Watumiaji wa Tecno

Watumiaji wa Tecno

commm

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2019
Posts
1,709
Reaction score
1,963
Hivi ni kwa nini watumiaji wa tecno simu zenu huwa hazina update ya android version?

Yaani kama ulinunua simu labda ina android 7, ili upate android 8, itakulazimu wewe kununua toleo jingine la simu yao yenye hiyo android 8.

Wakati wenzenu wa Samsung wao wanafanya ku-update tu na kupata version mpya

Hivi mshawahi kuuliza hata uongozi wa kampuni yao labda kuboresha matoleo yao ili kwenda na kasi ya teknolojia?
 
Hatupendi kukaa na simu moja kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kampuni yenyewe wanatujua watumiaji wao
 
hii H5 ninayotumia niliitupa uvunguni nikawa natumia H6 na yenyewe screen imevunjika na fundi anataka 30

h5 haina uwezo wa kuwa na Twitter na ndicho ninachomisi hasa yule mpuuzi Kigogo2014
 
🥃 simu ya tecno, inaweza kujituma meseji kwa wake zako imejiandika "nyie mafala tu"
Siku moja simu iko mfukoni ikajimute. Kila aliyepiga ilikuwa inamtumia ujumbe, nimebanana kwasasa tuma ujumbe, kuna kazi naifanya (hii ni moja ya meseji nilizosave kama quick response). Nilikuwa safarini siku hiyo. Nilikuta calls zaidi ya 30 zikionesha zimekuwa received na meseji kibao. Nilichoka baada ya kufungua meseji, mama anauliza kazi gani inayofanyikia kwenye basi ilhali sina kifaa tofauti na simu. Wife nay kivyake, pata picha jinsi gani nateseka na tekino wereva.
 
Ikianza kuvheza sindimba ndio utaijua. Mara imewasha torch mfukoni mara vile. Siwezi irudia hiyo kampuni

Dumelang
 
Back
Top Bottom