa Waziri ni hili la kuongeza makodi kwenye gas halafu mnazunguka nchi nzima kuhamasisha watu kutumia magari ya gas huku mnaweka gharama!
Kupenda kusifia kila jambo kunqpofusha hata uwezo wa kufikiri
 
Hakuna mahala hapa Duniani Finance Minister akawa popular,haipogo hiyo mtakuja na Kila narrative.

Hoja ya Mwigulu Iko wazi,na Kwa kukuongezea tuu ni kwamba hiyo tozo haiwezi fika hata nusu ya bei ya Lita ya Mafuta.

Kwa hiyo ndio itafanya wewe uache gesi ukomae na Mafuta?
Nishati ni very sensitive na inagusa kila sekta na familia zote, ndio maana nchi zinazojielewa serikali itafanya kila linalowezekana kupunguza tax na hata kuongeza pesa(subsidy) ili kupunguza makali, alichofanya ataongeza inflation na ugumu wa maisha kwa mamilioni ya watu
 
Back
Top Bottom