A
Anonymous
Guest
Ningependa kufikisha malalamiko kuhusu changamoto kubwa wanayokutana nayo watumiaji wa vituo vya mabasi ya mwendokasi katika njia ya Kimara, hususan wanapovuka Barabara ya Morogoro kwenda au kutoka vituoni.
Baada ya upanuzi wa barabara, umbali wa kuvuka umeongezeka, lakini katika baadhi ya maeneo hakuna alama zinazoonekana wazi kuwaonya madereva kuhusu vivuko vya waenda kwa miguu. Pia, hakuna mifumo ya kutosha ya kuwasaidia abiria kuvuka kwa usalama, kama vile taa za kuongoza waenda kwa miguu, matuta ya kupunguza mwendo au madaraja ya kuvukia.
Kutokana na hali hiyo, waenda kwa miguu hulazimika kusubiri kwa muda mrefu hadi magari yapungue ndipo wavuke. Wakati mwingine tunalazimika kuvuka huku magari yakipita kwa mwendo kasi, jambo linalotuweka katika hatari kubwa ya kugongwa. Hali hii ni mbaya zaidi kwa wazee, watoto, wajawazito, watu wenye ulemavu na abiria wanaowahi usafiri.
Tunaziomba mamlaka husika, ikiwemo TANROADS, LATRA, DART, Manispaa ya Ubungo na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, kufanya ukaguzi katika vituo vyote vya mwendokasi vilivyopo kwenye njia ya Kimara na kuchukua hatua zifuatazo:
Mamlaka husika, tafadhali chukueni hatua haraka kabla hali hii haijasababisha madhara makubwa.

- Kuweka alama kubwa na zinazoonekana wazi za vivuko vya waenda kwa miguu.
- Kuweka taa maalumu za kuongoza waenda kwa miguu katika maeneo yenye magari mengi.
- Kuweka miundombinu kama taa au alama za kuwalazimisha madereva kupunguza mwendo wanapokaribia vivuko
- Kutoa elimu na kusimamia kikamilifu sheria zinazowataka madereva kuwapa nafasi waenda kwa miguu.