Watumiaji wa iPhone acheni ushamba na ulimbukeni

Watumiaji wa iPhone acheni ushamba na ulimbukeni

Status
Not open for further replies.

Miss_Mariaah

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
2,176
Reaction score
4,979
Habari za jioni Wana JF,

Nimegundua watumiaji wa iPhone asilimia kubwa Wana ushamba na ulimbukeni.

Yani akiwa nayo atataka watu waione wajue kama ana iPhone, ulimbukeni wenyewe ni huu huwa wanaona iPhone ndo simu Bora kuliko simu zingine na kuzidharau hizi brand nyingine za simu.

Mimi si mpenzi wa iPhone kabisa ingawa uwezo wa kununua ninao Ila sipendelei napendelea Oppo natumia Oppo Reno 8 5G pro ninayo tangu 2022 ni simu nzuri Sana kimuonekano pia features zake za ndani Ni unique camera ndo usiseme iko Bomba sana.

Juzi kulikuwa na kasherehe kidogo ofisini ikafika Muda Yukawa tunapiga picha staff nikatoa simu yangu nikampa mtu atupige akatokea mwenye iPhone nanunukuu "chukua hii piga na Hii" Yule mpigaj akasema basi nitawapiga Na zote mbili. Ile iPhone picha zilitoka mbaya nyeusii Oppo yangu picha zilitoka vizuri sana watu

Waka-appreciate.

iPhone ni brand tu ile kuna simu zina feature nzuri kukiko iPhone.
 
Kawaida bidhaa fulani kuwa na status si kwa simu tu.
Hata magari, toyota ni gari reliable sana ila bado ukiwa na gari ya mjerumani au mwingereza unavimba. Hivyo kuna simu na kuna iphone. Hata marekani kuna kitu kinaitwa the blue bubble effect... Inahusu iPhone vs Android
 
Mimi binafsi si mpenzi wa iphone kabisa ni mpenzi wa samsung ila hii ya kusema kwamba wanaotumia iphone ni mashoga sijui wadangaji sioni kama imekaa sawa, mambo ya kusema kuna vitu kama simu au magari vya kiume na vya kike ni dalili ya kuwa na stress na roho za kimasikini, hao watengenezaji wenyewe sidhani kama huwa wanasema kwamba hizi wanatengenezea jinsia fulani au fulani
 
Kawaida bidhaa fulani kuwa na status si kwa simu tu.
Hata magari, toyota bi gari reliable sana ila bado ukiwa na gari ya mjerumani au mwingereva unavimba. Hivyo kuna simu na kuna iphone. Hata marekani kuna kitu kinaitwa the blue bubble effect... Inahusu iPhone vs Android
iPhone Ni brand kubwa sikatai tatizo Kwa hapa tz watumiaj wengi Wanaomoliki hiyo ni washamba Na malimbukeni sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom