Watumiaji wa simu - mambo yanayokera

Watumiaji wa simu - mambo yanayokera

Mtu anapiga simu na namba ngeni halafu anauliza "unajua unaongea na nani"khaaa hua nakereka sana
 
Unampigia mtu simu hasahasa wadada....haipokelewi......baadae kabisa anakwambia simu ilikua kwenye pochi...na hapo ni baada ya masaa matatu mbele....
 
mtu kujibu text kwa vifupi , unakuta umetuma text ndefu mtu anajibu p,k, pp, kuandika texts za msingi kwa vifupi ani dah me mtu akiniandikia p,k,pp simjibu hadi akili imkae sawa
 
Hiyo tabia ya kupiga calls kumi inakera, piga mara moja then tuma sms kama unadhani ujumbe ni wa muhimu sana.

Kukata simu katikati ya maongezi (hii mara nyingi ni kwa wapendanao), watu mkipishana kauli kidogo tu mtu anakata simu, sijui anataka abembelezwe au vipi. Ukinikatia simu katikati ya maongezi hakika hutaona call yangu.

Kupiga simu then mtu haweki sikioni, ukipokea haongei, yupo zake anapiga story, unasema "vipi upo?" Ongea basi...nakereka balaa!!
 
Namba 9 hapo. Nikupigie simu usipokee, nikutext usijibu halafu ndio ukae kimya, Hiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!! Hata ukikutana na mimi barabarani usithubutu kuongea na mimi
 
Kuna hawa wanaokosea namba basi akikupigia baada ya kupokea utasikia mpe mwenye simu niongee nae ukimwambia simu ni yangu anakomaa umpe mwenye simu yaani mbishi hataki kuamini simu ni yako.
 
Mi kuna hii ya mtu bando limemkamata hana mtu wakumpigia basi anakutafuta anakupigia afu anakuacha hewani yaani hakuongeleshi wala nn naichukia sana kwan bando ukishindwa kumaliza si uliache liende lazima ulitumie?
 
Kuna hawa wanaokosea namba basi akikupigia baada ya kupokea utasikia mpe mwenye simu niongee nae ukimwambia simu ni yangu anakomaa umpe mwenye simu yaani mbishi hataki kuamini simu ni yako.
Anapiga simu ukimwambia umekosea namba anaanza kukuhoji "kwani we nani,uko wapi" mara "basi tuendelee tu kuwasiliana"
Sasa mtu nimeshakwambia umekosea namba,mimi siyo unaemtafuta umekazana tuwasiliane na maswali kama police
 
Michepuko: unaweza kukupigia na kukuta upo kwenye kwenye mazingira hatarishi (upo na waziri mkuu kwa mfano) na inabidi uikate ile simu. Badala ya mtu kujiongeza, unashangaa anapiga tena na tena na tenaaa😀
 
Michepuko: unaweza kukupigia na kukuta upo kwenye kwenye mazingira hatarishi (upo na waziri mkuu kwa mfano) na inabidi uikate ile simu. Badala ya mtu kujiongeza, unashangaa anapiga tena na tena na tenaaa😀
hahahahahhaa
 
Mimi namba 9 nipo.... Naweza nikatoka nyumbani wanataka kuniuliza kitu au kuniagiza akianza kupiga inaita alipo.


Nimeshindwa kuacha hii.
 
Habari zenu..
Naomba ieleweke haya ni maoni yangu binafsi. Katika kipindi cha miaka 10 nilichotumia simu nimekutana na mambo haya yanayonitibua nyongo.

1. Kupiga simu kwa fujo. Kuna watu akili zao sijui ziko vipi, akipiga simu hujapokea muda huohuo anapiga tena, anaweza kupiga hata mara tano ndani ya muda huo huo ukija unakuta missed call tano zimepishana sekunde tu unaweza kudhani labda alikuwa na jambo la dharula kumbe walaa ukimtafuta anapiga stori tu. Sijui huwa wanawaza nini kwa kweli....ukimpigia mtu simu hajapokea vuta subira huwezi kujua kwa nini mtu hajapokea.

2. Unapiga simu kwa namba ngeni halafu unasubiria hadi uulizwe we nani..unapiga unaanza kujiongelesha tu wakati unajua namba yako ngeni kwangu. Siku zote mimi nikipiga simu kwa mtu ambae najua hana namba yangu naanza salamu then najitambulisha ndio naaza masuala mengine.

3. Mtu kujifanya mtabiri - anajua kile mpigaji anataka kusema. Unaweza kumtuma mtu dukani kununua sukari, unakumbuka baadae kuwa na mkate unahitajika...unampigia aliyeenda dukani anunue na mkate anafikiri unataka kumhimiza afanye haraka basi yeye anakaza mwendo kurudi nyumbani.
Au mfano mmekubaliana na mtu kuwa mtapitiana kwenda mahali akiona simu yako anajua ndio unamwambia twende anaacha kupokea anakazana tu kujiandaa. Pokea simu usikie nasema nini basi

4. Wazee wa kupaniki. Kuna mtu ukitaka kumvuruga asiwasiliane tena na wewe akuoigie then umuulize 'naongea na nani'? Utashangaa mtu anakata simu, kwa nini usiulize imekuwaje uwe huna namba yangu? Mwingine atajitahidi kuuliza 'kwa hiyo namba yangu umefuta sio'? Kuna mambo mengi yanatokea, kuna kupoteza au kubadilusha simu na namba zikapotea, pia naweza kuwa nimefuta ndio what's wrong about that? Si ndio ndio kazi ya kitufe cha delete?

5. Hivi mtu akikupigia simu ni lazima useme 'haloo' au mimi mshamba? Mtu kila siku mnawasiliana ila kila ukimpigia anapokea simu halooo anakaa kimya anasikiliza duuh mimi nikipokea simu nimeshajua huyu nani moja kwa moja naanza kumsemesha. Nimeshajua huyu anayepiga ni espy moja kwa moja naanza mambo... hata nikisema haloo naunganisha na salamu.

6. Kuna wale wa kubipu kwa sms. Mtu anatuma sms vipi Khantwe...ukute hapo huna hata salio unaamua kuzama Nipige tafu ili ujibu sms maana huwezi jua mtu ana shida gani unamjibu 'safi Heaven Sent mzima wewe'? Halafu ye hakujibu ng'ooo utasubiria hadi kifurushi ulichojiunga kina expire. ..watu wa aina hii mbinguni hamuendi nawaambia.

7. Wapo wale wa kupigia ndugu zao kupitia simu za watu daah hawa nao..mtu anachukua simu ya mtu anampigia sijui hawara yake halafu hasemi kwa mwenye simu dadek mnasababisha ugomvi usio na maana. Unashangaa unapokea simu haloo naongea na nani? Mama we si ulinipigia nimekuta missed call yako halafu ukiangalia we hujapiga simu yoyote unabaki kusema mbona mimi sijapiga na kama wote wawili mmekosa simile mnaweza kujikuta mnarushiana matusi ya nguoni.

8. Kuna wale wapenzi mnaopokeleana simu aisee sijui nani kawaambia kupokeleana simu ndio mapenzi. Mtu umejiunga zako kifurushi dakika tano una shida ya muhimu may be ya kikazi au unampigia ndugu yako anapokea mtu siye ukimuuliza kama mhusika wa simu yupo anaanza kukuhoji kwani we nani? Hapo umepiga simu muda wa kawaida hata sio usiku...unaongea kuja kupokea mwenyewe voda wameshachukua chao.
Wengine wanawaachia watoto wapokee simu aisee mimi nikupigie apokee mtoto sitokaa nikupigie.

9. Wapo wale ambao siku zote wako mbali na simu yaani katika simu unazopiga kwake asilimia 90 hazipokelewi na hata baadae hakutafuti halafu siku nyingine ukimpigia sababu ni zilezile, nilikuwa kuoga, niliisahau simu nikaenda kazini, kuna rafiki yangu mmoja ndio zake aisee huwa nachukia sema namvumilia tu coz she has been my best friend tangu tupo primary.

Na nyie wadau ongezeeni ya kwenu mimi yangu ni hayo. Muwe na usiku mwema
Namba 6 ni kiboko
 
kuna x wangu mmoja nilimtumia sms kumjulisha kuwa wale wadogo zake walio kuwa wana tafuta kazi,awajulishe wanitafute niweze kuwapa maelekezo juu ya nafasi za kazi,mara paa mwanaume ananipigia simu na kunitumia sms kuwa mke wa mtu anauma...nikaishia kucheka na kumjibu kuwa ..unaumia nini wakati kitumbua unacho karibu..si utafune ,,unakaa muda wote umeangalia simu ya demu wako.badala ya kushughulika.
 
Unatumia hela demu wako mpaka tena umpigie kujua kama kaiona ndipo atajibu nimeiona Asante.
Mama nikimtumia hela muda huohuo anaunga bando la mia 500,anakupigia utasikia "Asante mwanangu nimeiona ubarikiwe sana baba yangu, Mungu abariki za mikono yako najivunia kukuzaa wewe na wadogo zako wamefurahi sana.
Nakupenda mama,wadogo zangu wa kike wafundishe huo ukarimu kwa wanaume zao .
 
mtu kujibu text kwa vifupi , unakuta umetuma text ndefu mtu anajibu p,k, pp, kuandika texts za msingi kwa vifupi ani dah me mtu akiniandikia p,k,pp simjibu hadi akili imkae sawa
Harafu unakuta ni mwanaume [emoji3][emoji3]kuna washikaji zangu kama wawili huwa wananikera sana,unampa maelezo marefu kabisa na ya msingi harafu anakujibu k,p
 
Back
Top Bottom