Watumiaji wa simu - mambo yanayokera

Mtu anapiga simu na namba ngeni halafu anauliza "unajua unaongea na nani"khaaa hua nakereka sana
 
Unampigia mtu simu hasahasa wadada....haipokelewi......baadae kabisa anakwambia simu ilikua kwenye pochi...na hapo ni baada ya masaa matatu mbele....
 
mtu kujibu text kwa vifupi , unakuta umetuma text ndefu mtu anajibu p,k, pp, kuandika texts za msingi kwa vifupi ani dah me mtu akiniandikia p,k,pp simjibu hadi akili imkae sawa
 
Hiyo tabia ya kupiga calls kumi inakera, piga mara moja then tuma sms kama unadhani ujumbe ni wa muhimu sana.

Kukata simu katikati ya maongezi (hii mara nyingi ni kwa wapendanao), watu mkipishana kauli kidogo tu mtu anakata simu, sijui anataka abembelezwe au vipi. Ukinikatia simu katikati ya maongezi hakika hutaona call yangu.

Kupiga simu then mtu haweki sikioni, ukipokea haongei, yupo zake anapiga story, unasema "vipi upo?" Ongea basi...nakereka balaa!!
 
Namba 9 hapo. Nikupigie simu usipokee, nikutext usijibu halafu ndio ukae kimya, Hiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!! Hata ukikutana na mimi barabarani usithubutu kuongea na mimi
 
Kuna hawa wanaokosea namba basi akikupigia baada ya kupokea utasikia mpe mwenye simu niongee nae ukimwambia simu ni yangu anakomaa umpe mwenye simu yaani mbishi hataki kuamini simu ni yako.
 
Mi kuna hii ya mtu bando limemkamata hana mtu wakumpigia basi anakutafuta anakupigia afu anakuacha hewani yaani hakuongeleshi wala nn naichukia sana kwan bando ukishindwa kumaliza si uliache liende lazima ulitumie?
 
Kuna hawa wanaokosea namba basi akikupigia baada ya kupokea utasikia mpe mwenye simu niongee nae ukimwambia simu ni yangu anakomaa umpe mwenye simu yaani mbishi hataki kuamini simu ni yako.
Anapiga simu ukimwambia umekosea namba anaanza kukuhoji "kwani we nani,uko wapi" mara "basi tuendelee tu kuwasiliana"
Sasa mtu nimeshakwambia umekosea namba,mimi siyo unaemtafuta umekazana tuwasiliane na maswali kama police
 
Michepuko: unaweza kukupigia na kukuta upo kwenye kwenye mazingira hatarishi (upo na waziri mkuu kwa mfano) na inabidi uikate ile simu. Badala ya mtu kujiongeza, unashangaa anapiga tena na tena na tenaaa😀
 
hahahahahhaa
 
Mimi namba 9 nipo.... Naweza nikatoka nyumbani wanataka kuniuliza kitu au kuniagiza akianza kupiga inaita alipo.

Nimeshindwa kuacha hii.
 
Namba 6 ni kiboko
 
kuna x wangu mmoja nilimtumia sms kumjulisha kuwa wale wadogo zake walio kuwa wana tafuta kazi,awajulishe wanitafute niweze kuwapa maelekezo juu ya nafasi za kazi,mara paa mwanaume ananipigia simu na kunitumia sms kuwa mke wa mtu anauma...nikaishia kucheka na kumjibu kuwa ..unaumia nini wakati kitumbua unacho karibu..si utafune ,,unakaa muda wote umeangalia simu ya demu wako.badala ya kushughulika.
 
Unatumia hela demu wako mpaka tena umpigie kujua kama kaiona ndipo atajibu nimeiona Asante.
Mama nikimtumia hela muda huohuo anaunga bando la mia 500,anakupigia utasikia "Asante mwanangu nimeiona ubarikiwe sana baba yangu, Mungu abariki za mikono yako najivunia kukuzaa wewe na wadogo zako wamefurahi sana.
Nakupenda mama,wadogo zangu wa kike wafundishe huo ukarimu kwa wanaume zao .
 
mtu kujibu text kwa vifupi , unakuta umetuma text ndefu mtu anajibu p,k, pp, kuandika texts za msingi kwa vifupi ani dah me mtu akiniandikia p,k,pp simjibu hadi akili imkae sawa
Harafu unakuta ni mwanaume [emoji3][emoji3]kuna washikaji zangu kama wawili huwa wananikera sana,unampa maelezo marefu kabisa na ya msingi harafu anakujibu k,p
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…